Ndugu zangu,
Kwa jinsi mambo yanavyoendelea sasa ni dhahiri Zitto Kabwe kazidiwa nguvu muda mfupi na Maalim Seif na wenzake.Tangu Maalim Seif na wenzake watangaze kujiunga na ACT maamuzi yote yanafanyika Vuga.
Imefika pahala Zitto huitwa ghafla tu Unguja na kuitishwa kikao ambacho hupitisha maamuzi bila kuwepo wajumbe wa ACT toka Tanganyika. Ni dhahiri sasa udhibiti wa masuala ya fedha upo chini ya mshauri Mkuu wa Chama hicho ndugu Seif Sharif Hamad.
Kundi la Sefu wamejifunza baada ya Prof.Lipumba kuwazidi kete ni dhahiri wanataka kuziba mianya yote kisheria,kiufundi na kifedha.Katika kipindi hiki ambacho Zitto yupo "excited" na Siasa za Zanzibar huku akiwa amesaini "blank check" lazima vijana wa Seif watatumia kipindi hiki kumbana hasa ukizingatia Zitto kaamua kuwatenga wenzie kutoka afisi ya Taifa ambao walisota pamoja.
Nimwambie maneno machache ya wahenga "ajizi nyumba ya njaa",hakika unanaswa na mtego wa kawaida sana ambao huenda baadae ukahitaji msaada wa Chama Dola.