tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha ADA TADEA, Ally Makame, amesema kuwa hatua ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kujiuzulu hadharani ililenga kuleta mvutano kati ya wananchi na serikali.
Soma pia: Ndugai, Majaliwa na Mpango wamepigwa bao na Polepole
Akizungumza katika kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, Makame amejibu swali kuhusu sakata la Polepole kwa kutolea mfano namna ambavyo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango alivyoandika barua ya kujiuzulu.
Makame amesema Polepole anajua vyema utaratibu wa kujiuzulu kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma, lakini aliamua kuvunja taratibu hizo kwa makusudi na kuweka barua mtandaoni, akiamini kufanya hivyo kutamletea umaarufu wa kisiasa.
Chanzo: Jambo tv