Makamba, Londa waufyata kwa Mdee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba, Londa waufyata kwa Mdee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Jul 31, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa viti maalum, Halima Mdee, amewatoa 'knock out' Makamba na Londa, ambao walilazimika kuondoa malalamiko yao kwa Spika wa Bunge dhidi yake Mbunge huyo kutokana na kauli yake (Mdee) akiwatuhumu kwa ufisadi katika sakata la ugawaji viwanja huko Kinondoni.
  Baada ya Mdee kutoa kauli hiyo Bungeni, Makamba na Londa walipeleka malalamiko kwa spika lakini wakati kamati inayafanyia kazi, Makamaba alimwandikia spika akisema anajitoa kwenye mashitaka kwa sababu machungu aliyokuwa nayo yalishakwisha.
  Baadaye, wakati kamati inaendelea, baada ya Londa kuhojiwa, aliposikia kuwa Mdee naye amehojiwa na kutoa vielelezo lukuki, Londa naye alimwandikia Spika akimweleza kujiondioa kwenye shauri hilo.
  Katika ‘hukumu' aliyoisoma Bungeni jioni hii, Spika Sitta amesema kutokana na hali hiyo, maneno ya Mdee dhidi ya vigogo hao wawili yanabaki kama yalivyo na hakuna haja ya kuwaomba radhi
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  heheheh kaaazi kweli kweli! sasa basi ina maana kuna uwezekano wa kuwashitaki kama kuna jinai humo ndani!
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kama tuhuma zimethibitika bungeni, kitu gani kinafuata - Mdee kuombwa radhi, Makamba na Londa kuwajibishwa au busara za Spika kutumika ?
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Mkuu Mag3 hapo ndo zimeshatumika hivo!
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kaaazi kweli kweli ... sera ya funika kombe - mafisadi wazidi kupeta.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na kwenye hoja ya Selelii kuhusu barabara ya Chalinze, Spika anasema imebainika kwua fedha zilizoombwa zilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya changarawe, lakini waziri ameenda kusaini mktaba na mkandarasi wa kujenga barabara ya lami, akaongeza fedha zaidi ya zile zilizoruhusiwa na Bunge. lakini kwenye uamuzi wake Spika alisema hana la kufanya kwa sababu hakuna utaratibu wa kupanga vipaumbele vya kitaifa katika suala la ujenzi wa barabara.
  Sendeka na Kwaangw' walijitahidi kutaka waziri awajibishwe kwa maana kuwa alikwenda kufanya kitu ambacho hakikuagizwa na Bunge, lakini Sitta inaonekana aliamua kuwa diplomatic na kusisi tiza kuwa anadhani serikali imesikia
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naomba mungu 'BUTU NA MOI' huyu binti lisimkute la kumkuta!ccm ninayoijua mimi HAPANA BANA!

  -they may silence her IN MANY WAYS:
  1-
  2-
  3-
  4-
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Mpitanjia, saafi sana hapa nina barua moja ya Makamba ya siri sana iliyoandikwa kwa mkono wake kwa Spika, akimlilia kuhusu hii ishu ninayo hapa, naomba niwaandikie wana JF wote kama ilivyo na wakati muafaka nitaibandika hapa maana sasa JF tunaanza kwenda kwa mwendo wa mdundo like never before, inasema hivi-:

  - Sasa unaposema kwamba amechomoa, inaleta maswali mengi kuliko majibu, wakati hiki kibarua alikiandika kwenye kikao cha bunge lilopita iweje leo achomoe?

  - Halafu cheki eti na yeye anajua machungu ya kucheleshewa haki!

  Respect.

  Field Marshall Es.
   
 9. M

  Mvutakamba Member

  #9
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yangu maswali ni haya kwenu nyie wadau wenzangu

  1.Londa kulalamika kwa Spika kama mwananchi ama Naye ni Mbunge mie sijui ?

  2.Si sahihi sasa Mdee kwenda mahakamani kuendeleza na litampa heshima kule Kawe ambako CCM wana wasi wasi sana kushindwa wakati wa Uchaguzi mkuu ?

  Msaada wenu tafadhali
   
 10. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kazi ya Chief Prosecutor ni nini????? Kama Bunge limethibitisha hilo kuwa maneno ya Mbunge Mdee yanabaki kama yalivyo ina maana kuwa Londa na Makamba wamethibitika kuwa walitenda yale makosa. Nafikiri ni jukumu la Chief Prosecutor kufanya kazi yake.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Amelalamika kama mwananchi wa kawaida. Kwa mujibu wa kanuni zilizopo, Mbunge analindwa kwa anayoyasema Bungeni. Lakini iwapo atakayoyasema yatahusu tuhuma dhidi ya mtu aliye nje ya Bunge, ambaye hawezi kujitetea moja kwa moja Bungeni, mtu huyo ana haki ya kumwandikia Spika akijitetea au kulalamikia kauli ya Mbunge
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unaweza kuta chief-prosecutor huyu POLITICALLY makamba ni boss wake.sasa unategemea nin kwenye serikali ''ya kulindana-lindana''?
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kazi kwelikweli. Na tatizo ni kuwa Londa na Makamba ni sewhemu tu ya vigogo ambao wanahusika na sakata hili.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Awali walimu-undermine, walimuona kuwa ni 'dogo' tu. Kumbe mwenzao alikuwa amejipanga. Alitumia elimu nyake ya sheria kuwabana. Alijaribu hivyo nje ya Bunge wakawa wajanja, wakaruka kisiasa. Akaamua kukusanya nondo kamili na kurusha mambo Bungeni. Huko sasa hakukuwa na longolomgo na wazee wakaingia kichwakichwa na kutaka kumnyamazisha 'dogo'. It was too late walipobaini kuwa ana nondo zote. Wakashaurwa na wenzao wajondoa 'mashitaka' yao lkn nadhani Sita akala jiwe na kuamuru kamati iendelee na mchakato hata kama walioshitaki wameamua kujitoa.
  tatizo ni kuwa Makamba na Londa ni sehemu ya vigogo wengi wanaohusika na madudu haya, walijua kama wataliendeleza hili, wengi watavutwa na mwisho wa siku 'dogo' angeonekana amewashinda wengi
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Halafu anataka kutudanganya kwamba mafisadi wanatishia uhai wake! Wakati kila kukicha anawakingia kifua kutoka na ufisadi mbali mbali walioufanya!! Hii ni kesi ambayo inatakiwa ikabidhiwe kwa vyombo vya sheria ili mkondo wa sheria ufanye kazi yake. Mkondo huo wa sheria ndiyo huo huo umeshindwa kumtia hatiani yeyote hadi sasa katika kesi ya EPA, kesi ya Richmond, kesi ya Rada, Kesi ya Meremeta, Kagoda n.k. n.k. :(
   
Loading...