Makamba chupuchupu tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba chupuchupu tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 10, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Date::11/10/2008
  Makamba chupuchupu tena

  Na Ramadhan Semtawa, Dodoma
  Mwananchi

  NJAMA za kumng’oa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba, zimegonga ukuta.

  Kugonga ukuta kwa fitna hizo kumekuja siku chache baada ya baadhi ya wabunge wa CCM, kutaka katibu mkuu huyo ang’oke ili kukijenga chama.

  Matarajio ilikuwa ni kuona ajenda hiyo ikipenyezwa siku ya kwanza ya mkutano huo hapo juzi, lakini haikuwa hivyo na hadi mkutano unamalizika haikuwepo hata katika mengineyo.

  Duru za habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), zilisema ajenda hiyo haikuwepo kabisa tangu awali kuanza kwa mkutano.

  Kwa mujibu wa duru hizo, uamuzi huo wa NEC kutoipenyeza ajenda hiyo unatokana na kwamba waliokuwa wametoa maoni yao ni wabunge katika kikao chao kama wabunge wa CCM.

  “Hiyo haikuwa ajenda ya mkutano, haikuwepo kabisa, wala hakuna aliyeiingiza hata katika mengineyo,” zilisema duru hizo za kuaminika.

  Kwa mujibu wea duru hizo, ajenda za mkutano zilihusu zaidi nafasi za majina ya wanachama katika jumuiya na namna bora ya kupata wagombea kuanzia ngazi za mashina, kata na ubunge.

  Akijibu tuhuma hizo dhidi yake, Makamba aliliambia gazeti hili kwamba hakuwa na tatizo na maoni ya wabunge hao kwani ni wao waliokaa wakazungumza si chama.

  Makamba huku akionekana kuwa na matumaini na kujiamini, alisema hakuwa na wasiwasi kwani hiyo haikuwa ajenda ya chama.

  “Sikia ndugu yangu, ninachokwambia hayo yalikuwa ni maoni ya baadhi ya wabunge wa CCM, wao walikaa katika mkutano wao si chama,” alisema Makamba.

  Huku akiwa mchangamfu, aliongeza: “Sasa mimi ndiyo nakwambia hivyo, lakini unataka habari za kuokoteza mitaani kaandike,” alisema.

  Alipoelezwa kwamba, Mwananchi ni gazeti halitaki kuokoteza habari za mitaani kama mengine ndiyo limemtafuta (Makamba), alijibu: “ Hilo nafahamu ninyi ni watu makini, msisikilize habari za kuokoteza mitaani.”

  Katibu Mkuu huyo ambaye muda mwingi hupenda kuzungumza kwa kuchanganya maneno ya Kisambaa na kunukuuu aya za vitabu vya dini, alisema alishtushwa pia na taarifa kwamba juzi alitolewa katika kikao kwa muda.

  “Ninavyokwambia, mimi ndiye nimekuwa naandiki muhtasari wa mkutano, sasa nitolewe nje kivipi?” alihoji na kuongeza:

  “Hapa ninapokwambia ndiyo natoka kumsindikiza mwenyekiti akapumzike, sasa haya mambo mengine ni ya kuchekesha.”

  Makamba ni Katibu Mkuu ambaye katika uongozi wake, amekuwa akipata upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama wakielezwa kutoridhishwa na utendaji wake.

  Joto la hali hiyo lilipanda zaidi baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime, ambao CCM ilipoteza kiti hicho.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hata muwe na mipango mikali kiasi gani, bila ya kuwa na assasin hamuwezi kufanikiwa.

  Hao wabunge ni waoga, wanajadili huko bungeni, wakifika kwenye kikao ni kimya. Hakuna mwenye nguvu ya kumfunga paka kengere.

  Makamba endelea kutamba, hao wabunge waoga kiasi hicho unafikiri watakuweza?
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sasa inakuwaje chupuchupu wakati hata ajenda yenyewe haikuwasilishwa kwenye kikao?
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio njia ya kuuza magazeti bongo. Kama hauna headlines za "nguvu", biashara inaweza kukudodea siku hiyo. Its common kukuta headline inasema hivi, wakati story ya ndani ni tofauti. Kila mbuzi anakula urefu wa kamba yake. Na wajinga ndio waliwao.

  Back to the Makamba saga. Hii sio dalili nzuri hata kidogo. Whether hiyo impeachment imefanikiwa au haikufanikiwa sio hoja ya msingi sana. The argument is, watu wamekaa chini na kuona kwamba huyu jamaa hafai. Hiyo tu inatosha kukupa picha kwamba kuna tatizo. And, as far as I'm concerned, he has not delivered to the expectations of CCM supporters. Mimi nilidhani kile cheo cha Katibu Mwenezi wa chama ndio kingemfaa huyu bwana na maneno yake ya kiswahili. Cheo cha Katibu Mkuu wa CCM ni zaidi ya uwezo wake. Time will tell. Ngoja tuone nguvu ya CCM katika changuzi ndogo zinazokuja.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa CCM walikutana katika kikao cha dharura na mwenyekiti wao Pinda, ambapo walimpa ujumbe aupeleke kwa mwenyekiti Rais wa sasa, kwamba hawako radhi kwenda kwenye uchaguzi ujao na katibu Makamba, kwenye kikao hiki rais amesema ampata ujumbe bado anautafakari, na wala haikuwa agenda ndani ya huu mkutano, isipokuwa rais aliulizwa na mjumbe mmoja kama ameupoata ujumbe, akakubali kuwa anao,

  Sasa what this has to do na hii habari ya gazeti, maana naona hazina uhusiano wowote, au kuna kitu nina-miss hapa? Wabunge waliokaa chini na kumtaka Pinda afikishe ujumbe kwa rais, eti ni waoga?

  Hivi ni nini maana ya neno njama? Sio kitu kiinachofanywa kwa siri, sasa hii ishu ya wabunge inakuaje ni siri wakati kwenye kikao cha wabunge hao Makamba mwenyewe alikuwepo? Uoga wa wabunge unatoka wapi hapa baada ya kumtuma Pinda mbele ya Makamba mwenyewe?
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo basi yaani mambo mengine yanashangaza kweli
   
Loading...