Dooooooooh makamera man wa zamani

Fext

Member
Dec 26, 2016
47
49
Makamera man walikuwa majeuri
kishenzi yaani! Kwanza unakuta hii
Kamera ina likamba fulani jeusi
inaning'inizwa shingoni.....
Kameraman ana kabaskeli kake hapa...
nyuma kana begi lina picha za watu ambao hawajamaliza madeni.
Kamera man anakupiga picha leo
anakwambia picha yako utaipata panapo
majaaliwa mkanda ukijaa... unaweza
kusubiri miezi miwili...
Enzi hizo kamera man ndiye anayekupangia pozi gani ukae ili upigwe....
Kamera man anampanga hadi baba yako
mzazi kwenye picha hahahahah! Baba
anakuwa mpoleeee! Kamera man anapita na kabaskeli kake
watu wanamuita anaringa huyoooo!....
ukute msimu wa sikukuu mnaweka oda
kwa kameraman wiki mbili kabla....... akija
anaanza kwanza kula pilau na soda yake
ipo amehifadhiwa.... baada ya hapo ndo anapiga picha......
Enzi hizo picha inatoka umefumba
macho, na unailipia... sio siku hizi mtu
anapiga picha mia anachagua moja ndo
anaipost mtandaoni......
*Enzi hizo sisi watoto* *tukililia picha tunapigwa* *flash kilio kinaisha*
*hapohapo.......*
 
Zamani ipi iyo?, mimi siikumbuki, au wewe umri wako ni mkubwa sana? Una miaka mingapi?, hiyo zamani uliishi mkoa gani wenye hayo mambo ya kameraman?
 
Fext uko sahihi. Hawa wengine wajuzi wanasubiria kupangiwa form five
 
Umenikumbusha Konica na negative, Mna piga picha ya kundi halafu negative mnamtuma cameraman akawasafishie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom