Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,104
- 5,665
Hivi Kazi ya Makamu wa Rais katika nchi yetu ni nini? inawezekana hii ikana ni issue ya kuadress kwenye Katiba yetu pia? Huwa najiuliza ni kwa nini Makamu wa Rais haonekani kwenye ulingo wa kisiasa, kwa mfano ni kwa nini hatumuoni akijishughulisha na kulisimamia baraza la mawaziri kama ambavyo tunamtegemea Rais kufanya? Kwa nini simsikii japo akijifaragua kupambana na Rushwa? au basi tatizo la kuporomoka kwa kiwango cha Elimu nchini? au tatizo la Ajira? au ulinzi na usalama? au swala la kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu? au tatizo la umeme? au utoroshaji wa wanyama hai kwenda nje ya nchi? au mfumuko wa bei? au mchakato wa kuandika katiba mpya? au tatizo la vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua? au Malaria basi?
Au katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ni wakati Gani Makamu wetu wa Rais alipata kuassume full presidential position?
Nauliza maswali haya kwa dhati kwa sababu nafasi hii ni ya kikatiba, na tunatumia mapesa mengi sana kuimaintain.
Chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuna wizara mbili, Wizara ya Muungano na wizara ya Mazingira, Hasa Makamu wa Rais wa sasa, mbona sijaona jitihada zake binafsi za kujishughulisha na chokochoko za Muungano hata baada ya kushambuliwa na mawimbi makubwa makubwa? au hiyo wizara ya mambo ya muungano inajishughulisha na mambo gani haswa?
Kuna wizara ya mazingira, mbona haonekani japo kwa usanii basi kushughulikia swala la uchafuzi wa mazingira unaofanywa na viwanda hapa nchini? sijawahi kumsikia akizungumzia uchafuzi wa mazingira uliosababisha athari kubwa kwa wakazi wa ny'amongo, majuzi kuna hoteli imebainika kumwaga kinyesi baharini iko oesterbay, mbona hakuweka japo neno?
Tatizo ni personality yake au ndio tatizo lile lile la CCM?
Nashukuru kwamba, baada ya post hii, kama sio coincidence
Wizara ya Mazingira iliyo chini ya ofisi ya makamu wa rais imeifungia hotel ya Double Tree Hilton kwa sababu za uchafuzi wa mazingira ya bahari ya hindi.