Makanisa ya kilokole

Makanisa ya kilokole

Uandishi wako unapotosha maudhui.
Kama huamini hilo, waza pia mtu atayekuja na thread yenye kusema kuna utofauti gani kati ya Ukristo (ambao kutwa kuwaaminisha watu kuwa ukiwa mkristo na ukifa utakwenda mbinguni) na huyo Paul Mackenzie wa Kenya?
 
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa huyu mhubiri kuwahubiria watu wafunge mpaka kufa ili wamwone Yesu, wakati yeye anakula kwa siri. Dini zimetumika vibaya kurudisha nyuma maendeleo ya Africa
 
Haya makanisa yetu ya lilokole hapa TZ, yana tofauti gani na kanisa la huyo Paul Mackenzie wa Kenya. Yule aliyesababisha watu kufariki Moshi kwa ajili ya kukanyaga mafuta alichukuliwa hatua gani?
Ukitaka kanisa lako lisonge mbele, wajaze waumini wako hofu ya Mungu isivyo kawaida, waambie watoe kila walicho nacho maana maisha ya Duniani hayana maana yoyote - watishie kwamba wakati wowote Yesu anarudi kuwachukua walio wake je wao wapo tayari?. Baada ya hapo kusanya mapato.

Jitahidi kutumia kina mama kwa ushawishi - kanisa lako litapaaa na mapato yanapanda kila uchao.
 
Inabidi serikali iregulate haya makanisa. Infact sio makanisa ni Culty.
Watu wanakua maskini kwa kupeleka hela zao zote.
Watu wanakufa kwa kuacha dawa zao za hospitali na kuamini maombi yatawaponya.
 
Haya makanisa yetu ya lilokole hapa TZ, yana tofauti gani na kanisa la huyo Paul Mackenzie wa Kenya. Yule aliyesababisha watu kufariki Moshi kwa ajili ya kukanyaga mafuta alichukuliwa hatua gani?
Hakuna tofauti. hukumbuki mwamposa aliuwa watu kwa kumwb mafuta na kuwambia wakanyage,kila mmoja anastahili yake ya kafara..
 
Huyo wa Kenya ni cha mtoto, hapa Tz wengi wameshakufa japo wanatembea. Kumuanika mtu juani, usafiri wa shida, mtoto ana malaria ila unampeleka kuombewa, yote hayo ni mauwaji ya kimyakinya.
 
Inabidi serikali iregulate haya makanisa. Infact sio makanisa ni Culty.
Watu wanakua maskini kwa kupeleka hela zao zote.
Watu wanakufa kwa kuacha dawa zao za hospitali na kuamini maombi yatawaponya.
Sijui ni lini mamlaka zitachukua hatua maana Hali inazidi kuwa mbaya. Labda hili la Kenya litupe Somo tuamke.
 
Haya makanisa yetu ya lilokole hapa TZ, yana tofauti gani na kanisa la huyo Paul Mackenzie wa Kenya. Yule aliyesababisha watu kufariki Moshi kwa ajili ya kukanyaga mafuta alichukuliwa hatua gani?
Walokole wote wakamatwe na makanisa yao kuchomwa moto, hatuhitaji kizazi kisichojitambua.
 
Haya makanisa yetu ya lilokole hapa TZ, yana tofauti gani na kanisa la huyo Paul Mackenzie wa Kenya. Yule aliyesababisha watu kufariki Moshi kwa ajili ya kukanyaga mafuta alichukuliwa hatua gani?
kuna makanisa ya kilokole, na kuna makanisa ya mitume na manabii feki. tofautisha hayo, kuna makanisa mengi sana watu wanaamini ni ya kiokole lakini wala sio, na hata kwenye umoja wa makanisa ya kilokole hayapo. hao wote wanauza mafuta na maji, sio walokole.
 
Back
Top Bottom