Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknoloji, January Makamba, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuichunguza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Makamba alitoa agizo hilo jana baada ya kukutana na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao waliwasilisha matatizo, changamoto na kuwataja hadharani watu wanaoihujumu kampuni hiyo ikiwemo menejimenti.
Alisema endapo yaliyosemwa na wafanyakazi yatabainika kuwa ni ya kweli, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.
"Hawa ni wa kufungwa pingu si wa kuwalea, ni lazima wawajibishwe kama ni kweli kuna watu wanaihujumu kampuni kwa kiasi hiki na mimi taarifa nilikuwa nazipata siku nyingi na wafanyakazi waliniomba nikutane nao ili wanielezee shida zao," alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo kwa sasa katika kampuni hiyo hatoshangaa kuona kwamba bodi inakataa kupitisha uamuzi wa kufanyiwa ukaguzi ndani ya kampuni hiyo.
Aidha alisema kuwa anatarajia kuvunja uongozi mzima wa kampuni hiyo na kuweka mpya huku akielezea pia uchunguzi utakaofanyika utategemeana na maamuzi ya bodi ambayo atakutana nayo keshokutwa.
Awali wafanyakazi wakiwakilishwa na Lucas Ishengoma, walisema walikusanya sh bilioni 79.9 katika ofisi ya Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, lakini sh bilioni tatu hazikuonekana na kwamba zimetafunwa na wajanja.
"Kila mwezi tunafanya majumuisho na tulipata sh bilioni 7.9 Dar es Salaam, Mkoa wa Kusini, tulipotaka kujua fedha ziko wapi uongozi ukawa unatisha watu kuhamishwa na kuwabambikia kesi. Hii ni hatari waziri, ingilia kati," alisema.
Alisema wanataka kubadilishiwa meneja wao Karim Babhia kupelekwa Mkoa wa Mwanza kutokana na kuhoji fedha zilipokwenda, kitendo alichoeleza kuwa ni cha unyonyaji.