Makameraman wa enzi hizo

shav

Member
Nov 2, 2016
74
118
Makamera man walikuwa majeuri
kishenzi yaani!

Kwanza unakuta hii
Kamera ina likamba fulani jeusi
inaning'inizwa shingoni.....
Kameraman ana kabaskeli kake hapa...
nyuma kana begi lina picha za watu ambao hawajamaliza madeni.

Kamera man anakupiga picha leo
anakwambia picha yako utaipata panapo
majaaliwa mkanda ukijaa... unaweza
kusubiri miezi miwili...

Enzi hizo kamera man ndiye anayekupangia pozi gani ukae ili upigwe....
Kamera man anampanga hadi baba yako
mzazi kwenye picha hahahahah! Baba
anakuwa mpoleeee!

Kamera man anapita na kabaskeli kake
watu wanamuita anaringa huyoooo!....

ukute msimu wa sikukuu mnaweka oda
kwa kameraman wiki mbili kabla....... akija
anaanza kwanza kula pilau na soda yake
ipo amehifadhiwa.... baada ya hapo ndo anapiga picha......

Enzi hizo picha inatoka umefumba
macho, na unailipia... sio siku hizi mtu
anapiga picha mia anachagua moja ndo
anaipost mtandaoni......

Enzi hizo sisi watoto tukililia picha tunapigwa flash kilio kinaisha
Hapohapo.......
 
Hahahaaaaa....utakuwa mzaliwa Wa Simiyu au Shy...huku kwetu hamna hayo mambo ni digital toka 1943
 
Hahahaaaaaa! enzi hizo raha sana
59058b84463b7aec7d8e3395f7a0a9df.jpg
 
Nakumbuka tulipiga picha na Mjomba pale studio Flex Iringa miaka hiyo kwa mara ya kwanza unapangwa kama dakika tatu hivi camera aina ya Pentax ina lens mbili black and white na zinatoka hapohapo anaingia dark room kusafisha,that's why picha zilitoka utamu sana siku hizi kila mtu selfie hakuna tena picha za matukio ukiniambia matukio ya maisha yangu mengi yako pictured siku hizi mnapiga picha nyiingi na kuzijaza kwenye sumatifoni kisha baadae mnafuta eti no space kkkk
 
Makamera man walikuwa majeuri
kishenzi yaani!

Kwanza unakuta hii
Kamera ina likamba fulani jeusi
inaning'inizwa shingoni.....
Kameraman ana kabaskeli kake hapa...
nyuma kana begi lina picha za watu ambao hawajamaliza madeni.

Kamera man anakupiga picha leo
anakwambia picha yako utaipata panapo
majaaliwa mkanda ukijaa... unaweza
kusubiri miezi miwili...

Enzi hizo kamera man ndiye anayekupangia pozi gani ukae ili upigwe....
Kamera man anampanga hadi baba yako
mzazi kwenye picha hahahahah! Baba
anakuwa mpoleeee!

Kamera man anapita na kabaskeli kake
watu wanamuita anaringa huyoooo!....

ukute msimu wa sikukuu mnaweka oda
kwa kameraman wiki mbili kabla....... akija
anaanza kwanza kula pilau na soda yake
ipo amehifadhiwa.... baada ya hapo ndo anapiga picha......

Enzi hizo picha inatoka umefumba
macho, na unailipia... sio siku hizi mtu
anapiga picha mia anachagua moja ndo
anaipost mtandaoni......

Enzi hizo sisi watoto tukililia picha tunapigwa flash kilio kinaisha
Hapohapo.......
tumepigwa sana flash
 
Nakumbuka mwishon wa miaka ya tisini songea mjini pale alikua mpiga picha a naitwa mkanda wire kwny alipigaga watu flash mtaan akachukua na hela kabisa akaondoka na mjini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom