PreGE2025 Makalla: Waliohama CHADEMA tunawakaribisha CCM

PreGE2025 Makalla: Waliohama CHADEMA tunawakaribisha CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewakaribisha kujiunga na CCM Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA iliyomaliza muda wake ambao leo May 07,2025 wametangaza kuondoka CHADEMA akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na John Mremaz

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Makalla amesema hayo leo wakati akiongea na Wananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku saba mkoani humo.

Ndugu zangu Watanzania,

Nguli wa siasa za majukwaani na za kimkakati aliyefanikiwa kuisambaratisha CHADEMA kwa hoja nzito nzito Mheshimiwa CPA Amos Makalla amewakaribisha G55 kutoka CHADEMA ili waweze kujiunga na CCM chama ambacho ni kimbilio la wanyonge na wale wote wenye kuelemewa na Mizigo mizito,uonevu ,ukandamizwaji na udikteta kwenye vyama vyao.

Embu Soma hapa chini

👉CCM YAWAKARIBISHA WANACHADEMA NA G 55

•kutangaza kuhama kwa waliokua viongozi waandamizi ni uthibitisho mgogoro ndani ya Chadema

MVOMERO: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawakaribisha kujiunga na chama hicho John Mrema na wenzake kutoka katika kundi la G55 waliojiondoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 7,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku saba katika mkoa huo.

Makalla ameeleza hayo baada ya wajumbe wa Sekretarieti ya Chadema iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na Mrema kutangaza kujiondoa katika chama hicho kuanzia leo.

Makalla amebainisha kuwa amefurahishwa na kauli ya G55 kwamba walihitaji kuondoka Chadema kwa sababu wanachama hao ndoto na haja yao ni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Ameongeza pamoja na kundi hilo hawajaweka wazi ni chama gani ambacho wanania ya kwenda kujiunga nacho kati ya vyama 18 vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi, lakini Makalla alisema wanawakaribisha kuwa wanachama wapya wa CCM kwani wao wapo tayari kushiriki uchaguzi.

“Pamoja na kuondoka Chadema G-55 hamjaeleza chama mnachoenda sisi CCM tunawakaribisha milango iko wazi jiungeni na Chama cha Mapinduzi, vyama 18 vimeamua kushiriki uchaguzi kasoro chama kimoja,”amesema Makalla.

Ameongeza: “kwahiyo katika vyama 18 mnaweza kuangalia vyamba mbalimbali lakini mimi kama msemaji wa chama nawakaribisha CCM twende kwenye uchaguzi tushinde kwa kishindo”.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mwenyeji anawakaribishaje wenyeji wenzake?
CCM na G55 ni kitu kimoja, hakuna wakumkaribisha mwenzake.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewakaribisha kujiunga na CCM Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA iliyomaliza muda wake ambao leo May 07,2025 wametangaza kuondoka CHADEMA akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na John Mremaz

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Makalla amesema hayo leo wakati akiongea na Wananchi wa Mvomero Mkoani Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku saba mkoani humo.

Eeeh waende huko wakapewe majimbo ya Bure na vyeo vingine kama udc
 
Back
Top Bottom