Makamba mpiganaji! Mweh..

Huu mimi naona ni mchezo ambao watu "wazima wamekaa" wamekaa na kuamua cha kufanya ili kupunguza nguvu vita dhidi ya mafisadi na amini usiamini Makamba alikuwepo, Rostam ndani, UWT na majizi mengine makubwa katika nchi hii yalikuja na mkakati huu wa kijinga.
 
Neno ufisadi limeanza kuwa msemo mzuri sana kutafuta umaarufu wa kisiasa kuliko hata kueleza nini hasa mwanasiasa au wanasiasa watakifanyia nchi huu mimi naona ni aina nyingine ya upuuzi
a) wanaopinga ufisadi tuwaulize maswali matatu i. wao ni wasafi kiasi gani? (records zao) ii.wasitumia ufisadi kama mtaji wa kisiasa kuwatisha watu wasiende kwenye majimbo yao eti kila anayempinga Sitta, mwakyembe, slaa, zitto etc katumwa? (hapa napata wasiwasi) iii. Waongee isssues aprat from ufisadi kuna mambo mengi yanahitajika kuliko jambo moja tuuuu
b) Napata shida kwasababu kanisani (maaskofu) wanaongelea hayo hayo na miskitini hayo hayo utafikiri kuna mtu anaandaa ajenda inakuwa moja siku zote lets talk other issues of important!
 
Inasikitisha kuona jinsi viongozi wetu wanavyoweza kuchezea akili za wananchi na kuwafanya mabwege. Huu ni uhuni usiovumilika. Haiwezekani kiongozi wa ngazi ya juu katika Chama awe anabadilika kama kinyonga katika kutoa kauli. Naamini kabisa kwamba hivi karibuni zitaanza mbinu za kutumia jina la Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa madhumuni yale yale ya kuwarubuni wananchi kwamba viongozi wa CCM sasa 'wameokoka' wanaanza kufuata nyayo za Mwalimu. Wakishafanikiwa kwenye malengo yao kwa kuwarubuni wananchi, watarudi kule kule walikokuwa na kuwaacha solemba wananchi wakiendelea kuteseka na wao wakiendelea kujinufaisha kwa kutumia vyeo walivyopewa.

Mfumo wa kupata viongozi uangaliwe upya ili waweze kupatikana viongozi wenye nia ya kuwatumikia wananchi badala ya wanaotafuta uongozi ili watumie madaraka kujinufaisha. CCM wanaogopa nini kurudisha Azimio la Arusha? Ndani ya Azimio kuna miiko ya uongozi ambayo itamfanya yeyote anayetaka kugombea uongozi afikirie mara mbili mbili kama yuko tayari kutumikia wananchi badala ya kutafuta utajiri wa haraka haraka kwa kutumia uongozi aliopewa.Kwa msingi huo ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM unaweza kupungua. Marekani tunayoipapatikia sana wanayo maadili na miiko ya uongozi; iweje sisi twende Marekani kuomba vyandarua tu badala ya kwenda kujifunza namna ya kukomesha ufisadi ambao ni janga linaloimaliza nchi yetu na kudumaza maendeleo kwa ujumla? Tujisahihishe!
 
Ukisoma kitabu cha Nabii Yona katika Biblia Takatifu, mji wa Ninawi haufafanuliwi kinagaubaga kwamba huko wapi bali ni mji mkubwa mno na ukubwa wake ni mwendo wa siku 3. Mungu alimwamuru Nabii Yona aende Ninawi kwa maana watu walizidi kutenda dhambi. Lakini Yona alikimbilia Tarshishi apate kujiepusha na uso wa BWANA. Mara ya pili BWANA alimwamuru tena Yona aende Ninawi na alipoingia mjini aliwatangazia watu wake kwamba baada ya siku 40 BWANA atauangamiza mji wa Ninawi. Watu wa Ninawi walimwamini BWANA na wakaanza kufunga, wakajivika magunia na kuketi katika majivu tangu mdogo mpaka Mfalme. Kuona hivyo BWANA alighairi na kuiacha hasira yake ya kuuangamiza mji wa Ninawi.

Mji wa Ninawi (Ninev) ulikuwa nji mkuu wa himaya iliyokuwa inajulikana kama Ashuru (Assyria) kasikazini mashariki mwa Israel kabla ya kuzaliwa Kristu (BC). Mfalme wa Ashuru aliivamia Israel ya kasikazini na kuteka mji mkuu wa Israel (Kasikazini) Samaria mnamo mwaka 730 BC na kuwapeleka waisrael ya kasikazini utumwani huko Ashuru.

Yona alipeleka ujumbe wa Mungu kule Ninawi na watu walitubu na kupona. Je Makamba anapeleka ujumbe kama huyo huko anakozunguka ili CCM na wana-CCM watubu ili wapone ghadhabu ya umma 2010? Tafakari.
 
Makamba ahimiza mapambano dhidi ya ufisadi

na Jacob Ruvilo, Kigoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema ufisadi unapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania mzalendo, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia maendeleo ya nchi.

Makamba alisema hayo juzi kwenye semina ya viongozi wa CCM Jimbo la Kigoma Mjini iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Alisema suala la watu kujipatia mali kinyume cha utaratibu na kuhujumu nchi havina uhusiano wowote na CCM, kwani watuhumiwa wote hawakuagizwa na chama kufanya hivyo, bali ni hulka zao binafsi.

Makamba alifafanua kuwa suala la muumini wa dhehebu fulani kwenda kinyume na maadili au amri ya vitabu vya dini, hapaswi kulaumiwa sheikh au mchungaji, badala yake ni muumini husika ambaye mwisho wa siku ndiye atakayepata adhabu kwa Mungu.

Aidha, Makamba alisema suala la vyama vya upinzani kushika bango na kuidhihaki CCM kuwa ni mafisadi kutokana na viongozi wachache wasio waaminifu, halina maana, bali suala la umoja na mshikamano katika kupinga mafisadi hao ni jukumu la watu wote, ikiwamo CCM.

Mbali na hilo, Makamba alikemea baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia uwezo wao wa fedha kutoa rushwa ili kupita katika chaguzi mbalimbali kuwa ni moja ya upatikana wa viongozi mafisadi na wasiofaa kwa jamii.

Alisema Tanzania haikuandaliwa kutawaliwa na wenye nacho na kwamba hali hiyo inaweka tabaka la mwenye nacho na a asiyenacho, hali ambayo isipoangaliwa kwa umakini suala la rushwa litabaki kuwa ndoto.


My Take:
Nasubiri kina Rostam na wenyewe waunge mkono vita hii!!


Ili kujisalimisha mwizi anapofukuzwa na wananchi wenye hasira yeye pia huanza kupiga kelele MWIZI MWIZI ili kujibaraguza kuwa yeye sio mhusika!! Huyo ndio Makamba na ufisadi.
 
Makamba akiwa Kisarawe mwanzoni mwa mwaka huu alisema fisadi ni mtu mzinzi na muasherati, aliyekubuhu kwenye ngono zembe. Ingekuwa vema kwa mzee Makamba ama akawataja hao mafisadi kwa majina au akatueleza kinagaubaga fisadi ni mtu aliyefanya nini. Siajabu huyu mzee anapiga vita ngono zembe kwenye chama chake na sisi hatumuelewi, tunamlaumu buree.
 
Makamba ahimiza mapambano dhidi ya ufisadi

na Jacob Ruvilo, Kigoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema ufisadi unapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania mzalendo, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia maendeleo ya nchi.

Makamba alisema hayo juzi kwenye semina ya viongozi wa CCM Jimbo la Kigoma Mjini iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Alikuwa wapi fisadi huyu siku zote hizi katika vita hii dhidi ya mafisadi? Miezi 12 kabla ya uchaguzi Mkuu naona naye kaamua kudandia behewa kama vile alikuwemo katika safari hii dhidi ya mafisadi. Tutaona vioja na viroja vingi kuelekea 2010. Wapi Rostam, Manji, Jeetu, Karamagi, Mkono, Mzindakaya, Subhash Patel na mafisadi wengine nao waukemee ufisadi!? Ukistaajabu ya Mussa....
 
Eh! Makamba? Ya Ufisadi umekua "Saul to Paul"! Hii ni typical of Machiavellianism, ndio siasa yao CCM baada ya Mwalimu... kutulaghai tu! Makamba na CCM, 2010 hatudangayiki!! Habari ndio hiyo!
 
My Take:
Nasubiri kina Rostam na wenyewe waunge mkono vita hii!!

Mkuu kwani umesahau kama Rostam alishajiunga katika vita dhidi ya ufisadi pale alipoyataja ya Mengi na mwenyewe kukiri?

nani katika nchi hii aliyeweza kuweka wazi ufisadi wa Mengi zaidi ya Rostam?
 
Makamba akiwa Kisarawe mwanzoni mwa mwaka huu alisema fisadi ni mtu mzinzi na muasherati, aliyekubuhu kwenye ngono zembe. Ingekuwa vema kwa mzee Makamba ama akawataja hao mafisadi kwa majina au akatueleza kinagaubaga fisadi ni mtu aliyefanya nini. Siajabu huyu mzee anapiga vita ngono zembe kwenye chama chake na sisi hatumuelewi, tunamlaumu buree.


Ha ha ha ha! Mkuu umenifurahisha sana, kweli inabidi Makamba atoe definition yake kwanza tujue alimaanisha ufisadi uleule aliouzungumzia Kisarawe au kakengeuka? tusije kumlaumu sana kumbe hana maana tunayofikiria hapa jamvini.
 
Back
Top Bottom