Makamba amrushia kombora Mzindakaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba amrushia kombora Mzindakaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Makamba amrushia kombora Mzindakaya


  na Bakari Kimwanga


  [​IMG] KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, jana amevunja ukimya na kumrushia kombora Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya, na kusema kuwa kamwe CCM haitaepuka kupata na kutathmini mawazo na michango ya wazee wa chama hicho.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana katika mahojiano maalumu, alisema sasa uzee wala ujana si sifa ndani ya CCM ila kinachotakiwa ni kupima utendaji kazi na si kuishia kulaumu bila kutoa njia ya nini kifanyike kwa makosa yanayojitokeza ndani ya CCM.
  Februari 12 mwaka huu, Dk. Chrisant Mzindakaya, alisema baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechoka, hawana upeo na mbinu za kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii.
  Alisema ndani ya CCM kuna makundi mawili ya wazee, huku akilitaja kundi la kwanza ni lile ambalo limeombwa kutokana na busara zao na kubarikiwa na Kamati Kuu ya CCM na kundi la pili ni la wazee walioomba kugombea na wanachama wakawachagua katika mikutano ya uchaguzi.
  Alisema wakati umefika kwa baadhi ya viongozi kung’atuka na kuwaachia wenye mawazo mapya kuongoza.
  Kutokana na kauli hiyo, Makamba alisema ili chama hicho kiweze kufanya kazi zake kwa mujibu wa utaratibu ni muhimu wazee wakapewa nafasi ya kutoa mchango wao kwa taifa bila kuwa na ubaguzi wa aina yoyote.
  “Mimi nishatangaza sitagombea ubunge na itakapofika mwaka 2012, nitakuwa nimeitumikia CCM kwa miaka 30, hata nafasi hii ya ukatibu mkuu niliteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama, sasa maneno yanatoka wapi jamani?
  “Mwalimu J.K. Nyerere alisema hakuna shamba linalokosa mbuyu na hapa tunaona wazi umuhimu wa wazee katika kuongoza mambo na hakuna safari iliyo salama kama si busara za wazee, hao wanaowakana wazee hawana jipya ndani ya CCM, mbona CCM imeshinda huku wanaoongoza ni wazee?” alisema Makamba.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Wote Makamba na Mzindakaya ni wachovu kwa hiyo wasichekane...................tofauti ni kuwa Mzindakaya baada ya kusoma alama za wakati aling'atuka.................................lakini Makamba naye amezisoma alama za wakati na anajiandaa kubwaga manyanga mwaka 2012.......................................kwa hiyo ngoma na drooooooooooooooooooooo......................
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,627
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Dalili za UTAWALA ULIOFITINIKA, mifisadi inaanza kurushiana makombora, FISADI NI FISADI TUUUUUUUU.
   
 4. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Safi sana, acha waanikane ikiwezekana waandaliwe na mdahalo Ha ha ha aaa!
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wacha inyukane! mwepesi atawahi kudondoka
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wameanza kugeukana.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Yah kawaida ya mbwa warafi, saa zingine wanaumana wao kwa wao
   
 8. C

  Chagula Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa Mheshimiwa Yusuf Makamba kwa nini anajitetea?
  hata Mwalimu J.K. Nyerere alikuwa ni mpinzani mkubwa sana wa RUSHWA, UBINAFSI, HONGO.

  Rais Nyerere alitetea Taifa na wananchi wake, siyo familia yake.
  Rais Nyerere alikuwa na mshahara mmoja, kama alipewa posho ilikuwa ni lazima, lakini hakutoa mikopo ya magari kwa mawaziri wala pensheni za wabunge. Nakumbuka badala ya kuwakopesha wabunge na mawaziri magari, alimwambia Mh. Rashidi kwamba " Na sisi tuanze kwenda kazini kwa kuendesha baiskeli".

  Leo makamba anawatetea wazee wa CCM, ambao hawana jipya bali rushwa, kununua viwanja kila mahali, kunyang'anya wananchi mashamba yao, kuidhinisha kupiga kura kwa karatasi za bandia, kitu ambacho enzi za mwalimu hakikuwepo.

  Mimi ningependa kumuuliza Makamba, kama kweli wazee wa CCM wana akili za kubuni mbinu mpya, yeye na Kikwete walipanda ndege wakaenda Mwanza siku ya kupiga kura. Kufika Mwanza wakakuta hapakaliki na mtu wao waliyekuwa wanamtegemea akaishia Bugando baada ya kuzirai. Kuona hivyo wakachoma wakaelekea Shinyanga na mkoba wao wa kura za bandia. Kufika Shinyanga wakakuta habari kwamba CHADEMA imeshinda, loooh! Hapo wakachanganyikiwa. Hawahawa wazee wa CCM wakamuamuru Mkurugenzi wa usimamizi wa kura atangaze kuwa ni CCM ndiyo imeshinda. Hata mtu wao wa CCM wa hapo Shinyanga akawaambia kuwa ukweli ni kwamba CHADEMA wameshinda, lakini Makamba na Kikwete wakamwambia huyo Mkurugenzi: " Sisi tunakwambia tangaza kuwa CCM imeshinda" Hizi ndizo busara za wazee wa CCM. Mkurugenzi akatangaza, kilichofatia Shinyanga watu wote tanzania nzima wanajua. Baada ya kutangazwa, huyo Mkurugenzi na familia yake akaihama Shinyanga bila kupenda, mpaka leo hatujui alikimbilia wapi.

  Makamba naposema atajiudhuru mwakani ni kwa sababu ameisha kula vya kutosha na amejiwekea misingi mizuri ya pensheni, mashamba, viwanja na majumba ya kutosha kiasi kwamba watoto wake na wajukuu hawatakuwa na shida akisha staafu.

  Hawa ndio wazee wa CCM wanaojidai eti wana mbinu mpya za kuliendeleza taifa Tanzania. Jamani hebu acheni uongo na muanze kuwa wakweli. Jaribuni kusikiliza na kuona habari zinazotokea Afrika ya kaskazini na nchi za mashariki ya kati.

  Nasema " MWOGA UKIMKIMBIZA, ATAKIMBIA LAKINI AKICHOKA NA KUSIMAMA, BASI UJUE HAPO KUNA MAWILI - KUFA AU KUPONA". Na haya ndiyo yaliyotokea Misri na Tunisia. Kwa hiyo CCM msijidanganye. Kubalini kwamba mmezeeka na nchi sasa inahitaji nguvu mpya ya VIJANA, sio wazee wanaojifikiria wao tu na familia zao badala ya kuliendeleza taifa.
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona wanagombeana fito?
   
Loading...