Makamba, Msekwa kukalia kuti kavu NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba, Msekwa kukalia kuti kavu NEC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,790
  Likes Received: 83,162
  Trophy Points: 280
  Makamba, Msekwa kukalia kuti kavu NEC

  2008-10-26 13:52:30
  Na Mashaka Mgeta

  Hali inaelezwa si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufuatia kushindwa vibaya katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani katika jimbo la Tarime mkoani Mara hivi karibuni.

  Tayari shutuma za dhahiri zinaelekezwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vya kushindwa katika uchaguzi huo.

  Habari zilizopatikana kutoka ndani ya CCM jijini Dar es Salaam, zimedai kwamba kuna kundi la wana-CCM, wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wamejipanga kuwahoji Makamba na Msekwa, katika mkutano wake (NEC) unaotarajiwa kufanyika wiki ya pili ya mwezi ujao.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Makamba anashutumiwa kukiuka taratibu za mikakati ndani ya CCM, kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi huo, zilizoanza Septemba 14 na kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.

  Uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani jimboni humo, ulifanyika Oktoba 12, mwaka huu, ambapo wagombea ubunge na udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Charles Mwera na John Heche, waliwashinda washindani wa karibu (CCM), Christopher Kangoye na Peter Zakaria.

  ``Makamba alichangia kwa kiasi kikubwa kwa chama chetu kushindwa, kwa maana akiwa Katibu Mkuu, ndiye aliyewajibika kuratibu kila kitu kilichofanyika kule Tarime na uteuzi wa makada kwa ajili ya kampeni zile,`` kilidai moja ya vyanzo vyetu.

  Aidha, chanzo kingine ndani ya UV-CCM kilieleza kuwa, CCM chini ya Makamba, haikuandaa mazingira ya ushindi kwa kuwashirikisha vijana na wanawake wa chama hicho ipasavyo.

  Inadaiwa kuwa, kimsingi, Makamba alipaswa kuandika barua kuitaarifu ofisi ya UV-CCM- Taifa na UWT, kuomba idadi ya makada vijana na wanawake wanaohitajika kushiriki kampeni hizo, lakini haikuwa hivyo.

  ``UV-CCM na UWT ni jumuiya zilizo nguzo ya chama hasa wakati wa uchaguzi kwani ndio inawajua makada wake na uwezo wao, hivyo kupitia kwa vijana hasa wa mkoa wa Mara na katika jimbo la Tarime, tungeweza kushiriki kikamilifu na kuwafikia vijana kwa urahisi,`` alidai mmoja wa watoa taarifa wetu, ndani ya CCM.

  Aliendelea, ``lakini hakuna utaratibu rasmi unajulikana ni kwa namna gani makada waliokwenda Tarime walivyopatikana na wengine ni vijana kutoka wilaya za nje ya mkoa wa Mara, sasa tunajiuliza Makamba aliwajuaje hao vijana bila kuishirikisha UV-CCM,`` alihoji.

  Kwa upande mwingine, taarifa hizo zinadai kuwa hali kama hiyo ilipaswa kufanywa kwa UWT, hasa kwa kutambua ushahidi wa mazingira unaoonyesha kuwa wapiga kura walio wengi ni vijana na wanawake.

  ``Wanawake wa Mara hususani Tarime hawakupewa fursa nzuri ya kuwa sehemu ya kampeni, hili lilikuwa kosa kubwa kwa CCM katika kampeni zile,`` ilidaiwa.

  Hivyo, taarifa zinadai kuwa baadhi ya wajumbe wa NEC wanaandaa mkakati wa `kumuweka kati` Makamba, ili ajibu hoja hizo na nyingine, atakapowasilisha taarifa ya mwenendo wa kampeni na uchaguzi mdogo jimboni Tarime.

  Aidha, kwa upande mwingine, ilidaiwa kuwa suala la kiasi cha fedha na jinsi zilivyotumika, ni suala jingine linalopangwa kuhojiwa kwa nguvu na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.

  Hoja hiyo inaelezwa kuendelea kuelekezwa kwa Makamba, hasa baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, kukemea matumizi makubwa ya fedha wakati wa kampeni.

  Kwa mujibu wa mfumo wa mgawanyo wa uratibu na usimamizi wa kampeni, Msekwa alipangiwa kuratibu kampeni katika kata ya Sirari, akiwa na makada wa chama hicho, akiwemo aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (TLP), Thomas Ngawaiya.

  Baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa jimbo la Tarime, Msekwa alikaririwa akikemea kasumba ya kuwepo matumizi makubwa ya fedha wakati wa kampeni hasa za uchaguzi mdogo kama ilivyodaiwa kutokea jimboni humo.

  Hata hivyo, kauli ya Msekwa inadaiwa kutafsiriwa na baadhi ya wajumbe wa NEC na wanachama waandamizi wa CCM, kwamba ni kielelezo cha kutoshirikishwa kwake katika kupanga na kutumia fedha za chama hicho huko Tarime.

  ``CCM tunalaumiwa kwa matumizi makubwa ya fedha kule Tarime, Msekwa alikuwa kule, kama angeshiriki kupanga matumizi ya kampeni zetu ni dhahiri kwamba kauli aliyoitoa kwa umma isingekuwepo, bali angezungumzia ndani ya chama kule Tarime,`` alisema mmoja wa watoa taarifa wetu.
  Licha ya kuhoji matumizi hayo, Msekwa pia anatajwa kuchangia kuzorotesha uhai wa kampeni za CCM jimboni Tarime, kutokana na ukosefu wa stadi za kumiliki jukwaa la siasa na kuisoma hadhira.

  ``Mara nyingi Msekwa alikuwa akihutubia kwa kusoma, lakini kauli zake za vitisho zilipanua wigo wa wananchi wa Tarime dhidi ya CCM,`` alidai.

  Makamba na Msekwa, waliwasiliana na Nipashe kwa nyakati tofauti, huku kila mmoja akitoa maoni yake kuhusu madai na shutuma hizo dhidi yao.

  Kwa upande wake, Msekwa alisema haoni msingi wa hoja iliyowasilishwa, lakini ufafanuzi unaohusiana na kampeni hizo, unapaswa kutolewa na Katibu Mwenezi wa Siasa na Itikadi wa CCM, John Chiligati.

  ``Mimi mambo haya siyajui, hebu muulize Katibu Mwenezi, ndiye msemaji wa chama,`` alisema.

  Hata hivyo, Nipashe ilipowasiliana na Chiligati kwa njia ya simu, alisikiliza maswali, kisha akakata simu bila kujibu lolote.

  Aidha, alipopigiwa mara kadhaa baada ya kukata, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

  Makamba naye alisema mchakato wa wajumbe wa NEC kuwahoji viongozi wa CCM ni sehemu ya haki yao, kama ilivyo kwa kila mwanachama.

  ``Wakihoji ni halali yao, sisi tulikwenda kwenye kampeni, tukashindwa, acha wahoji ni halali yao,`` alisema.

  Makamba alisema hata kama wajumbe hao wasingehoji, bado uongozi wake ungelazimika kutoa taarifa ya kampeni na uchaguzi wa Tarime, kwa vile ni sehemu ya mchakato wa tathimini inayofanywa na chama hicho kila inapotokea uchaguzi.

  ``Wakinilaumu mimi ama Makamu Mwenyekiti kuchangia kushindwa kwa chama chetu Tarime, acha walaumu, hiyo ndio maana ya kuwa mjumbe wa NEC,`` alisema.

  Hata hivyo, Makamba alisema hoja inayohusu ushiriki wa UV-CCM na UWT katika kampeni za Tarime, inapaswa kuhojiwa na jumuiya hizo ndani ya vikao vya chama.

  ``Hayo ya UV-CCM na UWT kushiriki kwenye kampeni ni yetu, siyo yenu, waje wataniuliza kwenye vikao,`` alisema.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,955
  Trophy Points: 280
  Hayo ni mambo ya ndani ya ccm...Na kama alivyosema katibu wao...uvccm waende humo vikaoni wakalalamike na si kutumia media(kama anavyodai Makamba)
  Kimtizamo...Kwa level ya ccm...Makamba ni kiongozi wao bora sana tu...Hata Msekwa.

  Kwenye propaganda zao wako fine sana tu...Ila ikija kwenye real issues...Ni utata.

  Hakuna lolote ambalo Makamba,JK na ama Msekwa wangeweza kufanya kuwabadilisha mawazo wana Tarime...Wana Tarime walishafanya uamuzi wao na Makamba na Msekwa walienda kupoteza pesa za walipa kodi na walitumwa na chama na si kulaumu individuals.

  Kuwalaumu si haki kwani the same thing happened 2005...The only different ni kwamba nobody knew about EPA and all that.
  Msekwa kudai kuwa ccm inajali matumizi ni UNAFIKI uliokithiri.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni wakati wa kutafutana mchawi, pengine mengi yatasemwa ikiwa ni zile pesa za kukodi chopper ni nani alitoa, ni nani aliratibu magazeti kuandika uongo na uzushi kuhusu kifocha wangwe.

  mkimaliza kukamatana uchawi mtakuwa mmeshindwa chaguzi zingine ndogo mbili zaidi, hapo itabidi mumfukuze kikwete mwenyekiti wenu kwa kushindwa kuhamasisha kampeni za tarime
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Hapo tupo ukurasa mmoja, CCM wameshidnwa huko Tartime wka sababu nyingi sana hawa wawili Makamba na Msekwa wakiwa ni moja ya sababu.

  Wao ni wajumbe wa kundi la mafisadi ambao sio siri kwamba hawawezi shinda uchaguzi bila kutumia hela nyingi sana, kule Tarime walipeleka hela nyingi sana na nusu yake hazikuwa za chama, sasa wameshindwa wakubali sio kulaumu wengine, kimadaraka Msekwa ndiye bossi wa Makamba, sasa iweje eti hajui matumizi ya pesa huko wakati yeye mwenyewe alikuwepo huko kama kiongozi wa timu ya CCM, just pure nonesense!
   
Loading...