Makamba atoa zawadi ya Nguruwe

Status
Not open for further replies.
duh huyu mzee sasa amechoka
Kada Makamba alinukuliwa na gazeti la Msema Kweli Toleo Na. 040, hivi: "Makamba atoa zawadi ya nguruwe kwa shule".

Licha ya Mwandishi wa gazeti hilo kushangaa kwa kitendo hicho cha kada huyu kutoa nguruwe ambayo imeharamishwa na Mungu ni kudhihirisha yale Waislamu waliyokuwa na shaka nayo kuhusu Uislamu wake wakati anafanya mambo kinyume, sio kwa bahati mbaya, ila ni kwa jeuri na kibri ya utawala wa dunia.

Waislamu siku zote tumelalamika kuhusu kuzagaa kwa nguruwe na mabucha ya nyama ya nguruwe bila mafanikio, leo katudhihirishia kwamba kufuga nguruwe ni sera maalum. Vipi shule ambayo haifugi wewe uamue kutoa nguruwe halafu uhimize Waislamu kupeleka watoto wao waje. Siku wakipangiwa kusafisha zizi nani alaumiwe?

Waislamu tumepata madhila mengi juu ya huyu Bwana tangu awe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Mtume (s.a.w.) anasema Muislamu wa kweli ni yule ambaye Waislamu wenzake wanasalimika na ulimi wake na vitendo vyake.

Yeye alikuwa mtu wa kwanza kuwatuhumu Waislamu kuiba bia wakati wa vurugu za Mwembechai, kasema tumekamata silaha Msikitini, kumbe ni vigingi vya jukwaa si hilo tu wakati anafungua Bia mpya aliwahi kusema kuwa Watanzania kunyweni Bia hii kwa wingi ili serikali ipate kodi kwa wingi.

NASAHA: Ndugu Luteni amedai mtu asitawaliwe na dini bali yeye aitawale dini; watu wanasema ukistajaabu ya Musa utaona ya Firauni, lakini mimi nasema "ukistaajabu ya Firauni utaona ya Musa, kwanza yeye sio kiongozi wa dini yoyote wala si kiongozi wa taasisi ya dini kwa hiyo fatwa yake inamrejea yeye mwenyewe.

Kama ni umaarufu wengi wameutafuta, lakini dunia wameiacha, uhai ni kama mvua, leo mafuriko kesho ukame, yeye adai tusitumie kigezo cha dini kujenga tofauti zetu.

Je, mbona hawaambii chama tawala wasitumie chama kujenga tofauti na vyama vingine mbona amekuwa mstari wa mbele kuviponda vyama vya upinzani. Je, yeye haoni anazidisha tofauti? Je, mbona kama ni msuluhishi mzuri mbona haendi kuchangia vyama upinzani.

Je, umoja unaletwa kwa kulazimishwa matakwa yako katika dini. Mungu anasema: "Na wanapokuwa na walioamini husema tumeamini na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema "Hakika sisi tu pamoja nanyi tunawacheza shere tu" (2:14)

Usifikiri Mungu ameghafirika na yale wanayoyafanya watu madhalimu Hakika Yeye anawangojea siku yatakapotoka macho.

Haki iko juu wala haikaliwi Mungu ndiye Mjuzi, mtambuzi, mwenye nguvu, mshindi, mfalme wa wafalme. Kwake hakuna kugeuka geuka haramu ni haramu na halali ni halali.
 
Maana naona kwenye ulabu tunapigana nao vikumbo na uzinzi na uasherati ndiyo usipime, je huu si unafiki?

Napenda kukujulisha kuwa sio waislamu wote wanaohusika katika huo ufedhuli kama unavyodai.

Pia kama ilivyo katika dini nyingine kuna baadhi ya waumini ambao wana imani ya dini ikiambatana na matendo mema na kuepuka ambayo MUNGU amekataza lakini pia katika upande mwingine kuna ambao ni waislamu jina tuu (nadhani hao ndo umewalenga), watu wa aina hii wako wengi sana, rika mbalimbali na sehemu mbalimbali.
Ni kama katika Imani ya Ki-Rasta: Ki uhalisia, hairuhusiwi kula nyama lakini wapo marasta ambao wanakula nyama.

Nakumbuka Sir. Isaac Newton alishawahi ku-indicate kuwa at every action there is an equal and opposite reaction (Newton's 3rd law) same same applies katika kila kitu, kwa mfano: kuna kucheka na kulia, kusimama na kukaa, kuzaliwa na kufa, rafiki na adui n.k. vivyo hinyo ndo inavyotokea katika masuala ya dini (Imani), kuna waumini wa ushabiki tuu na kuna waumini walio wacha Mungu (wanaotekeleza imani kivitendo).

Kwahiyo vitu vingine tujizuie kudandia na hoja za u-simba na u-yanga tu.. bali tuangalie the facts.

However:
Nakushauri uachane na anasa za dunia hii, kwa kuwa hapa ni mapito tuu...tuko safarini, hivyo tenda mema na uache yale yanayomchukiza bwana Mungu wako.
Pia penda kutembelea wagonjwa hospitalini, watoto yatima, na kuhudhuria mazishi mbalimbali angalau utapata kukumbuka kuwa hapa ni mapito tu.

Asanteni kwa kusoma hii post yangu.. Bwana Mungu awabariki na amani iwe nanyi.
 
Kada Makamba alinukuliwa na gazeti la Msema Kweli Toleo Na. 040, hivi: "Makamba atoa zawadi ya nguruwe kwa shule".

Licha ya Mwandishi wa gazeti hilo kushangaa kwa kitendo hicho cha kada huyu kutoa nguruwe ambayo imeharamishwa na Mungu ni kudhihirisha yale Waislamu waliyokuwa na shaka nayo kuhusu Uislamu wake wakati anafanya mambo kinyume, sio kwa bahati mbaya, ila ni kwa jeuri na kibri ya utawala wa dunia.

Waislamu siku zote tumelalamika kuhusu kuzagaa kwa nguruwe na mabucha ya nyama ya nguruwe bila mafanikio, leo katudhihirishia kwamba kufuga nguruwe ni sera maalum. Vipi shule ambayo haifugi wewe uamue kutoa nguruwe halafu uhimize Waislamu kupeleka watoto wao waje. Siku wakipangiwa kusafisha zizi nani alaumiwe?

Waislamu tumepata madhila mengi juu ya huyu Bwana tangu awe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Mtume (s.a.w.) anasema Muislamu wa kweli ni yule ambaye Waislamu wenzake wanasalimika na ulimi wake na vitendo vyake.

Yeye alikuwa mtu wa kwanza kuwatuhumu Waislamu kuiba bia wakati wa vurugu za Mwembechai, kasema tumekamata silaha Msikitini, kumbe ni vigingi vya jukwaa si hilo tu wakati anafungua Bia mpya aliwahi kusema kuwa Watanzania kunyweni Bia hii kwa wingi ili serikali ipate kodi kwa wingi.

NASAHA: Ndugu Luteni amedai mtu asitawaliwe na dini bali yeye aitawale dini; watu wanasema ukistajaabu ya Musa utaona ya Firauni, lakini mimi nasema "ukistaajabu ya Firauni utaona ya Musa, kwanza yeye sio kiongozi wa dini yoyote wala si kiongozi wa taasisi ya dini kwa hiyo fatwa yake inamrejea yeye mwenyewe.

Kama ni umaarufu wengi wameutafuta, lakini dunia wameiacha, uhai ni kama mvua, leo mafuriko kesho ukame, yeye adai tusitumie kigezo cha dini kujenga tofauti zetu.

Je, mbona hawaambii chama tawala wasitumie chama kujenga tofauti na vyama vingine mbona amekuwa mstari wa mbele kuviponda vyama vya upinzani. Je, yeye haoni anazidisha tofauti? Je, mbona kama ni msuluhishi mzuri mbona haendi kuchangia vyama upinzani.

Je, umoja unaletwa kwa kulazimishwa matakwa yako katika dini. Mungu anasema: "Na wanapokuwa na walioamini husema tumeamini na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema "Hakika sisi tu pamoja nanyi tunawacheza shere tu" (2:14)

Usifikiri Mungu ameghafirika na yale wanayoyafanya watu madhalimu Hakika Yeye anawangojea siku yatakapotoka macho.

Haki iko juu wala haikaliwi Mungu ndiye Mjuzi, mtambuzi, mwenye nguvu, mshindi, mfalme wa wafalme. Kwake hakuna kugeuka geuka haramu ni haramu na halali ni halali.

Mpuuzi mkubwa, sasa kunaubaya gani? Yaani dini ndio iwafanye viongozi wetu wasifanye mazuri?
Mnakimbilia kuabudu madini mlioletewa na kutaka kuwafanya viongozi wetu waache kuwasaidia wananchi, eti kisa dini!
Kwani hujasikia wakuu wa nchi hata hapa kuingia misikitini na makanisani?
Kwani hujawaikumuona baba wa taifa akivaa kibarakashia na kuingia msikitini na kusherekea Idd?
Watu kama nyie ndio mnataka kutusamabaratisha, kwa Makamba kutoa nguruwe hakutakukosesha chakula chako, malazi, wala kukurusdisha nyuma kimaendeleo, acha Mh Makamba afanye kazi yake na wewe uendelee kulipa kodi na kutunza famila yako.
Kama mtu huwezi kuabudu kwa kutumia uislamu ni bora uwe mpagani, maana tunawajua wanaojua kuiabudu hii dini ipasavyo bila kutaka wala kuleta shari maisshani mwetu, ndio nyie mnageuka na kuvaa mabomu kwa kuamini mtaenda kukutana na zawadi ya bikira kibao huko mbinguni!
 
Mi nakula hii kitu japo tumekatazwa aisee aacha tuuu siku niliyoanza niliapa kuwa sitoiacha na tupo wengi tunaokula kwa kujificha kipindi hiki mauzo yamepungua sehemu nyingi ila subiri kiishe itakuwa soo!
 
Ndugu Muse A Muse Umesema kweli lakini kuhusu huyu Kada Makamba sio kiongozi wa Dini ya kiislam huyu ni kiongozi wa Chama au lugha nyingine ni Mwanasiasa hausiani na mambo ya Dini hata kama kada Makamba aliwazawadia Punda wanafunzi wa shule Hatawadhuru Waislam kwani Dini ipo pale pale yey ni kiongozi wa mambo ya siasa sio kiongozi wa Dini tusichanganye Dini na Siasa kama alivyosema Baba wa Taifa Seriakali ya Tanzania haina Dini wala Haifuati Dini yoyote mtu yoyote ana uhuru wa kuabudu Dini aitakayo hakuna wa kulazimishwa kuingia Katika Dini kila mtu Atabeba mzigo wake mwenyewe siku ya hukumu mwache Kada Makamba Mwenyeezi Mungu anamwamngalia iko siku Mungu atamtia kada makamba mkononi ndio itakuwa mwisho wake.

Mkuu mimi naona hakuna tija yoyote kuanza kum discuss makamba na uislam. Makamba anaangali maslahi ya nafsi yake tu haya maswala ya dini ni kupambia watu wapate kumuangalia kwa namna nyingine na sio uhalisi alioukuwa nao.

Binafsi i don't consider Makamba kuwa muislamu namuona kama mtu aliyokuwa neutral so uislam yupo na ukiristo yupo!! Naomba isimsumbua aliyeaanzisha thread hii kuwa Makamba anauchafua Uislam ila anajichafua yeye!!
 
Mi nakula hii kitu japo tumekatazwa aisee aacha tuuu siku niliyoanza niliapa kuwa sitoiacha na tupo wengi tunaokula kwa kujificha kipindi hiki mauzo yamepungua sehemu nyingi ila subiri kiishe itakuwa soo!
"Ambao waliifanya dini yao kuwa pumbao na mchezo na maisha ya Dunia yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kma walivyousahau mkutano wa siku yao hii na kwa sababu ya kule kuzikataa Aya zetu" Quran:7:51
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom