Makamba kung'olewa ukatibu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba kung'olewa ukatibu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Aug 11, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  • Adaiwa kuwa chanzo cha kuvurugika kwa kura za maoni

  MZIMU wa kuvurunda kwa uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), umemwangukia Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Luteni Yusuf Makamba.

  Kwa hali hiyo, safari hii wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, wakiwemo baadhi ya wabunge na mawaziri walioangukia pua, wamepania kuwasilisha hoja ya kutaka kumng'oa au kumlazimisha ajiuzulu wadhifa huo mara moja.

  Makamba ambaye yuko katika wakati mgumu, anadaiwa kuvuruga kura za maoni kwa kukiuka mapendekezo ya tume ya Dk. Ghalib Bilal, iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kusaka namna bora ya kuwapata wawakilishi wa Viti Maalum, pamoja na utaratibu bora za kura za maoni.

  Mapendekezo ya tume ya Dk. Bilal, yalipitishwa rasmi na NEC kwenye kikao chake kilichofanyika Aprili mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, lakini siku tatu kabla ya kura za maoni, Makamba alibadilisha maamuzi hayo na kutangaza utaratibu wake bila ridhaa ya chama.

  Vyanzo vya habari kutoka baadhi ya wajumbe wa NEC kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, walisema Makamba alimevuruga uchaguzi huo kwa kutaka kuwabeba baadhi ya wagombea wake.

  Maamuzi ya NEC yanayodaiwa kubatilishwa na Makamba ni pamoja na kuwataka wapiga kura wote wawe na kadi hai za CCM zilizolipiwa angalau kwa miezi mitatu nyuma.

  CCM pia ilipitisha azimio la kuwataka wapiga kura wote licha ya kuwa na kadi hai ya CCM, pia wawe na vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kudhibiti mamluki.

  Katika azimio la tatu, CCM ilikubali kuwa ifikapo Juni 30 iwe mwisho wa usajili wa wanachama wapya na watendaji wa chini waliagizwa kuorodhesha majina ya wanachama wao, kazi ambayo iligharimu mamilioni ya fedha kwa nchi nzima.

  "Kilichotokea ni kwamba siku tatu kabla ya kura za maoni, Makamba katangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa kila mwana CCM mwenye kadi, bila kuonyesha kitambulisho cha kupigia kura, aruhusiwe kupiga kura na hapo ndipo vurugu zilipoanza," alisema mmoja wa wajumbe wa NEC kutoka mkoani Mwanza.

  Kutokana na hali hiyo, wajumbe wa NEC, wakiwemo baadhi ya mawaziri na wabunge waliogombea na kushindwa, wanaotarajia kuanza vikao vyao vya mchujo mjini Dodoma, wamepania kumng'oa Makamba katika nafasi yake.

  "Mara nyingi Makamba tumekuwa tukimtetea pale kundi fulani lilipoendesha harakati za kutaka kumng'oa, lakini safari hii mkakati huu ni wa wajumbe wengi wa NEC," alisema mjumbe mwingine wa NEC kutoka jijini Dar es Salaam.

  Hivi sasa mkakati wa kutaka kumng'oa Makamba, unapenyezwa kwa wajumbe wa NEC kupitia njia ya ujumbe mfupi wa simu zao za mkononi, huku wakimtahadhalisha Rais Kikwete kutomkingia kifua.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaha mahoka wacha wachanganyane tehe tehe tehe tehe
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakimng'oa itakua busara kuu....Jamaa huwa hafikiri kabla ya kuongea.......
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Makamba anafanya kazi kwa maelekezo maalumu toka kwa mwenyekiti wake Kikwete na marafiki zake Lowasa na Rostam. He is just a kikaragosi, wasimlaumu..
  By the way wanalalamika sasa kwani hawakuona tangu mwanzo kuwa Makamba ni kilaza? Huu ndio unafiki wa wanasiasa wa Afrika. Uwezo wa kiongozi kuongoza unahojiwa pale anapogusa maslahi binafsi ya mtu..
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Mimi nilikuwa nawambia mwanzoni kuwa hakukuwa na Card fake za CCM ni ETHICS ilivurugwa hamkunielewa kwani nilijionea kwa macho yangu mwanachama ameandikishwa siku mbili au moja kabla kupiga kura za maoni ulisha ona wapi na jina unalikuta kwa Reja??

  Card maelfu na maelfo hazikuwa na picha wala stakabadhi ya ndani au malipo ya uanachama ya miezi mitatu tu nyuma?? ati kupiga kura card iwe na stamp(mhuli wa katibu tawi) na jina la mwenye kadi utathibitishaje kuwa yeye ni ndie mwenye Card halali ya CCM?

  Ndio Hayo mambo Mtangazanji Mmoja wa Clouds FM G. Hando kipindi cha PB alisema CCM wao wenyewe watatatua matatizo yao wenyewe na wasijaribu kuyahusisha na watu wengine wao ndio walio sababisha madudu yote hayo leo wanaanza kugeukana tena.

  Kwahio tukubaliane kuwa matokeo yote haya ya kura za maoni ni batiri??Au???

   
 7. F

  Fanta Member

  #7
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na hutenda bila kufikiri.

  sasa mzee mzima alitaka tu zoezi limazike bila kujali taratibu zinafuatwa au laah.
  ngoja nisubiri hatua zaidi zitakazochukuliwa, meanwhile naburudika na jinsi ccm wanavovurugana.
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Tatizo lililopo ni kwamba viongozi wengi wa cCM bado wanaishi katika pat groly (fikra za mwenyekiti ni sahihi na zidumu), hawapo kabisa katika wakati wa sasa ambapo watu wanafikiria na wana uhuru wa kusema. Ni wakati umefika sasa kwa jamii kulijua hili, hii itatusaidia kuwapata viongozi wanaotufaa.
   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Sasa mzee wa vinywaji,
  Hivi tukisema au kuianzisha hii Issue kuwa kubwa na kuwa huyu mzee alilipitisha au kubadilisha mapendekezo ya Bilal kwa NEC ili yawe in favor of his Son January Makamba atabisha huyo Yusuph Makamba mwenyewe??

  Katibu Mkuu antaka kusaha kuwa waliwawajibisha makatibu wa wilaya ya Bukombe na kuhamishwa immediately the same night pale wagombea waliposema hawana imani na katibu wa wilaya na pia ndicho kilicho tokea kwa Mr. Mzuri pale DODOMA na kutupwa Morogoro na kushushwa cheo kwa kumsaidia KIMBISA na ndilo lilikuwa kosa lake kwani familia ya mzuri iliweka wazi wazi mjini dodoma kuwa inamsaidia kimbisa kwani watoto wa mzuri mpaka baba yao ameamishwa wao walikuwa wanaendelea msaidia kimbisa kampeni wilaya ya dodoma mjini, kila kukicha wakishida vijijini esp Hombolo.

  Sasa leo makamba anasahau kusimamia katiba na mashauri yaliyopendekezwa na kuvuruga uchaguzi wa kura za maoni kwanini wana CCM wasi gome kwa hilo au kumsurubu Katibu wao Mkuu Mr.Y.Makambaaaaa?

   
 10. F

  Fanta Member

  #10
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa jethro, kuwajibishwa kuna tegemea nani ndo mtenda kosa (nionavyo mimi) sitashangaa mambo yatakavyopindishwa pindishwa ili tu ya-suit matakwa ya mtu au watu fulani na sitashangaa mtu mzima kuendelea kubaki kwenye post yake.(kwani yeye si mouthpiece tu)
  hii ndiyo CCM
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu
  (fikra za mwenyekiti ni sahihi na zidumu), Fikra za Mwanyekiti yupi?? Umesahau kuwa hawa CCM waliopo ndio walikuwa wanajiita wana mtandaoooo??

  Waliingia IKULU huku hawajui walichokifuata IKULU na ndicho kinacho wakuta sasa walikuwa makundi makundi walijiuunga gafla na kumpiga chini Salim Ahamed Salim huku wakisahau kabisa kuwa wakishinda wanatakiwa wakafanye nini IKULU?

  Wale unao sema
  (fikra za mwenyekiti ni sahihi na zidumu),ndio hao wakina butiku waliopigwa chini na mpaka sasa wanadharauliwa, wakitoa maonyoo wanaambiwa mbona wakati wao hawakufanya hivyoo

   
 12. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa maoni yangu itakuwa pigo kwa 'upinzani' endapo ma-rope atapigwa chini maana mimi ni kati ya watu wanaoamini kabisa 'uongozi mzuri na uliotukuka wa ma-rope' ndio utakaokifikisha chama hicho mahali ambapo ni 'beyond repair' na ndipo maisha bora kwa kila mtanzania yatakapoanza!
   
 13. H

  Heri JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  At this late hour i find it difficult CCM kumtupa Makamba. Walijaribu wakaambiwa kuwa , wakati huu wa uchaguzi siyo vizuri kumtoa SG . Ni kweli Makamba amevuruga mchakato mzima wa uteuzi wa wabunge na madiwani. Muda wa mtu kuchukuwa na kufanya kampeni ilikuwa mdogo. Ingekuwa minimum mwezi. Wabunge wengi wazamani wangeanguka na rushwa kwa kamati za siasa na wenyeviti wa kijiji zingepungua. Daftari / register za wanachama pia zingekuwa zimekaguliwa vizuri na ordha kamili kujulikana. Kanuni na menendo za uchaguzi hazikuwa zinaeleweka au kuwa na standard moja ,kwa mfano kuchangia chama wakati wa kuchukua form . Sidhani Makamba ana vision yeyote ya kuendeleza au kuboresha chama. Mangula was much better CEO.
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Ukisemacho ni kweli hawawezi mtoa muda huu wa uchaguzi
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,480
  Likes Received: 5,859
  Trophy Points: 280
  hapa kwenye huu mnuso anafuatilia kiti moto iko wapi.....shekhe huyu bana...biblia yake kiti moto yake
   
 16. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hawawezii kumngoaaa MAKAMBA UKATIBUU MKUU...
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,749
  Trophy Points: 280
  Let them kill each other, after all they are animals. TEHE TEHE TEHE TEHE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Thank you God
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tulishaandika haya mara baada ya uchaguzi. Ila wengi tulikuja kutukanwa na kubezwa saaana.

  Kuna madudu mengi sana yalifanyika wakati wa uchaguzi. Kuna majimbo ambayo watu walikuwa wakinunua vituo na kwa hiyo kutangaza matokeo yoyote wanayotaka wao. Kuna majimbo unakuta wamejiandikisha watu 9,000 na katika hao kuna wengi hawajalipia kadi na wengine hawapigi kura ila unashangaa mtu anashinda kwa kura 12,000. Hapo ndipo unaona kweli maneno ya Dr. watu wanayatumia kikwelikweli yaani "Kura za kupewa, changanya na za kwako."

  Jambo zuri alilolifanya Mkapa ni kuachia uongozi watu wabovu. CCM na Muungano vitamlipukia mtu mikononi. Na hapo kitakachofuata na mtu baki aje kutawala/kuongoza Tanzania. Nitafurahi kuwaona Mkapa na Mkewe Anna na mume mwenza Mramba wakipanda kizimbani Kisutu. Imma Advocate na Mkono Advocate nao lazima wapande. Nina imani mtoto wa Karume atarudi kwao Zanzibar na wengine wote watakaobaki watasaidia kujibu shutuma kubwa za BoT, Deepgreen nk nk nk

  Hao viongozi wanaollialia kama watoto shame on them. Yaani walikuwa wanamlea Makamba siyo, hihihiiiiiiiii
  Ukicheza na Nyani, MMEVUNA MABUA WAJOMBA. Msahaulike Milele.
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Unless Mnajimu wao sheikh Yahaya atabiri kuondoka kwake ndio watamuondoa. Mie nadhani Makamba wanamuonea tuu, yanayojitokeza CCM ndio hali halisi ya chama chenyewe kwa ujumla wake sio tatizo la Makamba.
   
 20. F

  Fanta Member

  #20
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante chakaza, na ndio maana hawawezi kumtoa.......japo na uvaluvalu wake unachangia
   
Loading...