Makamba amwandikia barua Pinda

Makamba amwandikia barua Pinda

Njopa

Senior Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
192
Reaction score
30
What Goes around comes around. Magamba sasa wanazinduka nao wnapata kibano kwa amri ya Waziri Mkuu wao..........................

MBUNGE wa Bumbuli (CCM), January Makamba, amemuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumuelezea chanzo kilichosababisha vurugu kati ya wananchi wa jimbo lake na polisi katika Kiwanda cha Chai cha Mponde, kilichopo katika Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga.


Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara jimboni humo, siku moja baada vurugu hizo kutokea, ambazo ziliwahusisha wananchi na Jeshi la Polisi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa vibaya kwa risasi na wengine kushikiliwa na jeshi hilo.

Mgogoro wa kiwanda hicho umedumu kwa muda mrefu kutokana na wakulima, wakiungwa mkono na mbunge wao kudai kusomewa mahesabu yanayotokana na uzalishaji wa kiwanda chao, hatua ambayo haijawahi kutekelezwa.

Kutokana na tukio la sasa, Makamba alisema aliamua kumuandikia barua ndefu Waziri Mkuu akieleza chanzo na hali inavyoendelea kuhusu mgogoro wa kiwanda hicho cha Chai.

Pamoja na hilo, Makamba pia alihoji uamuzi wa kutaka kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli akisema: “Niliposikia Halmashauri inavunjwa nilishangazwa, unapofuta halmashauri maana yake unawaadhibu wananchi, na pia unafuta madiwani wa kata zote 16, wala msiwe na wasiwasi, nitasimama kuhakikisha halmashauri yetu inaendelea, kama wanavyodhani wao wapo karibu na wakubwa na sisi wakubwa hao tuliwaomba na wakatupa halmashauri, kwa hiyo nasi tupo karibu nao,” alisema Makamba.

Pia alishangazwa na nguvu kubwa kutumika ili kiwanda kifunguliwe, pamoja na mambo mengine, alihoji kilichopo ndani ya kiwanda hicho, mpaka kufikia hatua ya bunduki kutumika ili kifunguliwe.

Alisema mwekezaji aliyekuwa anaendesha kiwanda hicho amekuwa akimfuata mara kwa mara kumtaka aruhusu gari moja ambalo linadaiwa kuwa na mzigo liondoke ili aachane na kiwanda hicho.

“Jamani chai ni yenu, kiwanda ni chenu, inakuwaje yatumike matumizi makubwa kiasi hiki mpaka kufikia kujeruhi watu kwa ajili ya kushinikiza kiwanda kifunguliwe, hatua hii inanifanya nijiulize kilichomo ndani mpaka nguvu zote hizi zitumike na wakati azma ya kufunga kiwanda ilikuwa ni maridhiano ya wakulima na mwekezaji?

Alisema hata kama akiitwa mchochezi, mhaini, lakini yeye ataendelea kuwa upande wa wananchi na hivyo aliomba matusi yote yasemwe juu yake, lakini wananchi wake wasiumizwe.

Kiwanda cha Chai cha Bumbuli, kinaendeshwa kwa ubia baina ya wananchi wa Bumbuli chini ya Ushirika wa Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) na mwekezaji, Nawab Mullah, ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Chai ya Lushoto
 
Na bado watazidi kujichanganya mpaka kufika 2015 hakuna mtu hata mmoja mwenye hamu na magamba!
 
Aliandika barua au report? Kama kumueleza Pinda, alishindwa nini kumpigia simu na wakazungumza. Hawa jamaa wanatia aibu kuwasikiliza
 
Mpuuzi sana Makamba walivunja vunja halmshauri Mwanza na Ilemela wamenyang,anya halmashauri na kumpa mwendawazimu kwao anaona haifai lakini hapa jamvini alikuwa anatamba akome
 
Dalili mbaya

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na bado watazidi kujichanganya mpaka kufika 2015 hakuna mtu hata mmoja mwenye hamu na magamba!

Kuna hadithi kwenye Biblia ila nimesahu ni kitabu gani ambapo baada ya wana wa Israeli kumwomba Mungu usbindi dhidi ya maadui zao waliokuwa wengi, Mungu alichofanya ni kuwafanya wale maadui kugeukiana na kupigana hadi kuuana. Israeli wakawa wameshinda vita wakaenda kuteka nyata. Ndicho ninachokiona kwenye chama tawala. Wananyukana na kugeukana. Hii ni kwa faida ya nani? Tafakari.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
What Goes around comes around. Magamba sasa wanazinduka nao wnapata kibano kwa amri ya Waziri Mkuu wao..........................

MBUNGE wa Bumbuli (CCM), January Makamba, amemuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumuelezea chanzo kilichosababisha vurugu kati ya wananchi wa jimbo lake na polisi katika Kiwanda cha Chai cha Mponde, kilichopo katika Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga.


Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara jimboni humo, siku moja baada vurugu hizo kutokea, ambazo ziliwahusisha wananchi na Jeshi la Polisi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa vibaya kwa risasi na wengine kushikiliwa na jeshi hilo.

Mgogoro wa kiwanda hicho umedumu kwa muda mrefu kutokana na wakulima, wakiungwa mkono na mbunge wao kudai kusomewa mahesabu yanayotokana na uzalishaji wa kiwanda chao, hatua ambayo haijawahi kutekelezwa.

Kutokana na tukio la sasa, Makamba alisema aliamua kumuandikia barua ndefu Waziri Mkuu akieleza chanzo na hali inavyoendelea kuhusu mgogoro wa kiwanda hicho cha Chai.

Pamoja na hilo, Makamba pia alihoji uamuzi wa kutaka kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli akisema: “Niliposikia Halmashauri inavunjwa nilishangazwa, unapofuta halmashauri maana yake unawaadhibu wananchi, na pia unafuta madiwani wa kata zote 16, wala msiwe na wasiwasi, nitasimama kuhakikisha halmashauri yetu inaendelea, kama wanavyodhani wao wapo karibu na wakubwa na sisi wakubwa hao tuliwaomba na wakatupa halmashauri, kwa hiyo nasi tupo karibu nao,” alisema Makamba.

Pia alishangazwa na nguvu kubwa kutumika ili kiwanda kifunguliwe, pamoja na mambo mengine, alihoji kilichopo ndani ya kiwanda hicho, mpaka kufikia hatua ya bunduki kutumika ili kifunguliwe.

Alisema mwekezaji aliyekuwa anaendesha kiwanda hicho amekuwa akimfuata mara kwa mara kumtaka aruhusu gari moja ambalo linadaiwa kuwa na mzigo liondoke ili aachane na kiwanda hicho.

“Jamani chai ni yenu, kiwanda ni chenu, inakuwaje yatumike matumizi makubwa kiasi hiki mpaka kufikia kujeruhi watu kwa ajili ya kushinikiza kiwanda kifunguliwe, hatua hii inanifanya nijiulize kilichomo ndani mpaka nguvu zote hizi zitumike na wakati azma ya kufunga kiwanda ilikuwa ni maridhiano ya wakulima na mwekezaji?

Alisema hata kama akiitwa mchochezi, mhaini, lakini yeye ataendelea kuwa upande wa wananchi na hivyo aliomba matusi yote yasemwe juu yake, lakini wananchi wake wasiumizwe.

Kiwanda cha Chai cha Bumbuli, kinaendeshwa kwa ubia baina ya wananchi wa Bumbuli chini ya Ushirika wa Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) na mwekezaji, Nawab Mullah, ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Chai ya Lushoto

...M4C ...ni habari njema kwa watu wote.....

....rohoni unaikubali....Mungu hali pilau....
.
 
makamba ni kiongozi anayeangalia maslahi ya wananchi wake.
 
Last edited by a moderator:
What Goes around comes around. Magamba sasa wanazinduka nao wnapata kibano kwa amri ya Waziri Mkuu wao..........................

MBUNGE wa Bumbuli (CCM), January Makamba, amemuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumuelezea chanzo kilichosababisha vurugu kati ya wananchi wa jimbo lake na polisi katika Kiwanda cha Chai cha Mponde, kilichopo katika Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga.


Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara jimboni humo, siku moja baada vurugu hizo kutokea, ambazo ziliwahusisha wananchi na Jeshi la Polisi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa vibaya kwa risasi na wengine kushikiliwa na jeshi hilo.

Mgogoro wa kiwanda hicho umedumu kwa muda mrefu kutokana na wakulima, wakiungwa mkono na mbunge wao kudai kusomewa mahesabu yanayotokana na uzalishaji wa kiwanda chao, hatua ambayo haijawahi kutekelezwa.

Kutokana na tukio la sasa, Makamba alisema aliamua kumuandikia barua ndefu Waziri Mkuu akieleza chanzo na hali inavyoendelea kuhusu mgogoro wa kiwanda hicho cha Chai.

Pamoja na hilo, Makamba pia alihoji uamuzi wa kutaka kuivunja Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli akisema: "Niliposikia Halmashauri inavunjwa nilishangazwa, unapofuta halmashauri maana yake unawaadhibu wananchi, na pia unafuta madiwani wa kata zote 16, wala msiwe na wasiwasi, nitasimama kuhakikisha halmashauri yetu inaendelea, kama wanavyodhani wao wapo karibu na wakubwa na sisi wakubwa hao tuliwaomba na wakatupa halmashauri, kwa hiyo nasi tupo karibu nao," alisema Makamba.

Pia alishangazwa na nguvu kubwa kutumika ili kiwanda kifunguliwe, pamoja na mambo mengine, alihoji kilichopo ndani ya kiwanda hicho, mpaka kufikia hatua ya bunduki kutumika ili kifunguliwe.

Alisema mwekezaji aliyekuwa anaendesha kiwanda hicho amekuwa akimfuata mara kwa mara kumtaka aruhusu gari moja ambalo linadaiwa kuwa na mzigo liondoke ili aachane na kiwanda hicho.

"Jamani chai ni yenu, kiwanda ni chenu, inakuwaje yatumike matumizi makubwa kiasi hiki mpaka kufikia kujeruhi watu kwa ajili ya kushinikiza kiwanda kifunguliwe, hatua hii inanifanya nijiulize kilichomo ndani mpaka nguvu zote hizi zitumike na wakati azma ya kufunga kiwanda ilikuwa ni maridhiano ya wakulima na mwekezaji?

Alisema hata kama akiitwa mchochezi, mhaini, lakini yeye ataendelea kuwa upande wa wananchi na hivyo aliomba matusi yote yasemwe juu yake, lakini wananchi wake wasiumizwe.

Kiwanda cha Chai cha Bumbuli, kinaendeshwa kwa ubia baina ya wananchi wa Bumbuli chini ya Ushirika wa Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) na mwekezaji, Nawab Mullah, ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Chai ya Lushoto
Nakuvulia kofia Makamba junior kwa kuongoza mapinduzi ya wakulima. Hapo wakulima sio wananyonywa tu bali wanaibiwa na kufanywa wajinga na mwekezaji. Kama kiwanda ni ubia kati ya wakulima na huyo mullah kwa nini hataki kuwasomea wanahisa taarifa ya mapato na matumizi? Walifikiri wakikuweka kwenye serikali hutapambana na ufisadi. Heko makamba junior
 
kote ni kulinda tu kura zake, vinginevyo January ni mnafiki na mpuuzi; Mbunge kwa mujibu wa katiba ni mwakilishi wa watanzania wote, sio wa jimbo lake tu, hivyo kama ameguswa na wananchi wake kupigwa na polisi, basi aguswe na kauli ya Pinda kwa umma wa watanzania;
 
magamba lazima yafanye kama yale ya mnara wa Babeli,yatakomaje maana itakuwa llugha gongana.
 
Kama ni mzalendo wa kweli ajiuzulu nafasi aliyonayo ajiunge na chama cha ukombozi(CHADEMA) tuikomboe TZ.
 
Aliandika barua au report? Kama kumueleza Pinda, alishindwa nini kumpigia simu na wakazungumza. Hawa jamaa wanatia aibu kuwasikiliza

Nadhani Januari anataka mambo yaende kwa maandishi zaidi ili huko waendako kuwe na ushahidi na vielelezo thabiti.
 
January Makamba atapoteza cheo chake cha unaibu waziri kwa kuwa taratibu za wakuu wake ni kutokukosolewa.
 
He is doing a right thing at a wrong place & wrong time.
Waziri hatakiwi kubishia maamuzi ya serikali yake, la sivyo ajiuzulu.

Hapo umesema ukweli mtupu mkuu Idimi. WM akitengua maamuzi ya serikali inambidi ajiuzulu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom