Mkuu
idawa,
Nakubaliana na mistari yako mitatu ya mwanzo kwa 100% na hata hitimisho lako nalikubali ingawa si kwa asilimia nyingi sana! Nakubali kwamba wapinzani wamejitahidi lakini wapinzani walichelewa sana huko kujitahidi kiasi kwamba sioni cha kujivunia! Huwa sing'ati maneno... opposition in Tanzania is one of the most failed opposition in Africa... wamebaki kkwenye vijisababu kwamba, "tumefungwa kwa sababu uwanja ulijaa maji...!" Mie ni miongoni mwa watu nilibisha hapa wazi wazi madai kwamba Dr. Slaa alishinda kwenye uchaguzi wa 2010 na bado naendelea kubisha! Ikiwa wewe ni mfuatiliaji mzuri nadhani unakumbuka kwamba by 2010 CHADEMA hawakuwa na base yoyote kwenye mikoa yote ya Pwani na Kusini... hawakuwa na base yoyote kwenye mikoa ya Kanda ya Kati ukiondoa sehemu ndogogo ya Singida! CHADEMA si tu kwamba hawakuwahi kabisa kutengeneza base mikoa ya kusini lakini hata wakati wa kampeni alitumia saa chache tu kwenye mikoa miwili... the same situation ilikuwepo kwenye mikoa mingine! Katika mazingira kama haya nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba CHADEMA walinyang'anywa ushindi... ushindi gani na kutoka wapi? Huna base yoyote kwenye karibu nusu ya mikoa halafu utegemee kushinda? HAIWEZEKANI... Halafu kuna hoja moja hapa huwa naizungumza sana lakini watu hawailewi lakini leo nitarudia! Hadi leo hii, ukisia eneo fulani CCM wana nguvu basi tafsiri yake ni kwamba wana nguvu au maguvu kweli kweli... kwenye eneo husika wana uwezo wa kushinda hata kwa 80%+! Kinyume chake, ukisikia eneo fulani CHADEMA wana nguvu basi tafsiri yake inakuwa tofauti na hiyo inayowahusu CCM... hapa tafsiri yake ni kwamba CHADEMA wana nafasi kubwa ya kushinda lakini vilevile si kwamba CCM hawana kabisa nafasi hiyo! Na ndio maana, ukitumia mfano huo, ndipo utakuta sehemu kama Arusha Mjini pamoja na kuonekana CHADEMA wana nguvu ukweli ni kwamba hawana uhakika wa 100% kwamba watashinda... watshinda lakini kwa mbinde! Ni maeneo machache sana nchini ambazo unaweza kusema CHADEMA wana uhakika wa 80%+ kushinda na eneo hilo sio Arusha wala Kilimanjaro bali ni Mkoa wa Kigoma.
Hivyo basi, ikiwa hata yale maeneo ambayo tunasema CHADEMA wana nguvu tafsiri yake ni kwamba wana uwezo wa kushinda lakini bila kupuuza uwepo wa CCM, unaokuja kwenye maeneo tunayosema kwamba CCM wana nguvu na nguvu zake tukiamaanisha wanaweza kushinda kwa 80%+ basi hapo utaona ugumu mwingine uliopo na maeneo kama hayo bado yapo hususani Mikoa ya Pwani including Kusini hadi Mikoa ya Kanda ya Kati excluding few areas.
Lakini kwa kuwa watu hatutaki kuukubali ukweli huo, wengine wamekua wakijikita kuilaumu Mikoa ya Pwani hususani Kuisni kwamba ndio wanaipa kura CCM... hawa watu wa aina hii wala hawaelekei kwamba wanafahamu wanachoongea kwani, kuna mikoa mingi sana nchi hii ambayo inaipa kura CCM! Tukiona Iringa Mijini kuna Msigwa basi ndo tunadhani Iringa hawaipi kura CCM lakini ukiangalia overall unakuta mikoa sawa na Iringa nayo ni contributors wakubwa wa kura za CCM! Hiyo Iringa ni mfano tu lakini ipo miko kadhaa sawa na Iringa bila kuisahau Singida, Tabora, Dodoma, Morogoro... hapo sitjataja mikoa ya pwani na kusini!
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 nilitoa hoja hapa kwamba ikiwa CHADEMA wanaamini katika utawala wa majimbo ni kwanini wasitumie concept ya majimbo ili kukiimarisha chama badala ya kuendelea kulia kuibiwa kura wakati ni mjinga tu ndie anaweza kuamini kwamba chama kinaweza kuibiwa kura kwenye eneo ambalo hata Mwenyekiti wa Kitingoji hakina! Na nikasema wazi kwamba, kwavile CHADEMA wanaonekana kuwa na nguvu kubwa kwenye maeneo yenye viongozi wa kitaifa basi hata kwenye hayo majimbo wawekwe viongozi ambao tayari wana influence! Lakini kama ilivyo kawaida ya mashabiki wa CHADEMA wakakataa kata kata kwamba kwamba CHADEMA huwa wanakuwa wanakuwa na nguvu kwenye maeneo wanakotoka viongozi wa kitaifa... ukiwauliza watoe mifano ya ku-defend hoja zao wangekutajia Iringa... eti as long as Iringa Mjini ipo mikonani mwa CHADEMA ndo basi tena tunataka kuaminishana kwamba CHADEMA wana nguvu Iringa...! Hawa sidhani kama wanataka kuusikia ukweli kwamba ni mistake ya CCM wenyewe ndio ilifanya jimbo la Iringa Mjini kwenda kwa Msigwa... ni sawa na mistake iliyokuwa imefanywa na CHADEMA kwenye jimbo la Tarime! I hope CCM are smart enough kufahamu kwamba kupata jimbo la Tarime iilikuwa ni sawa na kuokota embe dodo chini ya mti wa Mwarobaini!
Sasa basi, nikatoa hoja kwamba, viongozi wale wale weenye ushawishi ndio waende kuwa viongozi wa Kanda! Akina Mnyika hakuna wanachofanya Dar es salaam zaidi ya kuishia kutoa matamko kila leo... ingekuwa matamko na Press Conference zinaimarisha chama leo hii NCCR wangekuwa wana wabunge angalau 50 bungeni kv Mbatia alikuwa ndo hodari wa Press Conference huku mwenyewe akijidanganya eti anaendesha chama kisayansi wakati ukweli ni kwamba alishindwa kuendesha chama cha siasa kisiasa! Aushukuru ujinga wa timuana timuana wa CHADEMA uliosababisha kutimuliwa ama kuondoka kwa akina Mkosamali na Kafulila otherwise CHADEMA ingekuwa ipo kaburini hivi sasa au ikiendelea na utaratibu wake wa kuendesha chama kisayansi!
Sasa basi, sijui CHADEMA wazo la kupeleka chama kwenye kanda walikuja nalo weneyewe au waliona mchango wangu ule! Lakini kinyume chake wakaacha jambo la msingi la kuwapeleka viongozi wenye ushawishi wakawe ndio viongozi wa Kanda! Hivi umeshawahi kujiuliza, endapo Zitto Kabwe(assuming bado yupo CDM) ndo angekuwa kiongozi wa Kanda ya Kusini angeleta mtikisiko gani kule? Umeshawahi kujiuliza mtu kama Mnyika ndo angekuwa Kiongozi wa Kanda ya Kati angeleta mtikisiko gani kule?
Mifano ni mingi lakini kinyume chake wakaishia kuwaweka viongozi wale wale ambao walishindwa kuleta hamsha hamsha kwenye mikoa yao ndio viongozi wenyewe wa Kanda! Sidhani kama kuna cha maana wanachofanya huko! Kusini sidhani kama wana Kanda yenye uongozi... ukiuliza wanadanganya wameamua kuwaachia CUF... ni uongo wa kijinga kabisa huu! Tangu lini chama kikaacha kusimika uongozi eti kwa sababu eneo husika chama fulani cha upinzani kina nguvu? Lakini wafuasi wa CHADEMA na nyinyi mnakubali kudanganywa... kesho na kesho kutwa wakishindwa tena, oh tumeibiwa! Kesho na keshokutwa Dr. Slaa akipata kura 200 mkoa wa Lindi mtakuja hapa kuwakashifa watu wa Lindi! Wampigie kura kwa lipi? Kwavile wanamuona kwenye TV, au? Hivi yule Mnyika leo hii angekuwa ndo kiongozi wa Kanda ya Kusini ni kweli angeshindwa kuwahudumia watu wa Ubungo? Hivi mtu kama Lissu angekuwa ndie kiongozi wa Kanda ya Kati angeshindwa kuhudumu kama Mwanasheria wa Chama? Zile kazi za ofisini za akina Mnyika pale Makao Makuu zinaweza kufanywa na watu wengi tu lakini watu wenye influence kama yeye walitakiwa wakajenge chama! Vituko vya CHADEMA vikahitimishwa kwa kumpa Professa Safari nafasi ya juu kanda ya Mashariki!!! Hivi huyu Profesa Safari tangu lini amekuwa mtu wa siasa za majukwaani? Si ndo huyu huyu alilia lia pale CUF baada ya kupata kura moja dhidi ya Lipumba? Yaani alitaka kushindina na mtu anayezunguka Tanzania!
Anyway, ingwaje ni kweli kwamba upinzani wamejitahidi lakini kwangu naona kama hawajajitahidi vya kutosha na walichelewa huko kujitahidi! Kwamba Tanzania ni nchi kubwa, SAWA! Lakini leo hii CHADEMA wala wasisizingizie ukubwa wa nchi kwavile resources walizonazo zinatosha kabisa kufika kila mahali nchi hii... badala yake akina Lema wanasubiria bunge ili wamtoe Professa Muhongo bungeni kwa nguvu... kama sio utani kuwa nini! Unaleta utani kwenye siasa wakati juzi tu hapa uchaguzi umepita na chama kimepata chini ya 30%! Na katika hili CHADEMA wataendelea kugaragazwa hadi uongozi na wafuasi wao watakapokuja kukiri kwamba bado hawajipanga sawa sawa! Hadi leo CHADEMA wanategemea vijana wakati vijana wenyewe wanashinda Instagram... are you serious? Wale wanaojifanya wana uchungu wanashinda JF wanamsubiri mwana-CHADEMA mwenzao aanzishe mchezo wa "ukuti ukuti... wa nazi wa nazi" kisha waweke duara waanze kucheza wenyewe kwa wenyewe "ukija upepo, wapepea... ukija upepo, wapepea!" Thubutu... kwa staili hii dubwasha CCM litaishia kupepea pepea tu lakini msitarajie kwamba litadondoka!!!!
c.c
JokaKuu