Makanisa ya kiroho yana mchango gani kwenye kusaidia jamii?

Viongozi wa makanisa haya ni aibu tupu mbele za Mungu
Yesu angekuwa hai leo hii asingedai achangiwe pesa za Vogue au helicopter
 
Inasikitisha mno kuona mnajilimbizia mimali wakati waumini ni maskini ajabu
 
Mshagadanganywa hahahaha,,,,shtukenii muwe mnasali nyumbani inatosha ,Kanisani mizinga ya kutosha,mmeshashindiliwa imani hizoo mmekua vipofu,stukeni
 
jambo hili linasikitisha sana, kodi hawalipi lakini mchango wao kwenye jamii ni kama hakuna...ukiisikiliza Radio kama Praise Power 99.1 FM ndo utapata kichefuchefu jinsi wanavyomtukuza mmiliki Dr. Askofu Mkuu Mhe. Mama yetu Getruda
Njoo huku kwetu arachuga usikilize radio moja inaitwa ngurumo ya upako. Ni kero sijawahi ona...watangazaji wake utadhani wamelogwa vile , ni kumuabudu nabii wao 24/7. Unaweza sikiliza siku nzima usisikie habari za yesu au mafundisho yoyote yanayohusu maadili.
Ni mwendo wa utukufu kwa nabii wao na kampeni za kutoa hela. So boring..na ipo kitapeli wazi wazi kabisa. Sijawahi waelewa wafuasi wa huyu jamaa. Pole zao, bora nibaki na msimamo wangu. Haya makanisa mengi ni wapotoshaji live kabisa!
 
Mshagadanganywa hahahaha,,,,shtukenii muwe mnasali nyumbani inatosha ,Kanisani mizinga ya kutosha,mmeshashindiliwa imani hizoo mmekua vipofu,stukeni
Kweli huwa sielewi inakuaje mtu akadanganywa wazi wazi kabisa. Namshukuru huyu mungu wangu ninae mwamini hajanifanya niwe mpumbavu kiasi hicho.
 
Walokole mnajengwa katika misingi ya kutoa hukumu kwa wengine na kuwaona wasio faa mbele za mungu, mmejengewa misingi ya kujiona mpo karibu zaidi na mungu kuliko madhehebu mengine , na hayo yote si makosa yenu bali ni makosa ya wanao wahubiria hayo.
Mnatoa sana hukumu kwa wasio amini katika madhehebu yenu, nimesali madhehebu hayo kwa miaka mingi hivyo ninacho kiongea sio cha kusimuliwa nayajua kwa kina.
Sitaki kuwasema walokole wote ila kuna wale wenye tabia ya kujiona watakatifu.... yaani mtu ukiwa sio mlokole au ambaye haupo kwenye kanisa lao utapata shida
 
Ni tatizo la watu wanaosoma Biblia lakini hawaielewi na badala ya kuifuta wao wanataka Biblia iwafuate wao,mengine yamekuwa yakitapeli watu
 
Hahaha naona watu mmeamua kufunguka wanaosema et kazi ya Yesu ilikuwa kiroho peke yake Bali hata kimwili aliweza kulisha kundi LA watu kwa mikate na samaki mpaka wakasaza au wanatumia maandiko gani, wachungaji wanaishi kufalme kabisa wakat wananchi wao wanaishi kwa shida wakati huo huo kashfa nyingi zinawahusu kutembea na wake wa za waumini wao huku waumini wakiwa kama mazombi na kuwateteaa, kuna baadhi yao wanaishi kawaida ila hawa wanaojiita wakubwa ni majipu
 
Mengi ni machanga kiuchumi,yapo mengine yameanza kutoa huduma za kijamii kama afya na elimu,na hii ni baada ya kujitathmini uwepo wake hapa ulimwenguni pamoja na uchanga wake.
 
Makanisa yote yanatakiwa yawe ya Kiroho ndugu...kuna kanisa lisilo la Kiroho? Michango yake kwa jamii ni mikubwa...hata kuhubiri watu waache kutenda dhambi ni mchango pia kwa jamii..
 
Yapo yaliyoanza kufanya kama RC,KKKT,KAT na KMT kama vile FPCT,TAG na EAGT.
 
Watu walikuwa majambazi wanabaka watu...wanaua watu Leo wamebadikishwa kabisa...kuna watu walikuwa wanavunja ndoa za watu leo wamebadilishwa kabisa..kuna watu walikuwa wachawi Leo wamebadilishwa kabisa....Mkuu umeshasema makanisa ya kiroho yanadeal na roho. .. Mambo wanayofanya ni makubwa sana Mkuu...hata hivi ulivyo Leo umekaa na kuandika hivi wapo watu wanakuombea kwa baba....

Achana na walokole ..
Wana Mungu wale..
Wanaomba wale..
Wana nguvu wale..
Wana msaad wale..

Huyu mtoa post ni mtoto wa dawa ( in Gwajima's voice)
 
Back
Top Bottom