Makao Makuu ya Serikali ya Muungano yatakuwa wapi?

Khakha

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
2,983
1,009
wadau amani iwe juu yenu.

nimekuwa nikijiuliza kuwa since ikulu ya magogoni ndio ilikuwa makao ya serikali yetu tukufu ya TANGANYIKA (najivunia TANGANYIKA kurudi tena) sasa swali kuu ni kwamba, je makao makuu ya serikali ya muungano yatajengwa wapi? je ni dar, zanzibar au chumbe?
 
Makao makuu ya serikali ya Tanganyika yanapaswa kuhamia dodoma haraka, hii ikulu ya sasa ni makao makuu ya serikali ya muungano..Nilishatoaga maoni kuwa ikulu ihame..
 
Makao makuu ya serikali ya Tanganyika yanapaswa kuhamia dodoma haraka, hii ikulu ya sasa ni makao makuu ya serikali ya muungano..Nilishatoaga maoni kuwa ikulu ihame..

We vipi bana, kwani maoni yako ni sheria.

Mimi sitaki hata kuusikia huo muungano wenyewe, wa nini mimi?!

Hawa Wapemba tapeli, oooh mkiungana na sisi mtapata karafuu kwa ajili ya kujichua, mimi si siku moja nikajichua na salimia, weeeee, siamini kama nimeweza kuzaa. Hawana maana hawa, wache wende zao wallah!
 
wazanzibar wamesema kama ni ikulu ya muungano watatoa nyumba ya vyumba viwili sebule ya rais kufanya kazi zake na chumba cha kulala.
 
Huu Muungano una faida gani kwa Bara?

Gharama za kuendesha Muungano ni bara kutoa 97% na Visiwani kutoa 03%???

Kwa nini mateso yote haya?? Sii bora tu tutengene kila mtu ajiunge Afrika Mashariki kivyake???

Je Ikulu ya Muungano Bara watajenga wenyewe??

Why all these?
 
Hapo ndipo ukweli tuakapojua kuwa serikali tatu maana yake ni kuvunja muungano. Hata kama rais wa muungano atabaki magogoni na yule wa tanganyika kuwa Dodoma; ukweli ni kuwa atakuwa hana nguvu tena. Kila mshiriki wa muungano ataangalia mambo yake mwenyewe isipokuwa tu pale tunapokuwa na mambo kimataifa. Wananchi watajishughulisha zaidi na yale yanayoendeleza usitawi wa serikali ya ama Tanganyika au Zanzibar,
 
Kama kuna Jambo Gumu ambalo serikari unaona shida kulitekeleza basi ni kuhamia Dodoma ! Hakuna dalili ya kuhamia Dodoma kabsa ! Rasimu ya katiba mpya haijaupa umuhimu wa suala la kuhamia Dodoma . Watu wengi hawataki serikari tatu ili kuepuka gharama za kuziendesha lakini Nina Imani Wakihakikishiwa kwa asilimia zote Kuwa serikari tatu zitawezesha kuhamia Dodoma na kuliepusha jiji na foleni lazima watazikubali.lakini kinyume na hapo hawataki serikari tatu
 
Gavana wa ZNZ abaki huko na Gavana Wa Bara abaki magogoni Rais ahamie Dodoma
 
wadau amani iwe juu yenu.

nimekuwa nikijiuliza kuwa since ikulu ya magogoni ndio ilikuwa makao ya serikali yetu tukufu ya TANGANYIKA (najivunia TANGANYIKA kurudi tena) sasa swali kuu ni kwamba, je makao makuu ya serikali ya muungano yatajengwa wapi? je ni dar, zanzibar au chumbe?

Kutokana na viongozi wa juu wa SERIKALI niliobahatika kuongea nao wamependekezwa kujengwa MOSHI KILIMANJARO. Tunawakaribisha sana KILIMANJARO KWENYE FURSA ZA UWEKEZAJI.
 
wadau amani iwe juu yenu.

nimekuwa nikijiuliza kuwa since ikulu ya magogoni ndio ilikuwa makao ya serikali yetu tukufu ya TANGANYIKA (najivunia TANGANYIKA kurudi tena) sasa swali kuu ni kwamba, je makao makuu ya serikali ya muungano yatajengwa wapi? je ni dar, zanzibar au chumbe?

Mkuu naona makao Makuu ya serikali ya Muungano yatakuwa Dar. Halafu Makao makuu ya Tanganyika yanakuwa Dodoma ndani ya Ikulu ya Chamwino. Haya mambo yapo wazi kabisaaaaa.
 
wadau amani iwe juu yenu.

nimekuwa nikijiuliza kuwa since ikulu ya magogoni ndio ilikuwa makao ya serikali yetu tukufu ya TANGANYIKA (najivunia TANGANYIKA kurudi tena) sasa swali kuu ni kwamba, je makao makuu ya serikali ya muungano yatajengwa wapi? je ni dar, zanzibar au chumbe?

kp06062013.jpg
 
Serikali tatu ni fumbo kubwa sana,binafsi hii hoja kupitishwa na tume naiona kama vile ni hatua kubwa sana ya kipimo cha uzalendo.Hapa naona hesabu hii rahisi wamewachia watanzania wenyewe waamue nini cha kufanya kwani hesabu hiyo ni je
a). 1+1=2?
b). 1+1=3?
c). 1+1=1?
d).Kwanini jibu ni "a" , "b" au "c"?
d).Nini muundo wake kama jibu ni "a" ,"b" au ,"c"?

My take: 1+1=1 (mistari miwili iliyo sambamba kamwe haikutani na unapojaribu kuikutanisha kutoka umbali uliopo kati yao unapata mstari mmoja mmyoofu).Hii inawezekana tu iwapo vikwazo vyote vitabashiriwa kama havipo.(ukanda,udini,ukabila,uvyama na ubaguzi wa rangi).

Tukumbuke iliyotolewa ni rasimu (pa kuanzia ili kumalizia),na swali lako linaweza kupata jibu iwapo tu maswali hapo juu yataweza kujibiwa.Kama ulisoma hisabati hapo zamani jaribu kuzikumbuka angalau zile hesabu za "LOGIC".
 
Alhamdulillah, Katika kitu cha maana zaid kilichofanyika kwenye uongoz huu ni kurudisha Serikali huru ya Tanganyika tukiwa kwenye mchakato wa kuvunja muungano huu wa nguvu za giza, hakuna haja ya kuingia Gharama za kujenga makao makuu ya Serikal itayokufa muda mchache baada ya kuzaliwa, Jakaya aruhusiwe kugombea urais wa Tanganyika as alikuwa wa Tanzania!
 
Hivi watanganyika hamjawahi kusikia muungano wowote kuvunjika duniani mpaka leo muone maajabu?jipangeni kwa tanganyika yenu na ndio taifa lenu,mkataa kwao mtumwa.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom