hivi huwa wanachukua makapi kwa sababu chama hakina uwezo wa kuzalisha ngano yake wenyewe?
sijaona bado mantiki ya kuchukua makapi kisha ukayapa thamani ya zaidi ya ngano yenyewe hata kama yanafaida.
Mkuu, nani kawaambia CCM ndiyo yenye chujio lisilo na matunde tena yakuwekwa kwa makusudi ili wale wembamba kifedha wadondoke na wale wanene kifedha wabaki?Bahati mbaya huwezi kupata dona kutoka ktk ngano! Ktk ngano hakitupwi kitu hata zile pumba za majani yake hupewa farasi wakala.
ndio maana wachambuzi wa siasa wanasema Dr Slaa anafaa lakini ataundaje dola kwa watu wa kuazimaazima bila ya kuwajenga wafuasi wao muda marefu? Kila siku CHADEMA wanasema CCM ni mafisadi lakini ajabu wanapokea wagombea CCM bila hata kuwajua kwa undani.Bado naamini CHADEMA ni chama kizuri lakini hakijakomaa kukipa nchi. Kama leo Dr Slaa atashinda kuwa Rais hana watu wa kuunda serikali kwani kama CHADEMA wanathubutu kuokoteza wagombea wa nafasi mbalimbali bila mpangilio bila shaka wataokoteza watu wa kuunda serikali yao. Tuwape muda wa kujijenga zaidi.
Tafsiri ya makapi ni pana sana. Ukipembua mchele yale mapumba yanayotupwa ambayo huwa ni kiasi kidogo na kubaki mchele mwingi hii ni tafsiri moja. Pia ukichukua udongo na kupembua dhahabu ambayo ni kidogo na kutupa udongo ambao ni mwingi hapa makapi ni huu udongo.
Hawa watu wanaohama CCM ni dhahabu, hawakutumia rushwa ndio maana hawakupata kuteuliwa CCM. Ukitaka ubunge kupitia CCM ni lazima uwe tajiri (yaani uwe na hela nyingi za takrima). kama huna hutapata haijarishi wewe ni Malechela au Ntagazwa.
Mkuu, nani kawaambia CCM ndiyo yenye chujio lisilo na matunde tena yakuwekwa kwa makusudi ili wale wembamba kifedha wadondoke na wale wanene kifedha wabaki?
Nani kasema mchujo wa CCM ndio mchujo wenye ubora, na kila ambaye akuchaguliwa na CCM basi ni makapi?..........This is a skewed thinking. Sawa na kufikiri kuwa kwa vile Chadema haijawahi kuwa serikalini basi ikiingia itabidi iweke mpaka wakurugenzi wapya ambao ni wa Chadema.
kuna ubaya gani kuwa unafikiri unaweza ku-workout issues zenu na mkeo, then dakika ya mwisho anakwambia mbona mi sina time na wewe, what do you do? keep crying? go get a life!!
Hivi chama kinakomaa namna gani? Yaani kiishi miaka 50 au ni mfumo bora! CCM inayoitwa imekomaa mbona sioni siasa za ukomavu? Tunaingia ktk mtego wa CCM kila wakati kujigamba wamekomaa wakati hawana hata itikadi ya kueleweka kwa miaka 10 iliyopita.
Kinachotakiwa ni personalities na mfumo mzuri wa kuwapata viongozi. Hata CCM hili limewashinda. Ndo maana hata vibaka wanachaguliwa kiurahisi tu! Mtu anakata kadi wiki ya kuchukuwa fomu, anashinda na baadaye ni waziri. Au chama kinamkomaza?
Pale Malawi, chama kiliundwa na Rais akiwa madarakani na leo hii hakuna taabu ukilinganisha na waliokuwepo kabla yake.
Slaa akishinda hawezi kushindwa kuongoza dola maana sioni tofauti ya ubora wa hao walioko CCM ukilinganisha na CHADEMA.
Tukubali kwamba vyama na siasa zetu zitaendelea kuwa za kitoto mpaka tutakapokuwa na mifumo imara ya nchi bila kujali ni CCM, CUF au TLP anayeshika ikulu. Hili halitahitaji chama chenye miaka 90, itakuwa ni bahati kama tutampata Rawlings wetu.
Wewe ndugu mbona unaota mchana? Nani alikuambia kwenye siasa za Afrika kura 'kuamini sera' za chama ndio ujiunge!! Unajua hizi siasa za kwenye mtandao zinawapoteza wengi.Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM- ndipo wapewe nafasi hizi.
Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.
There we go again, stressing personalities over policies. Strongman complex.
Wewe ndugu mbona unaota mchana? Nani alikuambia kwenye siasa za Afrika kura 'kuamini sera' za chama ndio ujiunge!! Unajua hizi siasa za kwenye mtandao zinawapoteza wengi.
Ukiingalia Afrika na viongozi wetu wakiwa ktk mikutano yao hakuna anayeonyesha kuwa ana matatizo ya policies. Kila nchi policies safi na zenye matumaini kama National anthems zetu zilivyo.
Lakini ktk serikali zetu hizi nguvu za utendaji kila mtu anafahamu ziko ktk mtu mmoja. Hakuna jinsi kama huyo mtu mwenye nguvu hatapatikana mwenye niya njema.
Hata Europe ilikuwa hivyo ndo maana kila nchi ina shujaa wake aliyeweka misingi imara.
Utawaangaliaje wakiwa nje acha waingie wapewe kazi zitakazoifanya Chadema ione ubora wao.Huwezi kujua hili kwa hakika bila kuwapa muda wa kutosha kujionyesha true nature yao ndani ya upinzani. Inawezekana wamekuwa mzigo hata CCM ndiyo maana wakatoswa.
Ndiyo maana wengine tunapendekeza wapewe muda mpaka 2015 waangaliwe.
Ina maana wewe unakubaliana na hizi siasa zisizofuata sera ?