Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) umefunguliwa rasmi tarehe 14 Mei, 2024

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
825
521
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) umefunguliwa rasmi tarehe 14 Mei, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwashukuru washiriki wa Mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kushiriki Mkutano huo Mkuu wa Majeshi Duniani. Aidha, Dkt. Mpango aliwakumbusha washiriki wa mkutano huo umuhimu wa michezo katika kuleta Amani duniani, Umoja na Mshikamano na Urafiki kupitia Diplomasia ya Michezo.

Mkutano huo mkuu wa Baraza la Michezo Duniani unahudhuriwa na nchi wanachama 82 na wajumbe 290 kutoka sehemu mbalimbali duniani, unafanyika kwa mara ya pili nchini Tanzania baada ya miaka 30, umehudhuriwa pia na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi na kumkaribisha Mgeni rasmi, alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kwake kuhudhuria na kufungua Mkutano huo. Waziri Tax pia aliwafikishia wajumbe wa mkutano huo, salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Waziri Tax amewatakia washiriki wa mkutano huo, ushiriki mwema wa Mkutano Mkuu na kuwataka wajumbe kufurahi uwepo wao Tanzania.

Viongozi wengine wa Kitaifa waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Majeshi Duniani ni pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Khamis Mwinjuma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Othman, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Neema Msitha, pamoja na Makamanda Wakuu mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
 

Attachments

  • 20240516_094948_InSave_9.jpg
    20240516_094948_InSave_9.jpg
    70.7 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_10.jpg
    20240516_094948_InSave_10.jpg
    79 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_11.jpg
    20240516_094948_InSave_11.jpg
    73.5 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_0.jpg
    20240516_094948_InSave_0.jpg
    86.1 KB · Views: 3
  • 20240516_094948_InSave_1.jpg
    20240516_094948_InSave_1.jpg
    104.3 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_2.jpg
    20240516_094948_InSave_2.jpg
    110.3 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_3.jpg
    20240516_094948_InSave_3.jpg
    100.3 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_4.jpg
    20240516_094948_InSave_4.jpg
    81.5 KB · Views: 3
  • 20240516_094948_InSave_5.jpg
    20240516_094948_InSave_5.jpg
    140.8 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_6.jpg
    20240516_094948_InSave_6.jpg
    66.9 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_7.jpg
    20240516_094948_InSave_7.jpg
    78.3 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_8.jpg
    20240516_094948_InSave_8.jpg
    54.6 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_12.jpg
    20240516_094948_InSave_12.jpg
    62.6 KB · Views: 2
  • 20240516_094948_InSave_13.jpg
    20240516_094948_InSave_13.jpg
    70.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom