Wananchi wengi sana wameng'ang'ania misingi ya uongozi na kusahau kabisa mahitaji ya uongozi kama inavyowekwa wazi na falsafa za uongozi.
Unapoona mtu ambaye amewahi kufikia ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu anaongea pumba za namna hii, ujue kwamba wale wanaosema kwamba kuna ombwe la uongozi wanazungumzia Jambo kubwa sana zaidi ya ufisadii na uwajibikaji.
Katibu mkuu wa chama ambacho kinaongoza serikali iliyopo madarakani ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho hicho ana influence kubwa sana kwenye maamuzi ya nchi yetu, sasa angalia mtazamo wake jinsi ulivyo alafu ndio utajua kwamba serikali yetu imekuwa kwenye auto pilot mode kwa muda gani?
Anadanganya wananchi kwamba Siasa ni mchezo wa kudanganya danganya, ungekuwa mchezo wa kudanganya danganya wangetumia mabilioni ya fedha kwenye kampeni zao?
Kama siasa ni mchezo wa kudanganya danganya Lowasa ambaye tunategemea anaujua vizuri sana mchezo huo angekuwa radhi kutapanya mapesa yake kwa ajili ya kujipatia uongozi wa kisiasa.
Huyu mzee na chama chake wanatapatapa, Watanzania wameishagundua kwamba Mabadiliko ya maisha yao yatatokea pale tu patakapokuwa na mabadiliko katika chama cha siasa ambayo yataambatana na mabadiliko katika mfumo wa kisiasa na uongozi pia.
Watanzania wa leo wanajua kwamba alichokisema Sumaye kwamba anayetaka utajiri ajiunge na ccm alikuwa ametoa siri kubwa sana iliyokuwa ikizunguka kwenye makorido ya watawala peke yake.
Siasa ndio mtaji wa maendeleo. Hivyo watanzania tutaendelea kushiriki katika michakato ya kisiasa wakati wote, ije mvua, lije jua, lije giza, uje mwanga, siku saba za kila wiki tutaishiriki siasa, na katika hilo tutaendelea kuwabana ipasavyo watawala wa kisiasa watimize ama ahadi zao ama majukumu yao na sababu tunajua hawawezi kila tutakapopata nafasi tutawalalamikia, kuwasononokea, kuwalaumu, kuwazomea na fursa zikijitokeza kuwaondoa madarakani.