Makala hii katika Tanzania Daima imenivutia mno

luhala

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
412
142
Katika gazeti la jana la Tanzania Daima kulikuwa na makala hii ya Nkwazi Mhango iliyonisisimua na kunivutia sana. Mimi niko mbali na Dsm na husoma makala kwa njia ya mtandao. Kwa faida ya wengi ambao hawakubahatika kulipata gazeti hili jana naweka makala hii ili nao waisome na ikibidi wachangie hoja.
SI uzushi wala uchochezi. Tanzania inaelekea pabaya tena sana.

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza' kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.


Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?


Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA?

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough'.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
 
Asante sana Luhala kwa kutuletea hii makala. Kwa hakika mwandishi ametusemea watanzania wengi na nampongeza kwa ujasiri wake huu. Laiti kama waandishi wote wangekuwa na ujasiri wa namna hii angalau nchi ingenusurika na kuangamizwa na manyang'au hawa wanaojiita CCM (Chama cha Majambazi). Yaani hali inasikitisha mno, makampuni ya kigeni yanavuna wasichopanda, wanatorosha kila wanachotaka kwa msaada wa majambazi waliojipenyeza kwenye chama tawala na serikalini, wakati Kenya na Uganda makampuni ya simu ndiyo yanayoongoza kwa ulipaji kodi Tanzania hakuna hata kampuni mojawapo iliyoweza kuwa angalau katika kundi la walipaji kodi ishirini bora! Eti Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel wanapitwa na makampuni ya ulinzikwa ulipaji kodi. Natamani 2015 ije kesho ili watanzania tutoe ghadhabu zetu.
 
Asante
sana Luhala kwa kutuletea hii makala. Kwa hakika mwandishi ametusemea
watanzania wengi na nampongeza kwa ujasiri wake huu. Laiti kama
waandishi wote wangekuwa na ujasiri wa namna hii angalau nchi
ingenusurika na kuangamizwa na manyang'au hawa wanaojiita CCM (Chama
cha Majambazi). Yaani hali inasikitisha mno, makampuni ya kigeni
yanavuna wasichopanda, wanatorosha kila wanachotaka kwa msaada wa
majambazi waliojipenyeza kwenye chama tawala na serikalini, wakati
Kenya na Uganda makampuni ya simu ndiyo yanayoongoza kwa ulipaji kodi
Tanzania hakuna hata kampuni mojawapo iliyoweza kuwa angalau katika
kundi la walipaji kodi ishirini bora! Eti Vodacom, Airtel, Tigo na
Zantel wanapitwa na makampuni ya ulinzikwa ulipaji kodi. Natamani 2015
ije kesho ili watanzania tutoe ghadhabu zetu.

ni kweli inasikitisha. mwandishi kafanya upembuzi yakinifu.
 
Naungana na mtazamo wa mwandishi kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu japo hatuna mkia wala macho ya kisogoni.
Pia natoa shukrani kwako mkuu kwa kutamani kushare nasi hata tusio fanikiwa kulipata gazeti au kuijua website yao.

Na nahisi ule wimbo wa amani amani ndio umetuharibu kisakorogia kimsingi tunajifanya tunaipenda amani bila kuijua.

Kwa hali ilivyo sasa na nikitazama watanzania wenzangu tena wengine wako na hali iliyo poteza matumaini na bado wanajiondoa ufahamu wa kutoiona hali halisi hua tu najikuta natetemeka kwa hofu ya picture ya Tanzania yetu ijayo.

Mataifa ya magharibi yanafikia hatua kututusi waziwazi kwa kumuita kiongozi mkuu wa inji yetu ni Muzungu worshiper kwa jinsi anavyo watukuza na sisi bado tumelala tu kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kwake na lichama lake mmmh...cjui ni muujiza gani utakao tuamsha kwa kweli.

Wakuu tusichoke kuipigania Tanzania yetu naamini machozi yetu si bure hakuna marefu yasio na ncha ....itafika hata baadi ya walio kwenye system wanaguswa na maumivu yetu labda hofu ndio inayo watesa lakini sikumoja watasimama kiume nakuungana na waTanzania wazalendo.
 
Asante sana Luhala kwa kutuletea hii makala. Kwa hakika mwandishi ametusemea watanzania wengi na nampongeza kwa ujasiri wake huu. Laiti kama waandishi wote wangekuwa na ujasiri wa namna hii angalau nchi ingenusurika na kuangamizwa na manyang'au hawa wanaojiita CCM (Chama cha Majambazi). Yaani hali inasikitisha mno, makampuni ya kigeni yanavuna wasichopanda, wanatorosha kila wanachotaka kwa msaada wa majambazi waliojipenyeza kwenye chama tawala na serikalini, wakati Kenya na Uganda makampuni ya simu ndiyo yanayoongoza kwa ulipaji kodi Tanzania hakuna hata kampuni mojawapo iliyoweza kuwa angalau katika kundi la walipaji kodi ishirini bora! Eti Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel wanapitwa na makampuni ya ulinzikwa ulipaji kodi. Natamani 2015 ije kesho ili watanzania tutoe ghadhabu zetu.

Haitaji tochi kuyaona haya welldone mwandishi umetumia kalamu yako kazi kwetu na kuakikisha hizi habari zinawafikia wananchi wa vijijini.nilishasema kuwa uwepo wa CCM madarakani kunatokana na watu vijijini kutokujua uozo wa serikali ya ccm.kungekuwa na uelimishaji mkubwa kama unaofanyika wakati wa chaguzi ndogo
 
nchi imekauwa kama stoo ya nje isiyo na mlango......kila mgeni anakuja na kuchukua anachoweza kubeba na kutokomea kunakojulikana.......
 
Ni kweli nchi yetu imekuwa pango la wanyanganyi huku walinzi wakimsaidia mwizi kuiba. Inauma sana inatupasa tuikatae hali hii kwa kumaanisha tuwaondoe watu hawa madarakani.
 
mimi nalia tuuuuu jamani

UWiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....... Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii............... Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...!!!!!
Mwandishi umenikuna haswa,
Kalamu hakika umeitumia
Maovu na watawala ni sawa na macho na machozi yataturudia puani hakika nakuambia...
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.........
Ahaa ! ndo maana kuna nafasi/gape kubwa kati ya walionacho na wasionacho,
Ahaa ! ndo maana watoto wa vigogo hawana habari na maiisha ya wananchi wa kawaida
Ahaa !ndo maana ,viongozi kujilimbikizia mali wanaona ni haki yao
Ahaa ! ndo maana nikienda kwenye shule za kata kamwe huwezi kumkuta motto wa mkuu wa wilaya acha wa waziri.
Ahaa ! ndo maana kudhulumu ni jambo rahisi kama ilivyo sawa na kutoa uhai wa mtu ili mambo yako yasiwekwe wazi
Ahaa ! ndo maana wanao wafichua walafi wa mali ya umma hawaishi.
Ahaa ! ndo maana wasema kweli kama CHADEMA wanapopambana na ulafi huu huwa wanapigwa vita kwa nguvu zote.
Ahaa ! kumbe kuna haja ya kupeleka jumbe kama hizi kwa wanyonge na wasiyo na uwezo wa kuzipata.
Ahaa ! Kumbe ndo maana huwezi kumkuta motto wa kiongozi yeyote hana ajira.
Ahaa !kumbe ndo maana CCM WANACHUKIWA ,TENE KWA KASI YA AJABU
Ahaa! Kumbe ndo maana utawala wa haki umepotea.
KUMBEEE...AHAAA....TUMEKUELEWA MWANDISHI TENA SANA...ENDELEAAAAAAAAAA.
 
Mimi sitaki presha tena afadhali nitafute hata novel nisome maana kila unapogundua kuna ufisadi umefanyika ukifuatilia angalau uone maamuzi magumu yafanyike ili kukomesha watu wanabakia chekacheka tu..., ngoja nkachukue gazeti ya udaku nisome..
 
Ubinafsi umetamalaki miongoni mwetu.. sijui watoto wetu na wajukuu tutawarithisha nini

ila bado tuna miaka isiyozidi kumi ya kutawaliwa kama ngombe.. after that waombe mungu wasiwe hai kwani tutahakikisha wanalipa yote wanayoyatenda sasa
 
Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Mkuu hii issue iliniuma sana.. Yaani ndege ya kijeshi imekuja nchini na kutua.. ikaondoka na nyara za nchi na watu waliofanikisha hayo wako mtaani..! Yule Mpakistani alipewa dhamana na ametoroka.. Kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana lakini nikashangaa akapewa dhamana ili atoroke..! Na wote walio hucika bado wanapiga kazi kama kawaida..! Hakuna hata aibu..! Damn these people..!
 
Makala hii ni ya kweli, na hakika inavutia.
Mwandishi amejiatahidi kuwasilisha hoja zake katika mtiririko mzuri, lakini ametuacha tukining'inia kwani hajatuambia solution ni nini? Yaan mwananchi achukue hatua gani? kuilinda nchi yake na rasilimali zake kwa maslahi ya sasa ya UMMA na vizazi vijavyo.

Najua wengi watasema Ballot Box, lakini kwa kiwango hiki cha uchakachuaji wa matokeo na ugawanaji wa vyeo kwa maslahi ya kujuana bado hilo haliwezekani katika kiwango kinachokusudiwa. Je ni sahihi tukiendelea kulalamika bila kuchukua hatua? Ifike mahali, tuseme SASA BASI
 
Mkuu hii issue iliniuma sana.. Yaani ndege ya kijeshi imekuja nchini na kutua.. ikaondoka na nyara za nchi na watu waliofanikisha hayo wako mtaani..! Yule Mpakistani alipewa dhamana na ametoroka.. Kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana lakini nikashangaa akapewa dhamana ili atoroke..! Na wote walio hucika bado wanapiga kazi kama kawaida..! Hakuna hata aibu..! Damn these people..!

Dah! ni kweli inauma sana watu wachache wamejimilikisha nchi na rasilimali zote kuwa zao.Jamani tuamke wakati umefika wa kuwakataa hao na watoto wao wanaopenyezwa madarakani kila kukicha!!! shame on you!!!!
 
Nimesoma hii makala machozi yakanitoka....!
Ila nawahakikishia hayo ni 0.1% ya mambo yanayofanywa na CCM.

Naomba niwajuze..mimi nimfanyakazi hapa Tanzaniteone Mining Ltd.
Toka nimekuwa madini nyetu yanapelekwa nje kwa nia ya transfer prices.. yanaenda Dubai, South africa, Dubai, Bermuda...nk.

Imagine TRA wamelita Tanzanite one fro 2011 zaidi ya 800,000 eti hiyo ni VAT refund..inawezekanaje kweli sisi tukawlipa wawezeka kwa mali zetu wanazopeprusha kwao..
Wanakuja watu wa TMA wanapewa vumbi la Tanzanite wanafunga macho wanaruhusu Tanzanite inapelekwa nje...

inauma mno kuona tunavyodidimizwa kwenye dimbi la umaskina na viongozi wetu wa Tanzania.......
 
Back
Top Bottom