Makala yangu no 01: Ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
KILE KINACHOENDELEA BURUNDI JE KINASADIFU HISTORIA YAKE?

Makala yangu no 01. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.

Na. Comred Mbwana Allyamtu.

Burundi ndio taifa lenye uchumi mdogo kabisa katika mataifa matano ya Afrika mashaliki ukiitoa Sudani kusini ambaye ni mwanachama mchanga ndani ya jumuiya ya Afrika mashaliki ambayo Kenya huongoza cheni ya uchumi ikifatiwa na Tanzania kisha Rwanda na ikifuatiwa na Uganda na Burundi ikishika mkia.

Pamoja na Burundi kuwa taifa dogo pia ndio taifa la nne (4) kwa umasikini duniani likiwa na pato la taifa la dola za kimalekani US$16 billion huku uchumi kwa ujumla (Economy Index) yake ukiwa ni US$ bilion 12.6 (yani nominal & ppp income index) huku ukuwaji wa uchumi kwa mwaka ni 1.39% 2015-2016 kwa mujibu wa ripot ya UNDP na IMF ya mwaka 2016. Hali ya uchumi katika taifa hilo imekuwa ikidolola kwa kasi sana toka mwaka 2015-2016 kwa kasi ya 5% kwa kila miezi mitatu (3) na hii imetokana na kuzuka kwa mashafuko mala baada ya kutokea kwa mgogoro wa kikatiba juu ya kile kinachoitwa "ukomo wa awamu ya Rais Nkurunzinza" kitu kilichopelekea hali ya sintofahamu na kupelekea jalibio la mapinduzi liloshindwa na kusababisha kuzuka kwa machafuko, mauaji na mamia ya wakimbizi kuikimbia nchi.

Ukosefu wa utulivu wa kisiasa umepelekea kukosekana kwa amani na utengamano wa kitaifa hali iliyopelekea kuongezeka kwa mauaji ya kutisha ya watu walio karibu na Rais Nkurunzinza na wale wasio muunga mkono. Binafsi nimewahi kufika Burundi na kuishi hapo kwa zaidi ya miezi minne (4) nimekuwa pale na nilijionea hali jinsi ilivyo na kuamini kuwa kile kinachoendele Burundi ni kile nchi Hiyo inachokiishi kwani naifahamu Vizuri sana Nchi ya Burundi kutokana na kuishi miji kazaa ukiwemo Bujumbura, kayanza, Muyinga, Rumonge, Nyanza Lac, Mabanda na mji wa Makanba kwani nikifika Burundi hujiona kuwa niko Tanzania kwakuwa nimekuwa maarufu sehemu izo kutokana kuwahi kuishi na ndugu na jamaa maeneo hayo.

Mbali na hilo Burundi ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Uberigiji mwaka 1962 lakin toka uhuru huo taifa hilo limekuwa likikumbwa na machafuko ya mara kwa mara ikiwemo yale ya mwaka 1961, 1963, 1968, 1972, 1993, 1994, 1997 na haya ya sasa ya mwaka 2015

HISTORIA YA BURUNDI

Burundi ambayo huko nyuma ilijulikana kama Urundi ni eneo linalopatikana katika Afrika mashaliki katika ukanda wa mashaliki ya Afrika ya kati na imepakana na DRC kwa upande wa magharibi, kusini imepakana na ziwa Tanganyika na upande wa kaskazini imepakana na Rwanda huku upande wa mashaliki imepakana na Tanzania.

Mji wake mkuu ni Bujumbura ambayo huko nyuma ulijulikana kama Usumbura wenyeji wa nchi hiyo ni kabila la Watwa (Batwa) ambao waliishi hapo toka miaka ya 300 BC na baadae kati ya miaka 110 AD na 340 AD walikuja jamii nyingine ya wabantu waliotoka kwenye misitu ya Kongo na Kameroni waliojulikana kama Wahutu (Hutu) ambao walitawanyika katika ukanda wote wa milima ya "Ruanda na Urundi" na walikuwa wawindaji na baadae wakaanza kujihusisha na shuguri za kilimo mnamo miaka ya 600 AD.

Katikati ya miaka ya 900 AD jamii kubwa ya Nilotic kutoka kwenye kikundi cha jamii ya wafugaji ya Wahamatic iliyojulikana kama Watusi (Tusi) ilianza kuvamia ukanda wote wa nyanda za mashaliki ya Afrika ya kati kuanzia aridhi ya Kalamojog, Bunyoro na Buganda huko Uganda hali iliyopelekea kuzuka kwa vita za makabila dhidi ya kabila lenyeji na kabila vamizi kwa kuwa Watusi walikuwa na mifugo kuna mahali walishindwa vibaya sana na kukibia kama katika himaya ya Kalamoja lakin kuna mahali waliwashinda wenyeji na kuanzisha himaya mfano huko Nyankole na Bunyoro.

Wingi wa idadi ya wahamiaji wa jamii ya Watusi ilipelekea kuwafanya kutafuta aridhi na kujitanua ukanda wote wa kusini mwa Afrika mashaliki ya kati kitu kilichopelekea jamii hiyo ya Watusi kufika Rwanda na hatimaye miaka ya 987 AD kufika Tanganyika maeneo ya himaya ya chifu Rumanyika na baadae Burundi. Watusi walikuwa ni wafugaji wenye makundi makubwa ya ng'ombe ambao walikuwa nakitafuta makazi bora ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Kuanza kwa uvamizi wa wazungu mwanzoni mwa miaka ya 1800 kuliifanya Burundi kutawaliwa na Ujerumani ambapo Burundi, Rwanda na Tanganyika zote zilikuwa ni nchi moja iliojulikana kama Ujerumani ya Africa mashaliki (German east Africa) ambapo baadae Burundi na Rwanda alipewa uberigiji mara baada ya vita ya kwanza ya dunia kumalizika ndipo Urundi yani Burundi na Urwanda yani Rwanda ndipo zilipo pewa koloni lingine la uberigiji kwa kile kilichoitwa "Fidia ya kushindwa vita kwa ujerumani" kupitia mkataba wa Anglo-Belgium Treaty 1919 mara baada ya (mkataba wa Verseryas).

Ujio wa mbelgiji ndio chanzo cha kuibuka kwa matabaka baina ya makabila mkubwa mawili yani Wahutu na Watusi, hapa mbeligi alianza kuwatumia Watusi katika shuguli zake za kiutawala kama makalani, walimu,maafisa wa ngazi za chini na kuwapa fursa za kijamii tofauti na ilivyo kwa kabila la Wahutu waliowengi na hii ni kutokana na kabila la Wahutu walikuwa watu wakolofi, wabishi na wakali huku Watusi walikuwa watu wakimya, wapole na wastaalabu kitu kikichopelekea wazungu kuwapenda na kuwatumia katika shuguli za utawala jambo lililopelekea kuongezeka kwa chuki baina ya hayo makabila mawili yani Watusi na Wahutu kwani Watusi waliwanyanyapaa Wahutu kwa kiasi kikubwa na chuki hiyo iliongezewa chuki maradufu na wakoloni wa kizungu (Wabeligiji) kwakuwa karibu sehemu nyingi za utawala walipewa Watusi kama Askali wa usalama, Askali wa mageleza maafisa suluhu na sehemu nyigi za utawala.

Na ilipofika miaka ya 1949 wabeligiji waliona wa badili mfumo wa utawala na kuanzisha mfumo mpya ulioitwa "Tribe clasical system of administration" na hii ndio iliyo kuja kuchochea ukabila tunaouona ukiishi leo Burundi na Rwanda kwakuwa haya mataifa yanafanani kwa karibu kila kitu. Kwa Burundi uberigiji aliwapa mamlaka Watusi na kuwabagua Wahutu huku kwa Rwanda katika miaka ya 1950 mbeligiji alianza kuwapa kipaumbele Wahutu kutokana na msukumo wa wamissionari wa kikatoriki walioanza kuwatetea Wahutu kwa kuona wao ndio wanaonyanyaswa na kubaguriwa hivyo uberigiji aliona ni vyema kuwapa msukumo Wahutu kwakuwa kipindi hiko vuguvugu la Wahutu lilikuwa kubwa. Katika miaka ya 1950 ilionekana na kudhihirika ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu waliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.

Mwami Mutara Rudahigwa aliyejiita pia Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi. 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya Wahutu na Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani mkali kutoka kwa Watutsi walio amua kumuua mwaka 1959. Mtoto wake Mwami Kigeri V. alisimikwa kwenye kiti hicho. Hatua hii ilisababisha ghasia na vurugu nchini kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V. alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda. Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu. Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali hiyo nchini Rwanda. Hiyo ilizidisha hali ya mbeligiji kuamua kuwapa mamlaka Wahutu na kuwabagua Watusi.

Ikumbukwe kuwa katika jamii hizo mbili wahutu ndio waliokuwa watawala wa himaya ya Rwanda na Burundi kabla ya kuja mzungu (mkoloni) toka kuanzia miaka ya 400 AD lakini huko Rwanda katika miaka ya 720 AD Watusi waliwashinda wahutu katika mapigano makali yaliyojulikana kama "Vita ya Abahima" (Bahimma war) na kupelekea wao kuanzisha himaya ya utawala kwa Watusi huko Uruanda (Rwanda). Kwa Burundi pia wahutu ndio waliokuwa na himaya lakin awakupewa kipaumbele na mkoloni.

Kihistoria na jeograpia nchi hizi hufanana kalibu kila kitu. Katika Burundi kutokana kukomaa kwa ubaguzi wa kikabila mkoloni alichochea hali ya ubaguzi na chuki baina ya Wahutu na Watusi.

Ubeligiji ndipo miaka ya 1950 kulianza kuzuka vuguvugu la ukombozi barani Afrika hata hivyo Burundi nayo aikubaki nyuma. Mwaka 1956 ndipo mtoto wa mfalme Mwabusta V (Mwami Mwambusa) aliojulikana kama mwana mfalime Lous Lwagasore alipo unda chama cha ukombozi kilicho julikana kwa kiingeleza kama UNION PREPARATION FOR NATION (Unioñ le prépàrasio du ñational) UPRONA.

UKOMBOZI NA UHURU KWA BURUNDI

Kama nilivyo eleza apo juu vuguvugu la ukombozi Burundi lilikwenda kwa misingi ya ukabila na utabaka.

Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya UM na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemwoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila.

Mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urubdi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee.

Baada ya uchaguzi wa 1965 mapigano yalitokea kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali kilichukua serikali.

Mwaka 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Michel Micombero aliyejitangaza kuwa rais na nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa

Mwaka 1956 kiliundwa chama cha UPRONA cha Watusi wenye misimamo ya wastani kilichoongozwa na Prince Lous Lwagasore ambaye yeye alijibainisha kupinga ubaguzi wa kikabila uliokuwa ukiishi Burundi na kutaka kuwepo na umoja wa kitaifa. Japo kuwa chama cha UPRONA kuwa cha kitusi lakini kilionekana kuwa na Wahutu wachache kilianza kukubalika na kuungwa mkono karibu na idadi kubwa ya warundi.

Mapema mwaka 13/10/1961 Princes Lous Lwagasore aliuwawa na kikaragosi wa kiberigiji mwenye asili ya kigiriki aliyejulikana kama Jean Kageorgis akishilikiana na viongozi wa chama kikichokuwa kinaungwa mkono na wabeligiji cha PDC (cristianity Democratic party) katika hotel ya Club du Lac Tanganyika mjini Bujumbura kutokana na yeye kuonekana kutaka kujenga umoja wa kitaifa na kuhatalisha maslahi ya wakoloni wa kibeligiji nchini Burundi. Mapema baadae hali ya vuguvugu ya ukombozi ilizidi hali iliyopelekea uberigiji kuamua kutoa uhuru kwa Burundi mwaka 1/7/1962. Huku chama cha UPRONA kikiongoza katika uchaguzi wa bunge wa mwanzoni na hatimaye mwaka 1966 Burundi ikawa Jamuhuri baada ya mapinduzi na Micheli Michombelo kuwa Rais.

Pamoja na uhuru machafuko yaliendele pamoja na mauaji ya baina ya makabila mawili ya watusi na wahutu na hiyo ndio imekuwa kama sifa kubwa na historia ya Burundi, inaipambanua nchi hiyo katika sura ya mgogoro wa kikabila Hakuna sifa tofauti yenye kuvuma ulimwenguni zaidi hiyo. Jina Burundi kimataifa, muktadha wa karibu ambao hujitokeza nimapigano ya wenyewe kwawenyewe, Wahutu na Watutsi.Mapigano ya Wahutu na Watutsi yalichukua nafasi kubwa tangu miaka ya 1960 na kuendelea nyakati zote mpaka mwafaka mkubwa uliopatikana mwaka 2000, chini ya msuluhishi, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,marehemu Nelson Mandela.

Mandela alichukua nafasi ya usuluhishi, baada ya kazi kubwa kuwa imeshafanywa na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati mwalimu Jurius Nyerere.

Nyerere alianza kazi ya usuluhishi wa Burundi mwaka 1995 ikiwa ni baada ya vifo vya marais wawili. Oktoba 1993, Melchior Ndadaye, mwenye asili ya Kihutu, aliyetoka kushinda Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, mwaka huo, alitawala kwa miezi minne tu, kabla ya kuuawa na wapiganaji wa Kitutsi. Baada ya Ndadaye aliyeongoza kupitia Chama cha Front for Democracy in Burundi (FRODEBU), mapema mwaka 1994, Cyprien Ntaryamira (Mhutu) alichaguliwa kabla ya mwaka huohuo, kuuawa Rwanda, wakati ndege aliyokuwa amepanda yeye na aliyekuwa Rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana, kutunguliwa na kuangushwa, ilipokuwa inakaribia kutua Uwanja wa Ndege wa Kigali.

Kifo cha Ntaryamira kilisababisha aliyekuwa Spika wa Bunge la Burundi, Sylvestre Ntibantunganya (Mhutu), achaguliwe kuwa rais kabla ya Rais wa vipindi vingi vya nchi hiyo, Pierre Buyoya, kumpindua.

Mwafaka uliopatikana mwaka 2000 chini ya Mandela ambaye aliwatumia vizuri waliokuwa marais wa Marekani na Afrika Kusini, Bill Clinton na Thabo Mbeki, ulisainiwa na aliyekuwa Rais wa Burundi, Buyoya na vikundi 13 kati ya 19 vya waasi. Mandela aliagiza vikundi vilivyokubali visaini kisha mwafaka ukatekelezwe bila kuhusisha wasusiaji ambao hata hivyo baadaye waliomba kuunganishwa kwenye uundaji wa Serikali ya Mpito. Buyoya wa Chama cha UPRONA, baada ya mwafaka aliongoza mpaka mwaka 2003 kabla ya Domitien Ndayizeye wa FRODEBU kuchaguliwa kuongoza serikali ya mpito, iliyokwenda mpaka mwaka 2005, Bunge la Burundi lilipomchagua Pierre Nkurunziza kuwa rais kwa kipindi cha miaka mitano.

Tangu Nkurunziza achukue madaraka, hali ya amani ilipatikana Burundi, shughuli za kiuchumi zilifanyika bila mashaka yoyote, huku Wahutu na Watutsi wakishirikiana kuijenga upya nchi yao ambayo wao wenyewe waliibomoa kwa sababu za chuki za kikabila. Uchaguzi Mkuu 2010 ulifanyika kwa amani japo vyama vya upinzani vililalamikia kuchezewarafu lakini hakuna mtu aliyerejea msituni.

Ila kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, Burundi imerejea kwenye machafuko. Mpaka sasa, zaidi ya watu 1,000 wanaripotia kupoteza maisha, huku tayari watu zaidi ya 250,000 wakiwa wameshaikimbia nchi yao. CNARED ni muungano wa vyama vya upinzani zaidi ya 20 nchini Burundi ambavyo vimeungana kuhakikisha matakwa ya Katiba ya Burundi yanaheshimiwa, vilevile mwafaka wa mwaka 2000 uliosimamiwa na hayati Mandela. Kwa pamoja, CNARED wanampinga Nkurunziza wakimtuhumu kusigina katiba na kukiuka kile kilichoafikiwa mwaka 2000 jijini Arusha.

Hivi karibuni, nilifanya mahojiano na Naibu Katibu Mtendaji wa CNARED, Nzeyimana Abdoul kuhusu masuala mbalimbali nchini mwake.Nzeyimama ambaye anaishi Ubelgiji, niliweza kupata mawasiliano yake kupitia maafisa wa umoja wa mataifa waliopo jijini Goma jimbo la Kivu kaskazini katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo nilipo izuru Goma siku kazaa hapo nyuma.

Akiwa uhamishoni baada ya kukimbia Burundi kutokana na machafuko ya kisiasa, anasema kuwa ripoti za wakimbizi nchini mwake zinaonesha kuwa zaidi ya watu 150,000 wamekimbilia Tanzania na wanaishi kwenye kambi tofauti za wakimbizi. “Watu zaidi 38,000 wamekimbilia Uganda na Rwanda kunawakimbizi zaidi ya 75,000, wakati huohuo, tayari watu 1,000 wameshauawa,” alisema Nzeyimana, katika mahojiano niliyofanya naye, nilipokuwa jijini Goma DRC katika ziara yangu inayoendelea ambapo sasa niko nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati katika jiji la Bangui napo nikijalibu kujionea madhala ya vita ya kidini kati kikundi cha Seleka na Antibalaka vilivyo sababisha mauaji ya kinyama kabisa na mda sio mrefu nitatoa makala juu ya hali niliyoiona huku Bangui, pia huko DRC na Rwanda.

Katika mazungumzo yangu na Nzeyimama anaonya kuwa mgogoro wa sasa wa Burundi usitafsiriwe kuwa ni wa kikabila kati ya Wahutu na Watutsi kama ambavyo ilivyozoeleka, badala yake uliopo sasa unatokana na siasa mbaya na uongozi mbaya wa Nkurunziza wa kung’ang’aniamadaraka.

“CNARED ni muungano wa vyama 23, vipo vya Wahutu na Watutsi, wote tumeungana kupinga vitendo vya Nkurunziza kukanyaga katiba na mwafaka wa Arusha. “Kwetu sisi Warundi, kutokana na historia za mapigano, tunaheshimu sana mwafaka wa Arusha, ni kama Biblia kwa Wakristo,” anasema Nzeyimana. Anaendelea: “Mimi ni Mhutu, kwa hiyo inatakiwa ifahamike kuwa mgogoro wa Burundi siyo wa kikabila, maana Serikali ipo mikononi mwa Wahutu lakini Wahutu haohao wanaongoza kuwakimbiza Wahutu wenzao.” Akifafanua kuhusu kirefu cha CNARED, Nzeyimana anasema kuwa ni muungano wa vyama vya upinzani vinavyopigania uheshimishwaji wa Mkataba wa
Arusha na Katiba.

Anasema kuwa Nkurunziza ameshindwa kuwatendea haki Warundi, kwani ukaidi wa kung’ang’ania madaraka umesababisha kuwarejesha kwenye historia ya machafuko ambayo walikuwa wameshaisahau. “Ukiachana na suala la wakimbizi na vifo, vilevile wananchi wakiishi kwa tabu kwenye kambi kwa kukosa hata faragha, wanaume na wanawake wakilala pamoja, mgogoro wa Burundi sasa hivi unahatarisha ustawi wa Afrika Mashariki, hivyo kuleta athari ya kidiplomasia. “Sasa hivi Nkurunziza anaishutumu Rwanda kuwa inachochea machafuko Burundi, hili ni jambo ambalo halipo sawa hata kidogo. Inatakiwa hata Watanzania waujue mgogoro vizuri kuwa una athari kubwa kwa Afrika Mashariki,” anasema Nzeyimana.

Akichambua athari zaidi za machafuko Burundi kiuchumi, Nzeyimana anasema kuwa wananchi sasa hivi hawafanyi shughuli zao za kiuchumi, kitu ambacho kinawaweka katika mazingira magumu ya kimaisha. “Sarafu ya Burundi, Franca, kabla ya machafuko ilikuwa inabadilishwa kwa 1,650 dhidi ya dola moja ya Marekani lakini sasa hivi dola moja ya Marekani inabadilishwa kwa franca 2,400, hali ni mbaya,” anasema Nzeyimana.

Nzeyimana ambaye amepata kuwa Naibu Meya wa Jiji la Bujumbura, anasema kuwa sasa hivi tayari vikundi vitatu vya waasi vimeshajitokeza ambavyo vinapambana na Serikali ya Burundi. “Utaona ni ndani ya muda mfupi mno.Kuna Kundi linaitwa Forebu ambalo linaongozwa na Jenerali Godefroid Niyombare, huyu alikuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Burundi, vilevile Mkuu wa Majeshi. “Jenerali Niyombare alitofautiana na Nkurunziza alipomshauri asikanyage katiba na kujiongezea muhula mwingine wa uongozi. Walipotofautiana, alikwenda msituni kuanzisha kundi lake la uasi. Sasa hii ni hatari kubwa kwa nchi kwa sababu Jenerali Niyombare ni mtu ambaye anaheshimika sana jeshini na ana ushawishi mkubwa,” anasema Nzeyimana.

Anaongeza: “Mwishoni mwa mwaka jana, waasi wa Forebu walivamia ghala kuu la silaha za kijeshi Burundi na kupora silaha nyingi na katika mapigano makali watu 100 waliripotiwa kuuawa. Hii ni hatari lakini Nkurunziza anaziba masikio. Unawezaje kugombana kirahisirahisi na mkuu wa majeshi ambaye pia ni mkuu wa usalama wa taifa?” Nzeyimana anataja vikundi vingine kuwa ni FNL cha Jenerali Aloys Nzabampema na RED-TABARA cha Jenerali Melchiade Biremba.

“Nasisitiza, Burundi hakuna mgogoro wa kikabila, ni mgogoro wa madaraka. Tamaa za Nkurunziza zinasababisha mauaji ya watu wasio na hatia pamoja na usumbufu mkubwa kwa raia," anasema Nzeyimama. Anaongeza kuwa viongozi mbalimbali wa Kihutu wamekimbia nchi, wakiwemo marais wastaafu, kuonesha kuwa japo Rais ni Mhutu, hata Wahutu wenyewe wanapata wakati mgumu. Anawataja viongozi hao kuwa ni
Ntibantunganya, Pierre Ntanyohanyuma (alikuwa Spika wa Bunge), Gervais Rufyikiri(Naibu Rais), Leonidas Hatungimana (Msemaji wa Rais) na Onesmo Naiwimana (Msemaji wa Chama cha Nkurunzia CNDD- FDD). Wengine ni Bernarol Busokozaza, Alice Nzomukunda, Marina Baramama na Fredric Bamvuginyumvira ambao wote walipata kuwa manaibu rais, vilevile Hussein Radjabu, aliyekuwa Kiongozi wa CNDD- FDD.

Rais wa Awamu ya Tatu Tanzania, Benjamin Mkapa ndiye msuluhishi wa mgogoro wa Burundi, Nzeyimana anaelezeaje imani hiyo? Anajibu: “Tuna imani kubwa na mzee Mkapa. Sisi CNARED tulikutana naye Ubelgiji Juni 10 na 11, mwaka huu, tutakutana tena Julai 10 Arusha. Anafanya kazi nzuri, tofauti na msuluhishi wa awali ambaye ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.”

Maoni yangu

Maoni yangu juu ya kile kinachoendelea Burundi ni mwiba na doa kwa jumuiya ya Afrika mashariki kama Tanzania tunahaja ya kuchukua hatua za kidpromasia ili kunusulu taifa la Burundi kwa kuchukua hatua za kidpromasia na kuanzisha mazungumzo yenye mashaliti kwa kuliona lile linaloendela Burundi ni vita kubwa na haistaili kupuuzwa hata kidogo kama inavyo puuzwa sasa kuna haja ya kutafutwa ufumbuzi wa jambo hilo kwa ukinifu ili kunusuru maisha ya warundi wasio kuwa na hatia pamoja na kuzorota kwa amani. Ikumbukwe haistaili kuufanya mgogoro huu ni wa Burundi ni lazima tukubali kuwa si jambo la ndani ya Burundi tu.

Na mwisho japokuwa sio kwa umuhimu wake kuzorota kwa amani ya Burundi ni kuchochea uzorotaji kwa uchumi wa Tanzania na kupoteza ushawishi kwa Tanzania katika turufu yetu katika nchi za maziwa makuu na kupelekea kuongezeka kwa hali ya hatari ukanda wote wa maziwa makuu.

"Mungu bariki Afrika, Mungu baliki Warundi, Mungu ibariki Burundi".

Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu.

+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email: mbwanaallyamtu990@gmail.com
 
KILE KINACHOENDELEA BURUNDI JE KINASADIFU HISTORIA YAKE?

Makala yangu no 01. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.

Na. Comred Mbwana Allyamtu.

Burundi ndio taifa lenye uchumi mdogo kabisa katika mataifa matano ya Afrika mashaliki ukiitoa Sudani kusini ambaye ni mwanachama mchanga ndani ya jumuiya ya Afrika mashaliki ambayo Kenya huongoza cheni ya uchumi ikifatiwa na Tanzania kisha Rwanda na ikifuatiwa na Uganda na Burundi ikishika mkia.

Pamoja na Burundi kuwa taifa dogo pia ndio taifa la nne (4) kwa umasikini duniani likiwa na pato la taifa la dola za kimalekani US$16 billion huku uchumi kwa ujumla (Economy Index) yake ukiwa ni US$ bilion 12.6 (yani nominal & ppp income index) huku ukuwaji wa uchumi kwa mwaka ni 1.39% 2015-2016 kwa mujibu wa ripot ya UNDP na IMF ya mwaka 2016. Hali ya uchumi katika taifa hilo imekuwa ikidolola kwa kasi sana toka mwaka 2015-2016 kwa kasi ya 5% kwa kila miezi mitatu (3) na hii imetokana na kuzuka kwa mashafuko mala baada ya kutokea kwa mgogoro wa kikatiba juu ya kile kinachoitwa "ukomo wa awamu ya Rais Nkurunzinza" kitu kilichopelekea hali ya sintofahamu na kupelekea jalibio la mapinduzi liloshindwa na kusababisha kuzuka kwa machafuko, mauaji na mamia ya wakimbizi kuikimbia nchi. Ukosefu wa utulivu wa kisiasa umepelekea kukosekana kwa amani na utengamano wa kitaifa hali iliyopelekea kuongezeka kwa mauaji ya kutisha ya watu walio karibu na Rais Nkurunzinza na wale wasio muunga mkono. Binafsi nimewai kufika Burundi na kuishi hapo kwa zaidi ya miezi minne (4) nimekuwa pale na nilijionea hali jinsi ilivyo na kuamini kuwa kile kinachoendele Burundi ni kile nchi Hiyo inachokiishi kwani naifahamu Vizuri sana Nchi ya Burundi kutokana na kuishi miji kazaa ukiwemo Bujumbura, kayanza, Muyinga, Rumonge, Nyanza Lac, Mabanda na mji wa Makanba kwani nikifika Burundi hujiona kuwa niko Tanzania kwakuwa nimekuwa maarufu sehemu izo kutokana kuwahi kuishi na ndugu na jamaa maeneo hayo.

Mbali na hilo Burundi ilijipatia uhuru wake kutoka kwa Uberigiji mwaka 1962 lakin toka uhuru huo taifa hilo limekuwa likikumbwa na machafuko ya mara kwa mara ikiwemo yale ya mwaka 1961, 1963, 1968, 1972, 1993, 1994, 1997 na haya ya sasa ya mwaka 2015

HISTORIA YA BURUNDI.

Burundi ambayo huko nyuma ilijulikana kama Urundi ni eneo linalopatikana katika Afrika mashaliki katika ukanda wa mashaliki ya Afrika ya kati na imepakana na DRC kwa upande wa magharibi, kusini imepakana na ziwa Tanganyika na upande wa kaskazini imepakana na Rwanda huku upande wa mashaliki imepakana na Tanzania.

Mji wake mkuu ni Bujumbura ambayo huko nyuma ulijulikana kama Usumbura wenyeji wa nchi hiyo ni kabila la Watwa (Batwa) ambao waliishi hapo toka miaka ya 300 BC na baadae kati ya miaka 110 AD na 340 AD walikuja jamii nyingine ya wabantu waliotoka kwenye misitu ya Kongo na Kameroni waliojulikana kama Wahutu (Hutu) ambao walitawanyika katika ukanda wote wa milima ya "Ruanda na Urundi" na walikuwa wawindaji na baadae wakaanza kujihusisha na shuguri za kilimo mnamo miaka ya 600 AD. Katikati ya miaka ya 900 AD jamii kubwa ya Nilotic kutoka kwenye kikundi cha jamii ya wafugaji ya Wahamatic iliyojulikana kama Watusi (Tusi) ilianza kuvamia ukanda wote wa nyanda za mashaliki ya Afrika ya kati kuanzia aridhi ya Kalamojog, Bunyoro na Buganda huko Uganda hali iliyopelekea kuzuka kwa vita za makabila dhidi ya kabila lenyeji na kabila vamizi kwa kuwa Watusi walikuwa na mifugo kuna mahali walishindwa vibaya sana na kukibia kama katika himaya ya Kalamoja lakin kuna mahali waliwashinda wenyeji na kuanzisha himaya mfano huko Nyankole na Bunyoro.

Wingi wa idadi ya wahamiaji wa jamii ya Watusi ilipelekea kuwafanya kutafuta aridhi na kujitanua ukanda wote wa kusini mwa Afrika mashaliki ya kati kitu kilichopelekea jamii hiyo ya Watusi kufika Rwanda na hatimaye miaka ya 987 AD kufika Tanganyika maeneo ya himaya ya chifu Rumanyika na baadae Burundi. Watusi walikuwa ni wafugaji wenye makundi makubwa ya ng'ombe ambao walikuwa nakitafuta makazi bora ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Kuanza kwa uvamizi wa wazungu mwanzoni mwa miaka ya 1800 kuliifanya Burundi kutawaliwa na Ujerumani ambapo Burundi, Rwanda na Tanganyika zote zilikuwa ni nchi moja iliojulikana kama Ujerumani ya Africa mashaliki (German east Africa) ambapo baadae Burundi na Rwanda alipewa uberigiji mara baada ya vita ya kwanza ya dunia kumalizika ndipo Urundi yani Burundi na Urwanda yani Rwanda ndipo zilipo pewa koloni lingine la uberigiji kwa kile kilichoitwa "Fidia ya kushindwa vita kwa ujerumani" kupitia mkataba wa Anglo-Belgium Treaty 1919 mara baada ya (mkataba wa Verseryas).

Ujio wa mbelgiji ndio chanzo cha kuibuka kwa matabaka baina ya makabila mkubwa mawili yani Wahutu na Watusi, hapa mbeligi alianza kuwatumia Watusi katika shuguli zake za kiutawala kama makalani, walimu,maafisa wa ngazi za chini na kuwapa fursa za kijamii tofauti na ilivyo kwa kabila la Wahutu waliowengi na hii ni kutokana na kabila la Wahutu walikuwa watu wakolofi, wabishi na wakali huku Watusi walikuwa watu wakimya, wapole na wastaalabu kitu kikichopelekea wazungu kuwapenda na kuwatumia katika shuguli za utawala jambo lililopelekea kuongezeka kwa chuki baina ya hayo makabila mawili yani Watusi na Wahutu kwani Watusi waliwanyanyapaa Wahutu kwa kiasi kikubwa na chuki hiyo iliongezewa chuki maradufu na wakoloni wa kizungu (Wabeligiji) kwakuwa karibu sehemu nyingi za utawala walipewa Watusi kama Askali wa usalama, Askali wa mageleza maafisa suluhu na sehemu nyigi za utawala.

Na ilipofika miaka ya 1949 wabeligiji waliona wa badili mfumo wa utawala na kuanzisha mfumo mpya ulioitwa "Tribe clasical system of administration" na hii ndio iliyo kuja kuchochea ukabila tunaouona ukiishi leo Burundi na Rwanda kwakuwa haya mataifa yanafanani kwa karibu kila kitu. Kwa Burundi uberigiji aliwapa mamlaka Watusi na kuwabagua Wahutu huku kwa Rwanda katika miaka ya 1950 mbeligiji alianza kuwapa kipaumbele Wahutu kutokana na msukumo wa wamissionari wa kikatoriki walioanza kuwatetea Wahutu kwa kuona wao ndio wanaonyanyaswa na kubaguriwa hivyo uberigiji aliona ni vyema kuwapa msukumo Wahutu kwakuwa kipindi hiko vuguvugu la Wahutu lilikuwa kubwa. Katika miaka ya 1950 ilionekana na kudhihirika ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu waliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.

Mwami Mutara Rudahigwa aliyejiita pia Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi. 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya Wahutu na Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani mkali kutoka kwa Watutsi walio amua kumuua mwaka 1959. Mtoto wake Mwami Kigeri V. alisimikwa kwenye kiti hicho. Hatua hii ilisababisha ghasia na vurugu nchini kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V. alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda. Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu. Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali hiyo nchini Rwanda. Hiyo ilizidisha hali ya mbeligiji kuamua kuwapa mamlaka Wahutu na kuwabagua Watusi.

Ikumbukwe kuwa katika jamii hizo mbili wahutu ndio waliokuwa watawala wa himaya ya Rwanda na Burundi kabla ya kuja mzungu (mkoloni) toka kuanzia miaka ya 400 AD lakini huko Rwanda katika miaka ya 720 AD Watusi waliwashinda wahutu katika mapigano makali yaliyojulikana kama "Vita ya Abahima" (Bahimma war) na kupelekea wao kuanzisha himaya ya utawala kwa Watusi huko Uruanda (Rwanda). Kwa Burundi pia wahutu ndio waliokuwa na himaya lakin awakupewa kipaumbele na mkoloni.

Kihistoria na jeograpia nchi hizi hufanana kalibu kila kitu. Katika Burundi kutokana kukomaa kwa ubaguzi wa kikabila mkoloni alichochea hali ya ubaguzi na chuki baina ya Wahutu na Watusi.

Ubeligiji ndipo miaka ya 1950 kulianza kuzuka vuguvugu la ukombozi barani Afrika hata hivyo Burundi nayo aikubaki nyuma. Mwaka 1956 ndipo mtoto wa mfalme Mwabusta V (Mwami Mwambusa) aliojulikana kama mwana mfalime Lous Lwagasore alipo unda chama cha ukombozi kilicho julikana kwa kiingeleza kama UNION PREPARATION FOR NATION (Unioñ le prépàrasio du ñational) UPRONA.

UKOMBOZI NA UHURU KWA BURUNDI.

Kama nilivyo eleza apo juu vuguvugu la ukombozi Burundi lilikwenda kwa misingi ya ukabila na utabaka.

Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi ya UM na chama mshindi kilikuwa UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemwoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na ukabila.

Mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urubdi uhuru kamili, lakini kila nchi pekee.

Baada ya uchaguzi wa 1965 mapigano yalitokea kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali kilichukua serikali.

Mwaka 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Michel Micombero aliyejitangaza kuwa rais na nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa

Mwaka 1956 kiliundwa chama cha UPRONA cha Watusi wenye misimamo ya wastani kilichoongozwa na Prince Lous Lwagasore ambaye yeye alijibainisha kupinga ubaguzi wa kikabila uliokuwa ukiishi Burundi na kutaka kuwepo na umoja wa kitaifa. Japo kuwa chama cha UPRONA kuwa cha kitusi lakini kilionekana kuwa na Wahutu wachache kilianza kukubalika na kuungwa mkono karibu na idadi kubwa ya warundi.

Mapema mwaka 13/10/1961 Princes Lous Lwagasore aliuwawa na kikaragosi wa kiberigiji mwenye asili ya kigiriki aliyejulikana kama Jean Kageorgis akishilikiana na viongozi wa chama kikichokuwa kinaungwa mkono na wabeligiji cha PDC (cristianity Democratic party) katika hotel ya Club du Lac Tanganyika mjini Bujumbura kutokana na yeye kuonekana kutaka kujenga umoja wa kitaifa na kuhatalisha maslahi ya wakoloni wa kibeligiji nchini Burundi. Mapema baadae hali ya vuguvugu ya ukombozi ilizidi hali iliyopelekea uberigiji kuamua kutoa uhuru kwa Burundi mwaka 1/7/1962. Huku chama cha UPRONA kikiongoza katika uchaguzi wa bunge wa mwanzoni na hatimaye mwaka 1966 Burundi ikawa Jamuhuri baada ya mapinduzi na Micheli Michombelo kuwa Rais.

Pamoja na uhuru machafuko yaliendele pamoja na mauaji ya baina ya makabila mawili ya watusi na wahutu na hiyo ndio imekuwa kama sifa kubwa na historia ya Burundi, inaipambanua nchi hiyo katika sura ya mgogoro wa kikabila Hakuna sifa tofauti yenye kuvuma ulimwenguni zaidi hiyo. Jina Burundi kimataifa, muktadha wa karibu ambao hujitokeza nimapigano ya wenyewe kwawenyewe, Wahutu na Watutsi.Mapigano ya Wahutu na Watutsi yalichukua nafasi kubwa tangu miaka ya 1960 na kuendelea nyakati zote mpaka mwafaka mkubwa uliopatikana mwaka 2000, chini ya msuluhishi, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,marehemu Nelson Mandela.

Mandela alichukua nafasi ya usuluhishi, baada ya kazi kubwa kuwa imeshafanywa na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati mwalimu Jurius Nyerere.

Nyerere alianza kazi ya usuluhishi wa Burundi mwaka 1995 ikiwa ni baada ya vifo vya marais wawili. Oktoba 1993, Melchior Ndadaye, mwenye asili ya Kihutu, aliyetoka kushinda Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, mwaka huo, alitawala kwa miezi minne tu, kabla ya kuuawa na wapiganaji wa Kitutsi. Baada ya Ndadaye aliyeongoza kupitia Chama cha Front for Democracy in Burundi (FRODEBU), mapema mwaka 1994, Cyprien Ntaryamira (Mhutu) alichaguliwa kabla ya mwaka huohuo, kuuawa Rwanda, wakati ndege aliyokuwa amepanda yeye na aliyekuwa Rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana, kutunguliwa na kuangushwa, ilipokuwa inakaribia kutua Uwanja wa Ndege wa Kigali.

Kifo cha Ntaryamira kilisababisha aliyekuwa Spika wa Bunge la Burundi, Sylvestre Ntibantunganya (Mhutu), achaguliwe kuwa rais kabla ya Rais wa vipindi vingi vya nchi hiyo, Pierre Buyoya, kumpindua.

Mwafaka uliopatikana mwaka 2000 chini ya Mandela ambaye aliwatumia vizuri waliokuwa marais wa Marekani na Afrika Kusini, Bill Clinton na Thabo Mbeki, ulisainiwa na aliyekuwa Rais wa Burundi, Buyoya na vikundi 13 kati ya 19 vya waasi. Mandela aliagiza vikundi vilivyokubali visaini kisha mwafaka ukatekelezwe bila kuhusisha wasusiaji ambao hata hivyo baadaye waliomba kuunganishwa kwenye uundaji wa Serikali ya Mpito. Buyoya wa Chama cha UPRONA, baada ya mwafaka aliongoza mpaka mwaka 2003 kabla ya Domitien Ndayizeye wa FRODEBU kuchaguliwa kuongoza serikali ya mpito, iliyokwenda mpaka mwaka 2005, Bunge la Burundi lilipomchagua Pierre Nkurunziza kuwa rais kwa kipindi cha miaka mitano.

Tangu Nkurunziza achukue madaraka, hali ya amani ilipatikana Burundi, shughuli za kiuchumi zilifanyika bila mashaka yoyote, huku Wahutu na Watutsi wakishirikiana kuijenga upya nchi yao ambayo wao wenyewe waliibomoa kwa sababu za chuki za kikabila. Uchaguzi Mkuu 2010 ulifanyika kwa amani japo vyama vya upinzani vililalamikia kuchezewarafu lakini hakuna mtu aliyerejea msituni.

Ila kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, Burundi imerejea kwenye machafuko. Mpaka sasa, zaidi ya watu 1,000 wanaripotia kupoteza maisha, huku tayari watu zaidi ya 250,000 wakiwa wameshaikimbia nchi yao. CNARED ni muungano wa vyama vya upinzani zaidi ya 20 nchini Burundi ambavyo vimeungana kuhakikisha matakwa ya Katiba ya Burundi yanaheshimiwa, vilevile mwafaka wa mwaka 2000 uliosimamiwa na hayati Mandela. Kwa pamoja, CNARED wanampinga Nkurunziza wakimtuhumu kusigina katiba na kukiuka kile kilichoafikiwa mwaka 2000 jijini Arusha.

Hivi karibuni, nilifanya mahojiano na Naibu Katibu Mtendaji wa CNARED, Nzeyimana Abdoul kuhusu masuala mbalimbali nchini mwake.Nzeyimama ambaye anaishi Ubelgiji, niliweza kupata mawasiliano yake kupitia maafisa wa umoja wa mataifa waliopo jijini Goma jimbo la Kivu kaskazini katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo nilipo izuru Goma siku kazaa hapo nyuma.

Akiwa uhamishoni baada ya kukimbia Burundi kutokana na machafuko ya kisiasa, anasema kuwa ripoti za wakimbizi nchini mwake zinaonesha kuwa zaidi ya watu 150,000 wamekimbilia Tanzania na wanaishi kwenye kambi tofauti za wakimbizi. “Watu zaidi 38,000 wamekimbilia Uganda na Rwanda kunawakimbizi zaidi ya 75,000, wakati huohuo, tayari watu 1,000 wameshauawa,” alisema Nzeyimana, katika mahojiano niliyofanya naye, nilipokuwa jijini Goma DRC katika ziara yangu inayoendelea ambapo sasa niko nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati katika jiji la Bangui napo nikijalibu kujionea madhala ya vita ya kidini kati kikundi cha Seleka na Antibalaka vilivyo sababisha mauaji ya kinyama kabisa na mda sio mrefu nitatoa makala juu ya hali niliyoiona huku Bangui, pia huko DRC na Rwanda.

Katika mazungumzo yangu na Nzeyimama anaonya kuwa mgogoro wa sasa wa Burundi usitafsiriwe kuwa ni wa kikabila kati ya Wahutu na Watutsi kama ambavyo ilivyozoeleka, badala yake uliopo sasa unatokana na siasa mbaya na uongozi mbaya wa Nkurunziza wa kung’ang’aniamadaraka.

“CNARED ni muungano wa vyama 23, vipo vya Wahutu na Watutsi, wote tumeungana kupinga vitendo vya Nkurunziza kukanyaga katiba na mwafaka wa Arusha. “Kwetu sisi Warundi, kutokana na historia za mapigano, tunaheshimu sana mwafaka wa Arusha, ni kama Biblia kwa Wakristo,” anasema Nzeyimana. Anaendelea: “Mimi ni Mhutu, kwa hiyo inatakiwa ifahamike kuwa mgogoro wa Burundi siyo wa kikabila, maana Serikali ipo mikononi mwa Wahutu lakini Wahutu haohao wanaongoza kuwakimbiza Wahutu wenzao.” Akifafanua kuhusu kirefu cha CNARED, Nzeyimana anasema kuwa ni muungano wa vyama vya upinzani vinavyopigania uheshimishwaji wa Mkataba wa
Arusha na Katiba.

Anasema kuwa Nkurunziza ameshindwa kuwatendea haki Warundi, kwani ukaidi wa
kung’ang’ania madaraka umesababisha kuwarejesha kwenye historia ya machafuko
ambayo walikuwa wameshaisahau. “Ukiachana na suala la wakimbizi na vifo, vilevile wananchi wakiishi kwa tabu kwenye kambi kwa kukosa hata faragha, wanaume na wanawake wakilala pamoja, mgogoro wa Burundi sasa hivi unahatarisha ustawi wa Afrika Mashariki, hivyo kuleta athari ya kidiplomasia. “Sasa hivi Nkurunziza anaishutumu Rwanda kuwa inachochea machafuko Burundi, hili ni jambo ambalo halipo sawa hata kidogo. Inatakiwa hata Watanzania waujue mgogoro vizuri kuwa una athari kubwa kwa Afrika Mashariki,” anasema Nzeyimana.

Akichambua athari zaidi za machafuko Burundi kiuchumi, Nzeyimana anasema kuwa wananchi sasa hivi hawafanyi shughuli zao za kiuchumi, kitu ambacho kinawaweka katika mazingira magumu ya kimaisha. “Sarafu ya Burundi, Franca, kabla
ya machafuko ilikuwa inabadilishwa kwa 1,650 dhidi ya dola moja ya Marekani lakini sasa hivi dola moja ya Marekani inabadilishwa kwa franca 2,400, hali ni mbaya,” anasema Nzeyimana.

Nzeyimana ambaye amepata kuwa Naibu Meya wa Jiji la Bujumbura, anasema kuwa sasa hivi tayari vikundi vitatu vya waasi vimeshajitokeza ambavyo vinapambana na Serikali ya Burundi. “Utaona ni ndani ya muda mfupi mno.Kuna Kundi linaitwa Forebu ambalo linaongozwa na Jenerali Godefroid Niyombare, huyu alikuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Burundi, vilevile Mkuu wa Majeshi. “Jenerali Niyombare alitofautiana na Nkurunziza alipomshauri asikanyage katiba na kujiongezea muhula mwingine wa uongozi. Walipotofautiana, alikwenda msituni kuanzisha kundi lake la uasi. Sasa hii ni hatari kubwa kwa nchi kwa sababu Jenerali Niyombare ni mtu ambaye anaheshimika sana jeshini na ana ushawishi mkubwa,” anasema Nzeyimana.

Anaongeza: “Mwishoni mwa mwaka jana, waasi wa Forebu walivamia ghala kuu la silaha za kijeshi Burundi na kupora silaha nyingi na katika mapigano makali
watu 100 waliripotiwa kuuawa. Hii ni hatari lakini Nkurunziza anaziba masikio. Unawezaje kugombana kirahisirahisi na mkuu wa majeshi ambaye pia ni mkuu wa usalama wa taifa?” Nzeyimana anataja vikundi vingine kuwa ni FNL cha Jenerali Aloys Nzabampema na RED-TABARA cha Jenerali Melchiade Biremba. “Nasisitiza, Burundi hakuna mgogoro wa kikabila, ni mgogoro wa madaraka. Tamaa za Nkurunziza zinasababisha mauaji ya watu wasio na hatia pamoja na usumbufu mkubwa kwa raia, anasema Nzeyimama. Anaongeza kuwa viongozi mbalimbali wa Kihutu wamekimbia nchi, wakiwemo marais wastaafu, kuonesha kuwa japo Rais ni Mhutu, hata Wahutu wenyewe wanapata wakati mgumu. Anawataja viongozi hao kuwa ni
Ntibantunganya, Pierre Ntanyohanyuma (alikuwa Spika wa Bunge), Gervais Rufyikiri
(Naibu Rais), Leonidas Hatungimana (Msemaji wa Rais) na Onesmo Naiwimana (Msemaji wa Chama cha Nkurunzia CNDD- FDD). Wengine ni Bernarol Busokozaza, Alice Nzomukunda, Marina Baramama na Fredric Bamvuginyumvira ambao wote walipata kuwa manaibu rais, vilevile Hussein Radjabu, aliyekuwa Kiongozi wa CNDD- FDD. Rais wa Awamu ya Tatu Tanzania, Benjamin Mkapa ndiye msuluhishi wa mgogoro wa
Burundi, Nzeyimana anaelezeaje imani hiyo? Anajibu: “Tuna imani kubwa na mzee Mkapa. Sisi CNARED tulikutana naye Ubelgiji Juni 10 na 11, mwaka huu, tutakutana tena Julai 10 Arusha. Anafanya kazi nzuri, tofauti na msuluhishi wa awali ambaye ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.”

Maoni yangu

Maoni yangu juu ya kile kinachoendelea Burundi ni mwiba na doa kwa jumuiya ya Afrika mashaliki kama Tanzania tunahaja ya kuchukua hatua za kidpromasia ili kunusulu taifa la Burundi kwa kuchukua hatua za kidpromasia na kuanzisha mazungumzo yenye mashaliti kwa kuliona lile linaloendela Burundi ni vita kubwa na haistaili kupuuzwa hata kidogo kama inavyo puuzwa sasa kuna haja ya kutafutwa ufumbuzi wa jambo hilo kwa ukinifu ili kunusuru maisha ya warundi wasio kuwa na hatia pamoja na kuzorota kwa amani. Ikumbukwe haistaili kuufanya mgogoro huu ni wa Burundi ni lazima tukubali kuwa si jambo la ndani ya Burundi tu.

Na mwisho japokuwa sio kwa umuhimu wake kuzorota kwa amani ya Burundi ni kuchochea uzorotaji kwa uchumi wa Tanzania na kupoteza ushawishi kwa Tanzania katika turufu yetu katika nchi za maziwa makuu na kupelekea kuongezeka kwa hali ya hatari ukanda wote wa maziwa makuu.

"Mungu bariki Afrika, Mungu baliki Warundi, Mungu ibariki Burundi".

Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu.

+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com
 
Back
Top Bottom