Makamba: Enzi za ushindi wa kishindo CCM zimepita

Standalone

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
676
576
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

"Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.
===================

Dar es Salaam. Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

"Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo), huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika.

Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka 2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.

Akizungumza jana katika mahojiano na kipindi cha ‘Power Breakfast' cha Redio ya Clouds na baadaye kufafanua baadhi ya hoja alipozungumza na mwandishi wetu, Makamba alisema matokeo ya uchaguzi huo ni ishara kwamba kwa umri wa miaka 22 sasa, mfumo wa vyama vingi vya siasa umeanza kuimarika.

"Hata ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni mkubwa na hata kama tungepata asilimia 70 haupunguzi uhalali wa uongozi. Kusema CCM itang'oka madarakani, hapana, bado wananchi wanakiamini tena sana," alisema Makamba.

Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, alizungumzia pia namna ya kuwapata wagombea wa urais na kusema mwaka huu ndiyo utapima ukomavu wa chama katika harakati za kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.

Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwa
Makamba ambaye Julai 2, mwaka jana akiwa London, Uingereza alitangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, alisema mwaka 1995 mgombea alipatikana kwa malezi ya Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 2000 aliendelea aliyekuwapo.po. Alisema mwaka 2005 ilikuwa kama 1995 lakini mwaka huu ni tofauti na vipindi vingine kabisa.

"Hii ni mara ya kwanza hakuna uhakika wa nini kitatokea na kwa mara ya kwanza chama chetu kama taasisi kitajaribiwa... na sisi tuna utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa.

"Tuna sifa 13 za kumpata mgombea, sifa hizi na taratibu nyingine zikifuatwa tutampata. Mchakato ukiwa wa haki tutampata kwani nina imani na mwenyekiti (Rais Kikwete), Katibu Mkuu (Abdulrahman Kinana) na Kamati Kuu," alisema Makamba .

Ujana na uzee

Kuhusu hoja ya ujana au uzee ambayo imewagawa wagombea urais wa CCM, Makamba alisema kuna tofauti kati ya umri, uwezo na uzoefu ili wananchi waweze kumwamini mtu na kumpa fursa ya kuwatumikia, jambo ambalo alisema halihitaji kutumia fedha nyingi au kuweka mbele uchu wa madaraka ili kuyafanya mazingira yawe ya lazima kupata.

"Nchi ipo njiapanda na mwaka huu ndiyo itaamua kupaa au kuporomoka lakini kumchangua kiongozi ambaye ameshiriki kuuweka mfumo huu wa uongozi unaolalamikiwa sasa ni kurudisha nyuma maendeleo. Kuna vijana viongozi na viongozi vijana. Kuna vijana ambao wameandaliwa vyema kuja kushika uongozi wa juu, hivyo tukipata viongozi wa sasa wanaojua ulimwengu wa sasa, nchi yetu itaweza kupaa zaidi," alisema Makamba.

Kuhusu uzoefu

Akizungumzia uzoefu wa uongozi hasa urais, Makamba alisema Tanzania ina watu wanne pekee, mmoja akiwa marehemu, ambao ndiyo wazoefu na uongozi wa juu ambao ni Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na Rais Kikwete anayemaliza muda wake.

"Hakuna yeyote tofauti na hawa wanne anayeweza kusema ni mzoefu... Vijana wanaweza lakini tusingependa kurudi katika hoja hii na kinachotakiwa ni kubadili taswira ya uongozi kabisa ni wakati wa fikra na mawazo mapya.

"Kuna watu wamekuwa viongozi kwa zaidi ya miaka 40 lakini leo hii hawataki Muungano na kuna vijana ambao wanautaka hivyo hapa hoja siyo umri au uzoefu, bali ni kipi ambacho unataka kukifanya katika Taifa lenye kila aina ya rasilimali," alisema Makamba, mtoto wa katibu mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba.

Akizungumzia kitabu alichoandikiwa kinachoitwa, Maswali na Majibu 40: Mazungumzo na January Makamba kuhusu Tanzania Mpya alisema wananchi wanatakiwa kumjua kiongozi wanayetaka kumpa dhamana hivyo andiko hilo linatakiwa kuzua mjadala.

"Taifa litasonga mbele kama wananchi watamchagua kiongozi ambaye wanamfahamu, tusiwe kama msemo unaosema tusiuziwe mbuzi kwenye gunia," alisema.

Akijibu swali la na mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kama malengo yake aliyobainisha katika kitabu hicho yatafanikiwa kutokana na Watanzania wengi kutokuwa na utamaduni wa kujisomea alisema: "Sifa ya Mwalimu Nyerere alikuwa na dhana ya kuandika maandiko lakini si kweli kwamba Watanzania hawasomi, hapana, ukiangalia hata magazeti sasa yameongezeka, wangekuwa hawasomi yangekuwa magazeti mawili tu. Ila wanasoma mambo yanayowahusu na tumeona kitabu hiki kilivyopokewa sikutarajia na wengine sasa waandike maandiko ili wananchi waweze kuwafahamu."

Kuhusu uhusiano wake na Rais Mwinyi kutokana na kuandika dibaji katika kitabu hicho na iwapo anamuunga mkono katika harakati zake za urais, Makamba alijibu, "Hapana na nisingependa kuzungumza kwa niaba yake na yeye kukubali kuandika dibaji kuwa yuko nyuma yangu, siyo kweli na nisingependa kumwingiza katika siasa zetu lakini maelezo yake yanaeleweka... tusipende kumkwaza."

Katika dibaji ya kitabu hicho, Mzee Mwinyi alisema Makamba anaonekana dhahiri ameandaliwa au amejiandaa vilivyo kuwa kiongozi mkubwa wa nchi.

Mzee Mwinyi anasema kitabu hicho kimemfanya amfahamu zaidi kiongozi huyo kuliko awali alipokuwa kama kiongozi ndani ya chama na Serikali.

Anaeleza kufarijika kwake kuona nchi na Rais Kikwete wameendeleza utamaduni aliouanzisha Mwalimu Nyerere na kuendelezwa naye wa kuwaamini vijana na kuwapatia fursa za uongozi ili kuwaandaa kuongoza nchi.

Chanzo: Mwananchi
 
Alichokosea ni kujihakikishia kushinda, kawadanganya na wenzie eti kukua kwa demokrasia, waambie chama lao linachukiwa sana kwa u vampire wake.
 
True,hata kushindwa haitakuwa ajabu kupata 40%,kuna vijiji haikupata hata mjumbe mmoja,japo uchaguzi ulifanywa siri fulani bila kutangazwa ba kupewa umuhimu unaostahili
 
Kwaheri ccm, tulikupenda, lakini nguvu ya umma imekupenda zaidi.
 
Makamba bhana anajitekenya nakucheka mwenyewe,hivi hizo asilimia 57,60,na 77 atazitoa wapi?.Najua hata yeye anafahamu kwamba Ccm imeshakufa haitapata hata 40 hata wakiongeza nazile zakawaidayao!
 
Na hata huo ushindi si ushindi kwa sababu wanatumia mabavu kupitia vyombo vya dola kupindisha sheria mbali mbali za uchaguzi ikiwemo kutoa rushwa, kufuta majina ya wapiga kura, kunyanyasa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, kutumia polisi, jeshi, FFU na Tume ya MACCM ya uchaguzi kuiba kura na kuchakachua chaguzi. Bila kufanya haya basi majimbo mengi watashindwa kwa kiwango cha juu kabisa.
 
Tatizo hamfahamu kwamba Januari ameeleza uhalisia uliopo kwenye siasa za dunia! Ni Tanzania peke yake ambako upinzani huwa unashindwa vibaya! Nchi yoyote yenye demokrasia hata kama ni ya magumashi kama Tanzania huwezi kukuta chama kinaingia madarakani na ushindi wa kuanzia 60% na kuendelea. Ingawaje wafuasi wa upinzani wanajipa matumaini lakini Tanzania ni moja ya nchi ambazo upinzani hawana cha kujivunia! Nchi nyingi zilizotuzunguka na majirani zetu wengine pamoja na kwamba hata huko nako hakuna demokrasia iliyokomaa lakini bado upinzani umefanikiwa kufanya makubwa... kuanzia Kenya, Malawi, Zambia. Na endapo Uganda wangekuwa na demokrasia angalau sawa na ya TZ, Mu-7 leo asingekuwa madarakani... hali kadhalika kwa Mugabe.

Kati kati ya kashfa mzito ya Escrow lakini bado CCM wameweza kubeba zaidi ya 70% ya vijiji na vitongoji... hata kama kuna visingizio vya hapa na pale vya kukwepa ukweli lakini bado ni aibu kwa CCM kusinda hata kwa 50% wakati uchaguzi unafanyika kati kati ya kashfa mzito za ufisadi! Kwa bahati mbaya sana, wafuasi nao wameendelea kumeza kila wanachombiwa na viongozi na matoke yake ni kuendeleana kupeana force hopes badala ya kusema ukweli ili watu waendelee kupigana! By the way, hata ikiwa CCM mwaka huu watashinda kwa 51% bado wala sio suala la kujivunia kwa upinzani coz' lengo la upinzani sio kuwa wapinzani waliompelekesha CCM bali kuiondoa CCM lakini kwa jinsi watu wasivyojitambua, ikitokea CCM imeshinda kwa ushind mwembamba upinzani watafurahia kwamba "mwisho wao umekaribia...!"
 
..Kenya wao wanachagua kwa kuangalia KABILA.

..aliyeunda coalition na Wakikuyu ndiye mwenye nafasi kubwa kushinda uchaguzi.

..kwa hapa bongo kuna kazi kubwa kushinda uchaguzi. inaelekea wananchi wamejisalimisha kwa CCM na hata wafanywe nini na chama hicho hawawezi kukitupa mkono.
 
Mkuu NasDas, nadhani umechambua kiasilimia zaidi kuliko kiuhalisia.

Je unaamini Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ipo huru kama, Malawi, Zambia na kwingineko.?

Je Mazingira magumu ya upinzani Tanzania ni Sawa na hizo nchi tajwa.?
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hamfahamu kwamba Januari ameeleza uhalisia uliopo kwenye siasa za dunia! Ni Tanzania peke yake ambako upinzani huwa unashindwa vibaya! Nchi yoyote yenye demokrasia hata kama ni ya magumashi kama Tanzania huwezi kukuta chama kinaingia madarakani na ushindi wa kuanzia 60% na kuendelea. Ingawaje wafuasi wa upinzani wanajipa matumaini lakini Tanzania ni moja ya nchi ambazo upinzani hawana cha kujivunia! Nchi nyingi zilizotuzunguka na majirani zetu wengine pamoja na kwamba hata huko nako hakuna demokrasia iliyokomaa lakini bado upinzani umefanikiwa kufanya makubwa... kuanzia Kenya, Malawi, Zambia. Na endapo Uganda wangekuwa na demokrasia angalau sawa na ya TZ, Mu-7 leo asingekuwa madarakani... hali kadhalika kwa Mugabe.

Kati kati ya kashfa mzito ya Escrow lakini bado CCM wameweza kubeba zaidi ya 70% ya vijiji na vitongoji... hata kama kuna visingizio vya hapa na pale vya kukwepa ukweli lakini bado ni aibu kwa CCM kusinda hata kwa 50% wakati uchaguzi unafanyika kati kati ya kashfa mzito za ufisadi! Kwa bahati mbaya sana, wafuasi nao wameendelea kumeza kila wanachombiwa na viongozi na matoke yake ni kuendeleana kupeana force hopes badala ya kusema ukweli ili watu waendelee kupigana! By the way, hata ikiwa CCM mwaka huu watashinda kwa 51% bado wala sio suala la kujivunia kwa upinzani coz' lengo la upinzani sio kuwa wapinzani waliompelekesha CCM bali kuiondoa CCM lakini kwa jinsi watu wasivyojitambua, ikitokea CCM imeshinda kwa ushind mwembamba upinzani watafurahia kwamba "mwisho wao umekaribia...!"

....kama wana ccm na serikali wanajiamini toka moyon ushindi wanaopata kila siku ni wa halali basi wakubali maombi ya siku nyingi ya kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi tuone kama upinzani hawatakua na chako.

Leo hii nani acyejua kwamba zenji ccm uwa wanashindwa ila ubabe ndo unapga tafu.

Uchaguzi unasimamiwa na mkurugenzi afu inashangilia kwamba umeshinda kwa kishindo, tuache mbinu chafu ccm wakubali uwepo wa tume huru tuone hyi rudhaa wanayodai wananchi uwapa kama ipo au la
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kumbe anatambua hilo mbona anapoteza muda wake wakati ccm imeshakufa
 
Na hata huo ushindi si ushindi kwa sababu wanatumia mabavu kupitia vyombo vya dola kupindisha sheria mbali mbali za uchaguzi ikiwemo kutoa rushwa, kufuta majina ya wapiga kura, kunyanyasa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, kutumia polisi, jeshi, FFU na Tume ya MACCM ya uchaguzi kuiba kura na kuchakachua chaguzi. Bila kufanya haya basi majimbo mengi watashindwa kwa kiwango cha juu kabisa.

Heshima yako mkuu ccm bila vyombo vya ni na karatasi hawana nguvu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Heshima ikurudie na wewe Mkuu. Hilo wanalijua fika Mkuu ndio sababu wakaamua kufanya ujambazi na uhuni wao ili kuchakachua maoni ya katiba mpya yaliyokusanywa na Tume ya Warioba ili waweze kutumia mabavu kung'ang'ania madaraka.

Heshima yako mkuu ccm bila vyombo vya ni na karatasi hawana nguvu.
 
Kauli za kutabiri ni chama gani kitashinda na kwa asilimia ngapi katika uchaguzi ujao wa kushika dola ni kuvurumka na viashiria vya upeo mdogo wa uamuzi unaochangiwa na mapungufu mengi ukiwemo uchu wa uongozi. Ni vizuri tujifunze kubashiri na kutoa kauli zinazogusa hatima ya nchi yetu kutokana na tafiti za kuthibitishwa.

Katika swala zima la kumpata Mtanzania mahiri atakayetuongoza kwenye maendeleo ya kasi zaidi, umefika wakati sasa wale walio na dhamira ya uongozi huo wapimwe pia kwa kueleza mikakati na uwezo wao kwenye midahalo ya pamoja ya wazi kuanzia hatua ya uteuzi ndani ya vyama vyao.
 
....kama wana ccm na serikali wanajiamini toka moyon ushindi wanaopata kila siku ni wa halali basi wakubali maombi ya siku nyingi ya kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi tuone kama upinzani hawatakua na chako.

Leo hii nani acyejua kwamba zenji ccm uwa wanashindwa ila ubabe ndo unapga tafu.

Uchaguzi unasimamiwa na mkurugenzi afu inashangilia kwamba umeshinda kwa kishindo, tuache mbinu chafu ccm wakubali uwepo wa tume huru tuone hyi rudhaa wanayodai wananchi uwapa kama ipo au la
Haya maneno ya Tume Huru ni kudanganyana tu lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Watanzania ni wazito! Hiyo Tume Huru itatoka wapi? Kwenye jamii hii hii ambayo hata maaskofu wanapewa mamilioni ya pesa ambayo hatujui chanzo chake? Kwa Tume hii iliyopo, ikiwa Watanzania wanaamua kwamba CCM kapumzikeni, CCM itaondoka tu! Hata hizo nchi zingine wala sio kwamba kuna Tume Huru kivile lakini wananchi waliamua kwamba enough is enough, kapumzikeni na watu wakaenda likizo!

The problem with you guys mnadanganyika na mbwembwe za JF na matokeo yake watu wanashindwa kuwajibika kwavile ukishakuwa JF, unaweza kuamini kwamba kesho JK atafungasha virago vyake na kukimbia lakini ukienda in the real world, hali unakuta tofauti! Narudia, suala la CCM kushinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakati serikali ikiwa kati kati ya kashfa mzito ya Escrow si jambo dogo la kufanya watu waishie kutoa majibu mepesi... hapa kuna tatizo.

Mkuu idawa, trust me... hakuna tofauti yoyote kati ya hizi nchi... tofauti pekee ni kwamba kwenye nchi zingine wananchi waliamua na Watanzania ni wazito katika kufanya maamuzi. Chukulia hata katika mambo ya kawaida yanayohitaji umoja kama nchi,,, ni Watanzania wachache sana watakuwa tayari katika hilo... kila mmoja ataona halimuhusu. Hivi ni lini nchi hii imewahi kutikisika kutokana na uovu ambao unaendelea kila leo? Watu hawajali! Watu tuliongea sana kuhusu Division V, who else cares now? Limeshapita... I hate to say this, hata Katiba Pendekezwa itapita... sio kwa wizi wa kura bali kwa kuwa Watanzania bado kabisa hawajaelewa what's going on! Hata hiyo 2015 CCM watachukua tena nchi... na wala sio lazima waibe kura bali majority ya Watanzania hawajali who's in power... wengi wao wala hawaoni kama kuna uhusiano wa moja kwa moja wa shughuli zao za kila siku na uongozi uliopo madarakani... masikini wanaona kama umaskini ni fate yao.... JokaKuu kwenye post yake #11 hakutaka kuwa mnafiki...amezungumza ukweli kuhusu Watanzania walivyo! Ingawaje kwa haraka haraka unaweza kuona kwamba CCM imechokwa, na in fact ni kweli imechokwa lakini bado hakuna nia ya dhati ya kuonesha kwamba kweli Watanzania wameichoka CCM... ni kana kwamba upande mmoja wameichoka CCM lakini upande wa pili ni kama hawauamini upinzani...
 
Last edited by a moderator:
Haya maneno ya Tume Huru ni kudanganyana tu lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Watanzania ni wazito! Hiyo Tume Huru itatoka wapi? Kwenye jamii hii hii ambayo hata maaskofu wanapewa mamilioni ya pesa ambayo hatujui chanzo chake? Kwa Tume hii iliyopo, ikiwa Watanzania wanaamua kwamba CCM kapumzikeni, CCM itaondoka tu! Hata hizo nchi zingine wala sio kwamba kuna Tume Huru kivile lakini wananchi waliamua kwamba enough is enough, kapumzikeni na watu wakaenda likizo!

The problem with you guys mnadanganyika na mbwembwe za JF na matokeo yake watu wanashindwa kuwajibika kwavile ukishakuwa JF, unaweza kuamini kwamba kesho JK atafungasha virago vyake na kukimbia lakini ukienda in the real world, hali unakuta tofauti! Narudia, suala la CCM kushinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakati serikali ikiwa kati kati ya kashfa mzito ya Escrow si jambo dogo la kufanya watu waishie kutoa majibu mepesi... hapa kuna tatizo.

Mkuu idawa, trust me... hakuna tofauti yoyote kati ya hizi nchi... tofauti pekee ni kwamba kwenye nchi zingine wananchi waliamua na Watanzania ni wazito katika kufanya maamuzi. Chukulia hata katika mambo ya kawaida yanayohitaji umoja kama nchi,,, ni Watanzania wachache sana watakuwa tayari katika hilo... kila mmoja ataona halimuhusu. Hivi ni lini nchi hii imewahi kutikisika kutokana na uovu ambao unaendelea kila leo? Watu hawajali! Watu tuliongea sana kuhusu Division V, who else cares now? Limeshapita... I hate to say this, hata Katiba Pendekezwa itapita... sio kwa wizi wa kura bali kwa kuwa Watanzania bado kabisa hawajaelewa what's going on! Hata hiyo 2015 CCM watachukua tena nchi... na wala sio lazima waibe kurabali majority ya Watanzania hawajali who's in power... wengi wao wala hawaoni kama kuna uhusiano wa moja kwa moja wa shughuli zao za kila siku na uongozi uliopo madarakani... masikini wanaona kama umaskini ni fate yao....
Na huo ndo ukweli wenyewe, Watanzania wengi ukiwahamasisha kwenye maandamno ya kudai haki zao wanasingizia ubize.

Tatizo nchi nchi yetu tuliamianishwa huduma za Serikali ni Masada na sio wajibu wa serikali kutupa.

Na wengi wetu hatujui kua mabilioni ya fedha zinazoibiwa ni kodi kodi zetu,kwa hiyo inakua ngumu kufatilia.

Binafsi naona wapinzani wamejitaidi sana japo sio kwa kiasi cha kuridhisha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom