Makanisa kuwekwa wi-fi nchini Ujerumani

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,672
Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.
Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina "Godspots".
Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000.

Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la French Cathedral eneo la Gendarmenmarkt na kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial Church.
Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani nan je ya kanisa.
Wanaotumia huduma hiyo watalakiwa na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii na maelezo ya kidini.
Lakini baadaye, wataweza kuchakura chochote watakacho katika mtandao wote.
 
lengo nini hasa maana nahisi utafika wakati watu watakua wanatumiwa neno kwa simu tv na kuambiwa wachangie sadaka kwa tigo pesa ama m-pes ahalafu ibada ndiyo imetoka hapo
 
Back
Top Bottom