Cameraman wa enzi hizo...

Mamaa Africa

Member
Mar 1, 2018
59
278
Makamera man walikuwa majeuri
kishenzi yaani! Kwanza unakuta hii
Kamera ina likamba fulani jeusi
inaning'inizwa shingoni.....
Kameraman ana kabaskeli kake hapa...
nyuma kana begi lina picha za watu ambao hawajamaliza madeni.
Kamera man anakupiga picha leo
anakwambia picha yako utaipata panapo
majaaliwa mkanda ukijaa... unaweza
kusubiri miezi miwili...

Makamera man wengi walikuwa wanavaa suruali ya kitambaa anafungia juu tumboni, shati kubwa na anachomekea.

Enzi hizo kamera man ndiye anayekupangia pozi gani ukae ili upigwe....
Kamera man anampanga hadi baba yako
mzazi kwenye picha hahahahah! Baba
anakuwa mpoleeee! Kamera man anapita na kabaskeli kake
watu wanamuita anaringa huyoooo!....
ukute msimu wa sikukuu mnaweka oda
kwa kameraman wiki mbili kabla....... akija
anaanza kwanza kula pilau na soda yake
ipo amehifadhiwa.... baada ya hapo ndo anapiga picha......
Enzi hizo picha inatoka umefumba
macho, na unailipia... sio siku hizi mtu
anapiga picha mia anachagua moja ndo
anaipost mtandaoni......
*Enzi hizo sisi watoto* *tukililia picha tunapigwa* *flash kilio kinaisha*
*hapohapo.......*
 
Na picha zikitoka watu wanajazana nje ya nyumba kuzitazama utadhani kuna mkutano wa siasa!
 
Enzi hizo biashara hiyo ilikuwa na status yake. Kwenye dansi hutoi kiingilio. picha moja unalipwa mara mbili (unageuza negative wakati wa kusafisha, wa kushoto ataonekana amekaa kulia). Kwa wadada wanaoshindwa kugomboa picha zao ..... Achilia wale waliokuwa wanataka kupigwa puicha za x (Siyo video ).

Biashara ilikuwa baada ya kuingia vikamera vidogo vya YASHICA lakini vinatoa picha bomba. fani ikavamiwa kabla ya kuingia kwa digital kamera ndo basi tena.
 
Da umenikumbusha mbali sana.Songea kulikua na mpiga picha maarufu miaka ya tisini alikua anaitwa VYAKUMINYA jamaa alikua maarufu sana!
 
Paschal Maweda 1976 Mpaka 2008 John Manyanya 1988 Mpaka 2005 Hao Ndiyo Walikuwa Makameraman Mtaani Kwetu Chief Kashiki 1978 Kameraman Kwenye Mahafali Std 7
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom