MAKAMBA: Kamati ya Bunge kuhoji ufisadi Tanesco

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Exuper Kachenje
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba amesema kamati yake italihoji Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kuhusu upotevu wa mabilioni ya fedha kama ilivyoonyeshwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dar es Salaam jana, Makamba alisema taarifa hiyo ya ufisadi ndani ya Tanesco iliyotolewa na CAG imemsikitisha na kwamba hawezi kukaa kimya.

Taarifa ya CAG iliyoishia Juni 30, 2010 ambayo ilitolewa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge uliomalizika karibuni, ilibaini kuwa Tanesco imeilipa kampuni ya Dowans Sh1.8 bilioni ikiwa ni gharama ya kusafirisha mitambo ya kampuni hiyo kuja nchini kwa ndege badala ya Sh180 milioni.

Matumizi hayo ya ziada yanayokadiriwa kufikia Sh1.4 bilioni yaliingizwa katika akaunti ya Dowans kulipia gharama za usafirishaji mitambo hiyo kimakosa.

CAG alisema hadi sasa, Tanesco imeshindwa kumpelekea ripoti ya matumizi ya fedha hizo alizoziita kuwa ni ufisadi.
Jana, Makamba alisema: "CAG ameona madudu ndani ya Tanesco na sisi kama Kamati ya Bunge tunaona ni muhimu Tanesco watoe maelezo. Tutadai watoe maelezo ya kuridhisha kuhusu ufisadi huo."

AlisemaTanesco inashangaza kwa kufanya madudu hayo na kukaa kimya muda mrefu kana kwamba haijui ilichofanya au haina ukaguzi wa hesabu.

Alisema ingawa anatambua kuwa jukumu la kuhoji hesabu ya mashirika ya umma ni la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyo chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kamati yake itadai maelezo hayo kwa kuwa inahusika na shirika hilo.Hata hivyo, katika taarifa yake ya ukaguzi CAG pia ameitaka Tanesco impelekee mchanganuo wa matumizi ya Dola
4,865,000 sawa na Sh6.8 bilioni.

SOURCE: Kamati ya Bunge kuhoji ufisadi Tanesco
 
Wakishahoji huo ufisadi wa Tanesco then what? Kila siku Mrema nae anahoji, halikadhalika Zitto nae anahoji. Sijaona hata mtu mmoja amenyongwa kama China au hata kufungwa jela.
 
Na ile kamati ya Zitto ya mashirika ya umma ifanye kazi ipi? Kamati ya Makamba iishie wizarani vinginevyo hii ni vurugu na kuichanganya TANESCO.
 
Mimi kila siku likitokea jambo nasikia wanahoji tu, wanahoji tu sijui kamati fulani itahoji ubadhirifu wa kitu fulani ila hakuna actions zozote zinazochukuliwa sijui tuelewe vipi
 
hiyo kama ti basi iwe na nguvu ya kuwanyooshea kidole importers wa mafuta........ NTAWAHESHIMU ZAIDI
 
Back
Top Bottom