Makamu niliyofika nilipenda niwaone baba na mama wapo pamoja kama nyie wenzangu

Machuchu

JF-Expert Member
Mar 31, 2017
1,260
962
Habari zenu wakuu.

Nasikitika sana na naumia sana moyo wangu si kwa mabaya ila nasikitika sana kuwaona wazazi wangu wawili wametengana toka nikiwa mdogo hadi sasa na mimi nina mtoto. Nilijiuliza sana maswali bila kupata majibu na hasa niliumia niwaonapo wenzangu wakiwa na baba zao na mama zao hasa wakiwa OUT. Sijui ugomvi wao kiundani, ila tu mama ukimuuliza lawama ni kwa Baba. Ila sasaivi baba yangu anajuta sana kumpoteza mama, na mimi sina mapenzi nae baba kwa ujumla maana alivyomuacha mama hata mapenzi na sisi na wadogozangu wa2 yakawa yamepungua kabisa kwa kua alikuwa na mwanamke mwingine na tulikua tunaishi wote.

Ilifika stage hadi siku ya graduation yangu namaliza Mama wala Baba hakuwepo wakati wote wapo Dar es Salaam na mimi nikiwa nikisoma hapahapa, Nakumbuka nililia sana wenzangu walifurahi mimi nilikua darasan pekeyangu nalia tu.

LEO NIMEONA HII PICHA NIMEKUMBUKA MBALI SANA
picha.jpg

(Hawa wazee wako kwenye ndoa miaka 60 sasa. Ghafla bibi akapata stroke. Mzee wake anampenda sana anamuuguza na Hosp wamemruhusu kulala naye kumpa moyo. )
 
Mwenye Enzi Mungu alikutenga makusudi! Msikilize maana yeye ndiyo kila kwako!
 
Daaaah aisee mambo ya familia haya basi tu.....nikajua ni mimi tu kumbe tupo wengi, mie toka form two naishi na mshua tu kaoa mama mwingine na mama mzazi kapanga mtaa mwingine inauma sema basi tu.....nishamwachia mungu maana nlipigana kwa uwezo wangu kuwarudisha waishi pamoja nyumbani lakini sikuweza at the end mie nlikuwa mtoto wa mwisho kilichosaidia nlikuwa nasoma boarding but nkirudi nyumbani ndio hivyo nakosa kukaa na wazazi wote kwa pamoja....nw nimemaliza chuo, mzee kastaafu kapata hela mama analazimisha arudi, home kuna mama mwingine yaani ni shida.

Nakuomba ukaze moyo ndugu haupo peke ako mie nishazoea nahisi tu kawaida. Japo inaumiza sana.
 
Shukuru wametengana ndugu yangu maana kupitia kutengana kwako naamini utakuwa umejifunza mengi kuhusu maisha ya ndoa, umuhimu wa wazazi kuishi pamoja hadi kifo, furaha wa watoto kuona wazazi wao wakiwa pamoja, maumivu na shida wanazopitia watoto pindi wazazi wao wanapotengena. Hivyo kwa kifupi through divorce of your parents, you gonna be a good dad, caring and loving one.
Personally, niko kwenye same situation lakini nina furaha kubwa sana kwa hili coz nimejifunza mengi sana ambayo bila wao kutengana nisingejua.
 
Habari zenu wakuu.

Nasikitika sana na naumia sana moyo wangu si kwa mabaya ila nasikitika sana kuwaona wazazi wangu wawili wametengana toka nikiwa mdogo hadi sasa na mimi nina mtoto. Nilijiuliza sana maswali bila kupata majibu na hasa niliumia niwaonapo wenzangu wakiwa na baba zao na mama zao hasa wakiwa OUT. Sijui ugomvi wao kiundani, ila tu mama ukimuuliza lawama ni kwa Baba. Ila sasaivi baba yangu anajuta sana kumpoteza mama, na mimi sina mapenzi nae baba kwa ujumla maana alivyomuacha mama hata mapenzi na sisi na wadogozangu wa2 yakawa yamepungua kabisa kwa kua alikuwa na mwanamke mwingine na tulikua tunaishi wote.

Ilifika stage hadi siku ya graduation yangu namaliza Mama wala Baba hakuwepo wakati wote wapo Dar es Salaam na mimi nikiwa nikisoma hapahapa, Nakumbuka nililia sana wenzangu walifurahi mimi nilikua darasan pekeyangu nalia tu.

LEO NIMEONA HII PICHA NIMEKUMBUKA MBALI SANA
View attachment 521362

(Hawa wazee wako kwenye ndoa miaka 60 sasa. Ghafla bibi akapata stroke. Mzee wake anampenda sana anamuuguza na Hosp wamemruhusu kulala naye kumpa moyo. )
Mshukuru Mungu kwa kuwa upo hai ndugu yangu,ila usimlaumu wala kumchukia baba coz hujui exactly what was going on btn baba'ko na mama'ko,usimuhukumu baba'ko moja kwa moja coz mama'ko alikwambia baba'ko m'baya!Wanaume huwa mara nyingi wanakufaga na tai shingoni,wakiachana na mke huwa mara chache sana huwaeleza watoto mambo mabaya ambayo walikuwa wakifanyiwa na mama yao.Mimi kuna ndg yangu alikuwa akikorofishana mara kwa mara na mke wake mpaka kuna siku yule mwanamke akamropokea yule mwanaume kuwa na hata mtoto walie nae sio wake,jamaa kwa hasira akaondoka akamuacha mama na mtoto(huo ni mfano mmoja tu ila kuna mengi)
 
Shukuru wametengana ndugu yangu maana kupitia kutengana kwako naamini utakuwa umejifunza mengi kuhusu maisha ya ndoa, umuhimu wa wazazi kuishi pamoja hadi kifo, furaha wa watoto kuona wazazi wao wakiwa pamoja, maumivu na shida wanazopitia watoto pindi wazazi wao wanapotengena. Hivyo kwa kifupi through divorce of your parents, you gonna be a good dad, caring and loving one.
Personally, niko kwenye same situation lakini nina furaha kubwa sana kwa hili coz nimejifunza mengi sana ambayo bila wao kutengana nisingejua.
 
Obama kamuona baba yake mara chache tu, kajipiga kifua mtoto wa kiume mpaka kaoa, kapata watoto wake, kawa na mkewe,hawajaachana, kaenda kuwa rais wa Marekani.

Makosa yaliyofanyika unaweza kuyarekebisha kwa wanao kwa kutotengana na uliyenaye.

Hatuwezi kubadili jana, lakini tunaweza kupanga leo na kesho.
 
Una baba mmoja tu, jaribu kutofikira tofauti zao na upange muda wa kumfahamu baba yako.
I wish wanawake wengi wangalikuwa na mawazo kama haya dunia ingalikuwa imenyooka. Usipokuwa mwangalifu mwanamke anaweza kukufanya uchukie watoto waliotoka katika sperm zako. 'niachie wanangu kwani wewe na kibamia unaweza zaa watoto kama hawa' nieleze utafanyaje katika hali kama hiyo, kwa sasa tunapima DNA ila zamani niaje? CC Machuchu GedsellianTz MWANDENDEULE
 
Ilinitokea kwa mtu wa karibu sana, nilimshauri hivyo, ingawa amekulia malezi ya mama na sasa ni mtu anaejitegemea. Walipoonana na baba yake baba alifurahi sana, alimpeleka mpaka kwa bibi yake mzaa baba, alifahamu matatizo ya BP aliyonayo hata bibi yanamsumbua, alifahamu kuwa ni genetic issue kuliko life style. Baba anataka ampe mali lakini jamaa yuko fit wala hana mcheche na mali. Tatizo dingi anata wawe close sana, jamaa amemwambia mengine hayatawezekana tumeonana ukubwani. Tuheshimiane na mapenzi yapo lakini tusilazimishe.
 
Back
Top Bottom