Sijui kama kweli ni CC ndiyo tatizo ndani ya CCM. kujiuzulu kwa CC na Makamba siyo dawa hata kidogo. Mweneyekiti ndiyo tatizo, anafuata upepo wa kisiasa unakoelekea ndiko anakoegemea. Mfano Siku moja Kamati kuu ilipitisha kuwa Dowans lazima walipwe fedha zao baada ya kushinda kesi, baada ya siku mbili kwenye kikao cha wabune Raisi/Mweneyekiti wa chama akageuka maamuzi aliyofanya na wenzake akasema wasilipwe.
Mfano mwingine, Kwa sasa nchi ina shida kubwa ya miundombinu ya barabara, Waziri wake anachukua uamuzi w kusimamia sheria ili maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya upanduzi wa barabara yabomolewe yawe wazi. Wapambe wakamtumia Mesege Raisi/ Mwenyekiti wa chama akaigeuza sheria kuwa waache tu waliojenga kwenye eneo la barabara waendelee kukaa, hakujali kabisa sheria inasemaje. Mtu kama huyu utafanyaje naye kazi?
Kwa mifano hii michache, siamini kabisa kuwa tatizo au gamba la CCM limevuliwa, hii kuchukua mvinyo mpya kuweka kwenye chupa ileile.
Natabiri migogoro zaidi.