Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 303
• Adaiwa kuwa chanzo cha kuvurugika kwa kura za maoni
MZIMU wa kuvurunda kwa uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), umemwangukia Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Luteni Yusuf Makamba.
Kwa hali hiyo, safari hii wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, wakiwemo baadhi ya wabunge na mawaziri walioangukia pua, wamepania kuwasilisha hoja ya kutaka kumng'oa au kumlazimisha ajiuzulu wadhifa huo mara moja.
Makamba ambaye yuko katika wakati mgumu, anadaiwa kuvuruga kura za maoni kwa kukiuka mapendekezo ya tume ya Dk. Ghalib Bilal, iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kusaka namna bora ya kuwapata wawakilishi wa Viti Maalum, pamoja na utaratibu bora za kura za maoni.
Mapendekezo ya tume ya Dk. Bilal, yalipitishwa rasmi na NEC kwenye kikao chake kilichofanyika Aprili mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, lakini siku tatu kabla ya kura za maoni, Makamba alibadilisha maamuzi hayo na kutangaza utaratibu wake bila ridhaa ya chama.
Vyanzo vya habari kutoka baadhi ya wajumbe wa NEC kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, walisema Makamba alimevuruga uchaguzi huo kwa kutaka kuwabeba baadhi ya wagombea wake.
Maamuzi ya NEC yanayodaiwa kubatilishwa na Makamba ni pamoja na kuwataka wapiga kura wote wawe na kadi hai za CCM zilizolipiwa angalau kwa miezi mitatu nyuma.
CCM pia ilipitisha azimio la kuwataka wapiga kura wote licha ya kuwa na kadi hai ya CCM, pia wawe na vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kudhibiti mamluki.
Katika azimio la tatu, CCM ilikubali kuwa ifikapo Juni 30 iwe mwisho wa usajili wa wanachama wapya na watendaji wa chini waliagizwa kuorodhesha majina ya wanachama wao, kazi ambayo iligharimu mamilioni ya fedha kwa nchi nzima.
"Kilichotokea ni kwamba siku tatu kabla ya kura za maoni, Makamba katangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa kila mwana CCM mwenye kadi, bila kuonyesha kitambulisho cha kupigia kura, aruhusiwe kupiga kura na hapo ndipo vurugu zilipoanza," alisema mmoja wa wajumbe wa NEC kutoka mkoani Mwanza.
Kutokana na hali hiyo, wajumbe wa NEC, wakiwemo baadhi ya mawaziri na wabunge waliogombea na kushindwa, wanaotarajia kuanza vikao vyao vya mchujo mjini Dodoma, wamepania kumng'oa Makamba katika nafasi yake.
"Mara nyingi Makamba tumekuwa tukimtetea pale kundi fulani lilipoendesha harakati za kutaka kumng'oa, lakini safari hii mkakati huu ni wa wajumbe wengi wa NEC," alisema mjumbe mwingine wa NEC kutoka jijini Dar es Salaam.
Hivi sasa mkakati wa kutaka kumng'oa Makamba, unapenyezwa kwa wajumbe wa NEC kupitia njia ya ujumbe mfupi wa simu zao za mkononi, huku wakimtahadhalisha Rais Kikwete kutomkingia kifua.