Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Ni makampuni yanayowekeza katika Wilaya ya Kinondoni ambapo Halmashauri inalazimisha kila kampuni ilipe 3% ya mauzo, siyo faida. Gross Sales. Kwa yale ambayo hayajapata faida, ina maana kwamba wataingilia mitaji yao.
Aidha yale ambayo hayajalipa, yametishiwa kufungiwa. Nimeyapata haya malalamiko kwa wamiliki wawili wa makampuni eneo la Baraka Plaza. Kwa maoni yangu, naona serikali Ya Magufuli imeamua kuwakomoa wafanyabiashara. Kampuni moja ya Uingereza iliyopo karibu na Kairuki Hospital wametoa notisi ya kujiondoa, kwani kwa mwaka, taasisi kama sita za serikali zinakuja pale kudai mapato, nje ya 30% TRA.