Makamu wa Rais: Viongozi wanolazimisha penzi ofisini washughulikiwe

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa umma wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kulazimisha mahusiano ya kingono kazini, hasa kwa waandishi waendesha ofisi (makatibu mahsusi).

Dkt. Mpango alikuwa akizungumza katika mkutano wa 12 wa Chama cha Waandishi Waendesha ofisi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika mkoani Arusha leo Mei 15, 2025.

“Wapo viongozi wanaojiita mabosi wachache wenye tabia mbaya wanatumia nafasi zao vibaya, jambo la aibu. Baadhi yao wanalazimisha penzi maofisini na waandishi waendesha ofisi. Wengine ni watu wa hovyo, sijui kwa nini bado hawajaacha kazi”. amesema Dkt. Mpango

Aidha, Dkt. Mpango ameeleza kusikitishwa na taarifa kwamba baadhi ya waandishi waendesha ofisi hunyimwa fursa au hata posho iwapo hawajakubali mahusiano yasiyofaa na viongozi wao.

“Wengine wanawanyima fursa mpaka wapewe penzi. Hata posho wanawekewa kauzibe. Haya hayakubaliki kabisa”. ameongeza Dkt. Mpango

Makamu wa Rais amewaagiza Mawaziri, Makatibu Wakuu, na viongozi wengine wa juu kutowafumbia macho watumishi wenye tabia hizo, na kuhakikisha kuwepo kwa utaratibu wa siri wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya waandishi waendesha ofisi.

M
 
Hao wako kila kona
Natamani sheria iboresheshwe na kuongezewa makali ili Washughulikiwe kwa ukubwa na ukali zaidi
 
View attachment 3334685M
Huyu VP angejua wanavyoomba hela kwa wanaume hao wadada huko maofisini sidhani kama angethubutu kuongea hayo anayoona ni kuwatetea hao wanawake.
 
Kuna jimama lilinitaka kimapenzi likawa linaniambia ni vitu vya kawaida mapenzi kutamalaki maofisini. Liliniteka kimapenzi tukaenda mgahawa wa hadhi kula nyama chama choma na pombe nikaliambia pombe sinywi, nikanywa soda tu na nyama. Mara likaniambia twende benki nikadro fedha, tukaenda, likazama ndani ya benki mi nikabaki nje. Nikasepa zangu bila kuliaga maana nilishajua mpango wake ni kwenda gesti nikalinyandue. Kesho yake likaja kazini na kunisema vibaya kwa wenzagu huku linatumia code kuwa lilijilengesha kwangu ila nikampotezea na kusema mi ni themosi iliyopoa mpaka wenzangu wakagundua kisa kizima. Mapenzi maofisini yapo sana tu hadi kwa wake na waume za watu ligi ni moja
 
Mapenzi ni sehemu ya maisha chamsingi hakuna anayebakwa maana yake ni utashi na makubaliano ya watu wawili.

Hili jambo ni gumu tuwe bize na wanafunzi wanataka kuwa bize na watu wazima kweli. VP umefeli sana.

Kutetea mwanamke inabidi uwe kichaa au mwanaume fala. Unajua vile wanamaauzi hawa kazini ukimkazia kashasema unamtaka ndio maana unamsumbua kumbe ni lizembe kwenye kazi.
 
1-Mwanamke akimkubalia mwanaume(anaweza akawa vice versa)atanyamaza.
2-Akilazimishwa atatoa malalamiko.
NB;Umakini uwepo ili udhaifu wa ushahidi usitokee na kusababisha watu kuonewa kisheria.
 
Back
Top Bottom