Makampuni makubwa ya EV China

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,664
59,735
Kwenye masuala ya Technology China inakimbia kwa kasi ya mwanga.
Yafuatayo ni makampuni makubwa ya Electric Vehicles in China
1. Xpeng
2. NIO

Haya ndio makampuni makubwa yanayotengeneza EV nchini China na yanamilkiwa na wachina wenyewe.

Xpeng
Hii kampuni inatengeneza magari:-
Wapo SUV G3
800px-XPENG_G3_002.jpg

Sedan P7
800px-Xpeng_P7_001.jpg


NIO
Wapo na Sport EV EP 9
800px-Nio_EP9.jpg


SUV EC6
800px-NIO_EC6_001.jpg


SUV ES6
800px-Nio_ES6_001.jpg


SUV ES8
800px-NIO_ES8_01_China_2019-04-02.jpg


NB: Ndio maana USA anahaha sana kwa sasa.
 
Kwa sasa China ndiyo inayoongoza kwa matumizi EV.
Top_PEV_global_markets_stock_2017_final_with_California.png

Halafu kwenye hii statistics sijui kwanini United State na California Wamezitofautisha
Nadhani USA anaendelea kuhaha.
 
Hawa NIO wako vizuri, magari yao yana muonekano bomba zaidi ya XPENG, hiyo sedan 7 iko bomba, labda 2035 naweza nunua.
 
Halafu wameungana wote Europe
Halafu German, France, Norway, UK wameziondoa. Lakini bado kipigo kipo palepale.
Sijui kwanini wamewaengua, europe bkla france, ujerumani sijui europe gani, atleast kwenye europe wakiongeza fr, Germany, Sweden inawafikia wachina huko
 
China inafanya vizuri sana katika soko la EV kwa mauzo ya ndani. Lakini, kampuni zake kama NIO na XPeng bado si vinara ama key players katika soko la EV duniani (market share) hata katika soko la China pekee.

Soko lao kubwa linazifaidisha zaidi kampuni za nje kama Tesla, Volkswagen, Nissan na chache nyinginezo ambazo ndizo vinara katika uzalishaji na soko duniani kwa sasa.
 
Kwa sasa China ndiyo inayoongoza kwa matumizi EV.
View attachment 1735893
Halafu kwenye hii statistics sijui kwanini United State na California Wamezitofautisha
Nadhani USA anaendelea kuhaha.
California ni global powerhouse when it comes to EV technology, manufacturing and consumption.

Hapo ndipo ilipo kampuni kubwa zaidi ya EV duniani in terms of market share. Namaanisha Tesla, Inc.
 
California ni global powerhouse when it comes to EV technology, manufacturing and consumption.

Hapo ndipo ilipo kampuni kubwa zaidi ya EV duniani in terms of market share. Namaanisha Tesla, Inc.
Tembea uone rafiki. Dunia imebadilika.
Hii hapa ndio market share ya January 2021
Kampuni ya kwanza ni ya China. Halafu hesabu kampuni ngapi za USA na Kampuni ngapi za China
EV-Makers-640x1256.jpg
 
Mchina mbishi sana tutake tusitake...
Katika makampuni 20 duniani yeye yupo na makampuni 9
1. SGMW
2. BYD
3. SAIC
4. GREAT WALL
5. GAC
6. NIO
7. CHERY
8. XPENG
9. LI XIANG

Hawa jamaa wabishi sana.
 
Tembea uone rafiki. Dunia imebadilika.
Hii hapa ndio market share ya January 2021
Kampuni ya kwanza ni ya China. Halafu hesabu kampuni ngapi za USA na Kampuni ngapi za China
View attachment 1736028
Rafiki, hizi takwimu ulizoambatanisha hapa hazijitoshelezi!

Isitoshe, hicho kitu cha kwanza hapo ambacho ni SGMW sio kampuni. SGMW ni muunganiko wa kampuni zaidi ya moja, kwa lugha nyingine tunaita joint venture. Hiki hufanyika sana katika masuala ya kibiashara.

SGMW ni joint venture ambapo ndani yake kuna kampuni za China pamoja na kampuni ya uzalishaji magari ya Kimarekani inayofahamika kama General Motors. Ndio maana ya uwepo wa "GM" katikati ya hiyo abbreviation.

SGMW si kampuni ya China na wala si kampuni kabisa. Katika sekta ya EV kwa sasa, Tesla inasimama kama kampuni binafsi yenye market share kubwa zaidi duniani.
 
Back
Top Bottom