Nasubiri siku wakiwa wanatekeleza kazi kwa maelekezo ya serikali ya UKAWA kama mtatawala ndio nione comments zenu wanapopatwa na vifo, sijui mtasemaje.!
Mkuu hapa kinacholalamikiwa ni watawala kuitumia polisi kwa manufaa binafsi,
Kunapotokea hali hiyo polisi anajitawala kwani anajua watawala hawatamfanya lolote
kwani analinda maslahi yao.Serikali yoyote iwe ya ccm,ukawa au yeyote,ikiwa itaitumia polisi
kujinufaisha itakumbana na nguvu ya umma.Na polisi anayetumiwa asitegemee msaada wa raia
maana wanamuona ni adui badala ya kuwa rafiki.
Kuna aliyesema tukiwa na shida tunakimbilia polisi,hilo ni kweli
na tunafanya hivyo kwa sababu tunawalipa,mbona hakuna anayekimbilia kampuni za walinzi binafsi
ambao hana mkataba nao,cc tunalipa kodi inayowalipa polisi mishahara hivyo tuna haki
ya kulindwa na mali zetu,kwani tukiibiwa watalipwa mshahara kutoka wapi?