Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,238
Salamu wakuu,
Nimeona niandike huu uzi leo kwa manufaa ya serikali mpya, mamlaka mpya ya TRA na wananchi wa Tanzania kwa ujumla. Nitahadharishe kwamba ninachokiandika ninakifahamu vema na si mambo ya kusikia sikia.
Uchunguzi wangu umebaini kuwa asilimia 70 ya makampuni ya Kenya yenye makampuni toto (subsidiaries) nchini Tanzania yanakwepa kodi mbali mbali zikiongozwa na kodi inayotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi wake waliojiriwa Kenya lakini wakiwa wanafanya kazi nchini Tanzania.
Ukwepaji huu hufanyika kwa njia ya mishahara ya wafanyakazi hawa ambao wengi ni wa nafasi za juu (executives) kulipiwa huko Kenya na hivyo kutolipa kodi ya mapato huku Tanzania. Kinachoshangaza ni kwamba jambo hili limeruhusiwa na TRA kuendelea kutokea kwa miaka zaidi ya 9 ya uchunguzi wangu hadi sasa.
Ninamshauri Kamishna mkuu kufuatilia kampuni hizi. Mpaka sasa kampuni ninazozifahamu zenye wafanyakazi hawa wasiolipa kodi ziko kwenye sekta za mafuta, usafirishaji mafuta, kilimo, usambazaji bidhaa zilizozalishwa Kenya n.k. Kama nilivyotangulia kusema ninafahamu vyema ninalolisema kwa sababu nimehusika moja kwa moja makampuni haya kwa ukaribu ulioniwezesha kuyaona haya kwa undani.
Wakati umefika kwa hawa jirani zetu kuacha kutucheza shere na sisi tuijenge nchi yetu kwa kukusanya kodi stahiki kutoka kwa kila mmoja anayestahili kulipa.
Nawasilisha,
Prisoner 46664.