Serikali tatu ni fumbo kubwa sana,binafsi hii hoja kupitishwa na tume naiona kama vile ni hatua kubwa sana ya kipimo cha uzalendo.Hapa naona hesabu hii rahisi wamewachia watanzania wenyewe waamue nini cha kufanya kwani hesabu hiyo ni je
a). 1+1=2?
b). 1+1=3?
c). 1+1=1?
d).Kwanini jibu ni "a" , "b" au "c"?
d).Nini muundo wake kama jibu ni "a" ,"b" au ,"c"?
My take: 1+1=1 (mistari miwili iliyo sambamba kamwe haikutani na unapojaribu kuikutanisha kutoka umbali uliopo kati yao unapata mstari mmoja mmyoofu).Hii inawezekana tu iwapo vikwazo vyote vitabashiriwa kama havipo.(ukanda,udini,ukabila,uvyama na ubaguzi wa rangi).
Tukumbuke iliyotolewa ni rasimu (pa kuanzia ili kumalizia),na swali lako linaweza kupata jibu iwapo tu maswali hapo juu yataweza kujibiwa.Kama ulisoma hisabati hapo zamani jaribu kuzikumbuka angalau zile hesabu za "LOGIC".