Makamba ataka TTCL ichunguzwe na CAG

Makamba ataka TTCL ichunguzwe na CAG

kwanza tuleteeeni CAG report ya mwisho on TTCL kisha tujue yalisemwa yepi
 
Corporate governance hapa nchini ni ovyo kabisa na hii inatokana na ujinga wa kila kitu na mtu kuteuliwa na rais, na muda mrefu naona Mtendaji mkuu wa TTCL somebody ISSA anakaimu kwa muda mrefu nafikri hata miaka 10 inafika, je huoni utawala bora?. ni ujinga tu.TTCL inauwezo wa kukusanya fedha za kufa mtu kwa kutoa huduma chache kama vile Data telecommunication tu kwa makampuni mbali na voice lakini ulaji na strategizing ni ovyo.Je Msajili wa Hazina anafanya nini kama kampuni haikaguliwi na wakaguzi wa ndani na wa nje ?.

Anaitwa Said Amir Said
 
january Makamba TTCL matatizo makubwa yanaanzia kwa mmiliki wake. SERIKALI. Kama mlikubali kucheza tune ya wimbo wa Airtel wakati TTCL ilipotaka udhamini wa mkopo, hapo ndipo kosa kubwa lilipoanzia.
Serikali ni kama baba aliyetelekeza mwanae. Sijawai kuona mzazi asiye na uchungu na mwanae. Nimeiona kwa serikali ya ccm tu kwa issue ya TTCL.
 
Last edited by a moderator:
Wakimaliza auditing,investigation za ufisadi na rushwa ndani ya kampuni wawachukulie hatua wahusika then waiuze kampuni yote kwa watu binafsi wanaoweza kuiendesha,capital and good technology,serikali has no business kuendesha kampuni za simu waaachie private enterprises wafanye hizo kazi
 
Ndo anajikomba kwetu hivoo..msimuamini huyo anajaribu kufumba watu macho..wajanja wanaelewa
 
Ndo anajikomba kwetu hivoo..msimuamini huyo anajaribu kufumba watu macho..wajanja wanaelewa

Watanzania acheni kudanganyika,Makamba na wenzake ni watoa na wala rushwa wakubwa.Pale Lushoto na Bumbuli rushwa ni sawa na damu na moyo.Pale mponde kuna kiwanja cha madini kilifungiwa[2008] wananchi wasiendelee kuchimba lakini cha kushangaza akina makamba na kundi lao wanaiba usiku licha ya kiwanja hicho kulindwa na police.Ndugu zangu,kuna kazi kubwa ya kuokoa Lushoto kutoka kwenye lindi la Rushwa kwani jamii ya Lushoto pamoja na Takukuru ni sehemu ya rushwa.DEO KISANDU NI MOJA YA WATU WALIOPITIWA NA RUSHWA LUSHOTO.SOMETHING PURPOSELY SHOULD BE DONE TO MITIGATE CORUPTIO IN LUSHOTO.INAUDHI SANA TAKUKURU LUSHOTO KUBEBA RUSHWA EG.MWAKA 2010 MAJINA ZAIDI YA 30
YALIWASILISHWA TAKUKURU KWA USHAHIDI WA RUSHWA ALIYOTOA Shekifu[ Kisandu na mzee Mshangama walipewa majina haya] lakini at the end nao wamemezwa na rushwa.HIVYO JANUARI ASITHUBUTU KUMNYOOSHEA MTU KIDOLE DHIDI YA RUSHWA KWANI VIDOLE VI3 VINAMUONESHA YEYE KWA UDAU WA RUSHWA.
 
Makamba mwenyewe ni wakuwajibisha muda wote ni kupiga picha kwenye bajaji ili aweke kwenye twitter na Facebook
 
tunasubiri kwa hamu maamuzi ya bodi hiyo tukufu............
 
na tutashangaa sana tusiposikia watu wamepigwa chini pale.............
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknoloji, January Makamba, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuichunguza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Makamba alitoa agizo hilo jana baada ya kukutana na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao waliwasilisha matatizo, changamoto na kuwataja hadharani watu wanaoihujumu kampuni hiyo ikiwemo menejimenti.

Alisema endapo yaliyosemwa na wafanyakazi yatabainika kuwa ni ya kweli, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.

“Hawa ni wa kufungwa pingu si wa kuwalea, ni lazima wawajibishwe kama ni kweli kuna watu wanaihujumu kampuni kwa kiasi hiki na mimi taarifa nilikuwa nazipata siku nyingi na wafanyakazi waliniomba nikutane nao ili wanielezee shida zao,” alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo kwa sasa katika kampuni hiyo hatoshangaa kuona kwamba bodi inakataa kupitisha uamuzi wa kufanyiwa ukaguzi ndani ya kampuni hiyo.

Aidha alisema kuwa anatarajia kuvunja uongozi mzima wa kampuni hiyo na kuweka mpya huku akielezea pia uchunguzi utakaofanyika utategemeana na maamuzi ya bodi ambayo atakutana nayo keshokutwa.

Awali wafanyakazi wakiwakilishwa na Lucas Ishengoma, walisema walikusanya sh bilioni 79.9 katika ofisi ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, lakini sh bilioni tatu hazikuonekana na kwamba zimetafunwa na wajanja.

“Kila mwezi tunafanya majumuisho na tulipata sh bilioni 7.9 Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, tulipotaka kujua fedha ziko wapi uongozi ukawa unatisha watu kuhamishwa na kuwabambikia kesi. Hii ni hatari waziri, ingilia kati,” alisema.

Alisema wanataka kubadilishiwa meneja wao Karim Babhia kupelekwa Mkoa wa Mwanza kutokana na kuhoji fedha zilipokwenda, kitendo alichoeleza kuwa ni cha unyonyaji.

Someni tena hayo maneno yaliyosisitizwa halafu mtaniambia kama alieyazungumza ni kiongozi anaejua anachokiongea! Halafu pia sijui kama ana mamlaka ya kuiagiza ofisi ya CAG na TAKUKURU.
 
Na majibu ya kisisiasa. Uchunguzi ukimamikilika, na kama kweli utafanyika, utasikia hadithi nyingine. TTCL in bodi pamoja na mahesabu yake kukaguliwa, Je siku sote hizi walikuwa hawaoni. Ikiwa kuna baadhi ya vigogo wa CCM wakikutwa wamo si mambo yataishia hapo.
Bodi inateuliwa na wizara hivo kelele za nini wakati uwezo wa kuivunja bila kuomba ridhaa yetu wanao?
 
tunashukuru bodi imewapiga chini CEO na machifu wake wasiachwe ivi ivi wachunguzwe kisha washtakiwe mabadiliko hayo yamefanyika leo hii kamugisha kazaura kateuliwa kuwa CEO mpya
 
Hivi nilisikia wanajiandaa kuzindua Mitambo ya GSM wamefikia wapi? Maana Huawei waliwaingiza cha kike na hii technologia walio nayo sasa japo ndio Best Duniani.
 
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknoloji, January Makamba, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuichunguza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Makamba alitoa agizo hilo jana baada ya kukutana na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao waliwasilisha matatizo, changamoto na kuwataja hadharani watu wanaoihujumu kampuni hiyo ikiwemo menejimenti.

Alisema endapo yaliyosemwa na wafanyakazi yatabainika kuwa ni ya kweli, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.

“Hawa ni wa kufungwa pingu si wa kuwalea, ni lazima wawajibishwe kama ni kweli kuna watu wanaihujumu kampuni kwa kiasi hiki na mimi taarifa nilikuwa nazipata siku nyingi na wafanyakazi waliniomba nikutane nao ili wanielezee shida zao,” alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo kwa sasa katika kampuni hiyo hatoshangaa kuona kwamba bodi inakataa kupitisha uamuzi wa kufanyiwa ukaguzi ndani ya kampuni hiyo.

Aidha alisema kuwa anatarajia kuvunja uongozi mzima wa kampuni hiyo na kuweka mpya huku akielezea pia uchunguzi utakaofanyika utategemeana na maamuzi ya bodi ambayo atakutana nayo keshokutwa.

Awali wafanyakazi wakiwakilishwa na Lucas Ishengoma, walisema walikusanya sh bilioni 79.9 katika ofisi ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, lakini sh bilioni tatu hazikuonekana na kwamba zimetafunwa na wajanja.

“Kila mwezi tunafanya majumuisho na tulipata sh bilioni 7.9 Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, tulipotaka kujua fedha ziko wapi uongozi ukawa unatisha watu kuhamishwa na kuwabambikia kesi. Hii ni hatari waziri, ingilia kati,” alisema.

Alisema wanataka kubadilishiwa meneja wao Karim Babhia kupelekwa Mkoa wa Mwanza kutokana na kuhoji fedha zilipokwenda, kitendo alichoeleza kuwa ni cha unyonyaji.

Na hiyo RIPORT itapatikana kweli AU itaota VUMBI na Majina ya WAHALIFU SHIDA kuyaona...

Kwasababu; Ni Lazima anawajua fika VIONGOZI Wauza na Wapenda Unga Nchini lakini hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa...
 
mgomba101 ni 79.9 au 7.9? Jisome ulichotuletea halafu utuwekee sawa ipi ni sahihi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom