Makala ya Kijana wa Kitanzania

Jul 13, 2021
19
35
MAKALA YA KIJANA WA KITANZANIA


Sehemu ya kwanza

Mwandishi: Innocent Abisai

Kijana ni nani?

Kijana ni mtu ambaye umri wake unaanzia umri wa miaka 18 mpaka 45(Mujibu wa sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 na kufanyiwa mabadiliko mwaka 2007)

Taifa lolote asilimia zaidi 55% linategemea sana vijana ndio nguvu kazi ya kuleta maendeleo katika taifa na watu wake kwenye maisha ya kila siku. Tanzania pia inategemea sana Vijana wa kitanzania kuwa chachu ya maendeleo pamoja na mabadiliko kwa taifa

“Vijana wamekuwa chachu ya maendeleo kuanzia ngazi ya mtu mwenyewe, familia mpaka taifa kwa ujumla”

Vijana wengi wa kitanzania wanajishughulisha na kazi za aina mbalimbali inaweza kuwa kazi ya kujiajiri au kazi ya kuajiriwa ili kuweza kuingiza kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku

Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo vijana wake ambao wana vipaji na vipawa mbalimbali kama vile

1. Kuimba

2. Kuzungumza mbele ya watu

3. Mwalimu

4. Kucheza mpira

5. Mitindo na fasheni

6. Uandishi n.k

Lakini ni vijana wachache wanaweza kutumia vipawa na vipaji vyao ipasavyo kwa kuvitumia vipaji vyao(Kusudi la kuzaliwa kwao) ili kuendesha maisha yao, wapo vijana wengi sana mfano:

1. Mbwana Samatta

2. Flaviana Matata

3. Millard Ayo

4. Benjamin Fernandez

5. Barnaba

6. Masoud Kipanya n.k

Mimi na wewe ni vijana ambao tuna nafasi ya kufanikiwa kutimiza malengo yetu katika njia sahihi kwa kutumia vipaji na vipawa vyetu

MASWALI MUHIMU YA KUJIULIZA

~Je kijana wa kitanzania unayesoma makala hii unajua kipaji au talanta yako?

~ Je mpaka ulipofika unajitambua wewe ni nani?

~ Je, unajikubali wewe kama kijana wa kitanzania?

~ Je, una nidhamu binafsi kwenye maisha yako?

~ Je, ni mzalendo kwa taifa lako?

~ Je, ni muadilifu kwenye kile unachofanya?

~ Je, umethubutu na kuweka shauku kubwa kwenye malengo yako?

~ Je, kipi unajivunia umeifanyia Tanzania?
_____

Tukutane sehemu ya pili kwenye muendelezo wa makala hii......

Kauli mbiu yetu: “MAISHA NI KUTHUBUTU"

Imeandikwa na Innocent Abisai (Lolo Facts Founder)
 
Asante kwa makala nzuri ngoja na sisi vijana tujitafakari ili tuandikwe kwenye ubao kama ulivyo waandika vijana wenzetu.
@kasomi
 
Back
Top Bottom