BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,150
Posted Date::2/21/2008
Makao Makuu Jeshi Tanzania yakatiwa maji, yadaiwa Sh276milioni
*Dawasco wapigwa marufuku kuingia eneo la jeshi bila kibali
Na Pius Rugonzibwa
Mwananchi
MAKAO Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyoko Upanga jijini Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine nyeti ya kijeshi yalikatiwa maji kuanzia jana.
Katika operesheni maalum iliyoendeshwa na Kampuni ya Usambazaji Maji Dar es Salaa, (Dawasco) jana, maeneo kadhaa nyeti yanayomilikiwa na jeshi kama Hospitali ya Lugalo, kambi ya Lugalo, nyumba za maafisa wa jeshi zilizoko Muhimbili, Band Coy, Area J, na 361 Mzinga KJ yote yalikatiwa maji.
Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Biashara wa Dawasco, Raymond Mndolwa, huduma ya maji ilikatwa jeshini kufuatia kushindwa kulipa ankara ya maji yenye thamani ya Sh276 milioni iliyolimbikizwa tangu mwezi wa nane mwaka jana.
Mndolwa alisema kuwa kwa muda mrefu jeshi limekumbushwa juu ya deni hilo, lakini katika mazingira yasiyoeleweka mpaka sasa deni hilo halijalipwa.
Alisema kuwa mwezi uliopita Dawasco ilitoa notisi iliyofuatiwa na kumbusho maalum (reminder) iliyopelekwa wiki iliyopita, lakini bado jeshi likaendelea kukaa kimya.
Tuliwapa notisi, tukawaongezea na kumbusho maalum bado hawakuelewa somo, sasa tumeamua kukata maji ili kuwaonyesha wateja wetu wengine kuwa hatubagui katika kuwahudumia na katika kuwakatia maji wanaokaidi kulipia bili,� alisema Mndolwa.
Kundi la wafanyakazi wa Dawasco walioongozana na waandishi wa habari walishuhudia kazi ya kung�oa maungio ya maji kwenye nyumba za maofisa wa jeshi eneo la Upanga.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Dawasco, Badra Masoud zoezi kama hilo lilikuwa linaendelea kwenye maeneo yote yaliyotajwa na lingeendelea kwa siku nzima jana.
Awali Mndolwa alimweleza mwandishi wa Mwananchi kuwa juhudi za kuzungumza malipo ya deni hilo ili wasikikatie maji kwa chombo hicho nyeti yalifanyika mara kadhaa, lakini haukuwa na mafanikio yaliyopatikana.
Ndugu wa maofisa waliobaki nyumbani walishuhudia zoezi la chapuchapu likitekelezwa na kufumba na kufumbua maafande hawakuwa na maji.
Baada ya watu waliokuwa katika nyumba hizo kupiga simu, maafisa wa jeshi walifika na kuwasomba baadhi ya mafundi wa Dawasco hadi makao makuu ya jeshi ili wakaeleze nani aliwatuma kukata maji kwenye nyumba za jeshi.
Mashuhuda wanaeleza ilikuwa heka heka kwenye nyumba hiyo iliyoko ploti 289 Upanga ingawa hakuna vurugu zilizosababisha maumivu kwa watumishi hao.
Kundi la waandishi lililoshuhudia zoezi hilo liliamua kufuatilia makao makuu ya jeshi ambako kwa takriban saa tatu mahojiano yalikuwa yakiendelea baina ya mafundi hao na maofisa wa jeshi.
Mafundi hao Moses Leo Bakagya, Wendelin Komba, Bonaventure Mtesigwa, Kassimu Mumba na Zawadi Nganyanga inasemekana walihojiwa ili wamtaje aliyewatuma kukata maji lakini walishindwa, ndipo Mndolwa aliende kuokoa jahazi.
Habari zinasema kwamba baada ya Dawaco kumaliza kazi yao maafisa wa jeshi walitoa tahadhari kwa mafundi wa kampuni hiyo kuingia tena kwenye maeneo ya jeshi bila kibali.