Makamu wa Rais kulala kwa RC, Itifaki inasemaje?

Makamu wa Rais kulala kwa RC, Itifaki inasemaje?

Kwani kuna ikulu ndogo nyingine zaidi ya kwa mkuu wa mkoa..
Unaubishi ubishi wote kumbe hujui tofauti ya ikulu ndogo na anako ishi mkuu wa mkoa? Hapa mwanza ikulu ndogo iko kapripoint na mkuu wa mkoa anaishi kwa machemba karibu na hospital ya mkoa au jiji. Na ofisi ya mkuu wa mkoa iko kamanga karibu na mahakama kuu kanda ya mwanza.
 
Ujinga tu unasumbua awamu hii, wanabana matumizi ya lazima na kuacha matumizi ya anasa ya magari yao!!

Acheni kuigiza na kuleta mbwembwe katika kuongoza watu, tunahitaji maisha bora kwa kila Mtanzania.

Eti kubana matumizi ili hali mnagawana bilioni 2.7 kwa mambo ya kiuendawazimu.

Eti nilibeep tu kugombea urais simu ikang'ang'ania!!...... Hahahaha nchi hii kwa mwendo huu iko siku mwendawazimu atakuwa kiongozi wa nchi. Ccm urais wameufanya kuwa rahisi
Hata mbowe alirudisha shangingi la KuB au umesahau mkuu,ina maana mwenyekiti wetu wa maisha ni mjinga kurudisha lile shangingi?
 
Habari wana ndugu,

Naomba wataalamu wa itifaki wanipanue mawazo na kuniongezea uelewa kuhusu Makamu wa Rais kulala nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa na sio Ikulu ndogo.

Nauliza kwa nia njema tu.
Labda fafanua hiyo ikulu ndogo iko wapi na Mkuu wa Mkoa anaishi wapi?
Huyo John Mongella anaishi nyumba yake binafsi?
 
Mkapa akiwa rais alishawahi lala kwa RC Arusha
Mkuu ni kwamba Rais ama Makamo wa Rais akienda mkoani anaweza kulala Ikulu ndogo kama ipo na pia anaweza kulala kwa Mkuu wa Mkoa. Nyumba ya mkuu wa mkoa inabadilika na kuwa Ikulu. Wenyewe watakuambia ila nadhani mkuu wa mkoa huhama.
 
Back
Top Bottom