Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

Hahahhahaa! Mbona huna jipya…avoid repetition! Kiburi cha uzima kinakusumbua, while hujui one second ahead utakuwa kwenye hali gani!! Utanyooka tu utakapoanza kuvuna matunda ya mdomo wako! kuhusu wanangu...nimeshawaandalia kabla hata ya kuwapata! wewe fedha zako kazana kuzipeleka kwenye madanguro na vilabu vya gongo...mavuna yapo. napenda sana andiko lisemalo 'kila mtu atavuna alichopanda' yan sio hadi ufe..hapahapa duniani! mwanaume mzima kazi kushadadia umbea, na wanawake tufanyaje sasa! aibu zako!

Ndo Ukristo huo?? Hizo lugha unazotumia??
 
Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Takwimu imezitoa wapi za waumini 70000? halafu kumbuka wanavyokuwa wengi na kuwahudumia ni gharama, yote tisa, Hayo hayahusiani na matatizo tuliyonayo watz! Let Gwajima alone!!!
 
Last edited by a moderator:
hao maaskofu wengine walipewa uaskofu na nani? si na binadamu!? tena kwa taratibu zilizowekwa na binadamu. yaan kulikuwa na wa kwanza aliyeanzisha hiyo kitu! Mungu hajawahi kushuka akampa mtu uaskofu, ni taratibu za duniani. au kwa kuwa unakosali taratibu zilianzishwa na wazungu zamani kabla hujazaliwa ndo unaona big deal!! halafu pia, wewe huko kwa hao wanaolawiti vitoto vinavyotumikia kanisani unakosali...hutoagi sadaka? so unaliwa? maana kama kutoa sadaka kila muumini wa popote hutoa sadaka anaposali, lakini walokole kwa kuwa tunasali makanisa ambayo viongozi wake wa juu ni wa-TZ wenzetu ndo mnaona tunaliwa? nyie kwa kuwa waanzilishi ni wazungu tena msiowajua ndo hamliwi?? kuna nini kwenye kichwa chako? ni ubongo kweli??

Nakwambia wewe hujitambui. Hata arguments zako unaona kabisa hujitambui wewe ni nani. Umekanyagwa na Ulokole mpaka hujielewi! Hujui ukatoliki historia yake ndio maana hujitambui! Kama unaamini kuwa gwajima una UKIMWI atakuponya virus wayeyuke, hakika nakwambia hujitambui! Kama unaamini kwa kuja na kopo kanisani Gwajima ataliombea liwe Scania, hakika hujitambui
 
Sasa mi sijui hili lakihusu nini? Nashauri ufuate mambo yako! Achana na ya watumishi fake!

UOTE=MCHUNGUZI HURU;12379448]Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
Ukifahamu kama kuna kuingiza ujue kuna na kutoa vile vile. Mimi niko kwenye kamati ya kanisa lililoko mjini, makusanyo ya sadaka ni kidogo sana ukilinganisha na matumizi - mishahara, umeme, ulinzi, vifaa vya ibada mara si mara moja matumizi ya kawaida kugharamiwa na michango ya maendeleo kama harambee za ujenzi.

Mleta mada vile vile ukumbuke wale wanaomzunguka Gwajima na suti zao nao wana familia zao zinazohitaji kuhudumiwa vizuri na hizo hizo sadaka

Mkuu hakuna uhalisia wowote hapo, kukusanya watu sabini siyo kazi ndogo, angalia uwanja wa taifa baada ya m,echi kuisha hali inavyokua barabarani wakati wale ni 60,000 au chini yake.
 
Sijawahi kuona kanisa linalochukua idadi kubwa ya waumini inayofikia elfu ishirini hapa nchini achilia mbali elfu Sabin. Labda kanisa la TB Joshua huko Nigeria
 
Sijawahi kuona kanisa linalochukua idadi kubwa ya waumini inayofikia elfu ishirini hapa nchini achilia mbali elfu Sabin. Labda kanisa la TB Joshua huko Nigeria

Umenena vyema wewe hajawahi bali sisi tumewahi.Isitoshe yawezekana unaishi kijijini au uwa hautembei sehemu mbali mbali.
 
Msitake kudanganya watu, idadi ya watu elfu 70 sio mchezo. tazama tuu uwanja wa taifa wakitoka uwanjani barabara zote zinajaa, hakuna nafasi. na hao ni 60,000. ije kuwa hao wawili hapo kwa gwajima.? yaani kama wengi sana ni 20,000 sio zaidi. na data zipo sahihi kabisa.
 
Mtoa mada jaribu kutuletea zinazotumika baa,kasino,gesti ,night club na sehemu kama hizo ili watu waumie wamrudie Mungu.Wewe mtu katoa sadaka kanisani wala hajalazimishwa wewe inakuhusu nn.Kwanza watoaji wenyewe Wakristo wanajua siri ya kumtolea Mungu.Uliwaona wanaomtolea Mungu wamefilisika?Au lengo lako hasa nn?Mbona Ibrahim alimtoa mwanae sembuse pesa.

Ni vema kumtolea MUNGU na sio wachungaji feki wanaojitajirisha kimwili bila ya kibali cha MUNGU. Wanaojiita maaskofu wengine sio askofu ni wafuasi wa shetani ila wamevaa ngozi ya kondoo. Mtu wa MUNGU hana matamshi machafu, na hana sifa chafu. Eti unasema ni kabila moja na wamesoma wote hivyo unataka wasitembeleane na wachukiane au sio? Tunashauriwa kujenga chuki au upendo?.
 
Watu wanaacha kupga mahesabu ya TRA jinsi yanavoliwa na maCCM mnakuja na vijihesabu vya kataasis ambako hata hakatugusi wengine, acheni majungu nyiny, lete hesabu zenye maslahi mapana ya nchi bwana mnaboa sana

Huyu ametoa mtizamo wake kuhusu chanzo cha mapato ya Gwajima, kuna conspiracy theory nyingi kuhusu huyu jamaa amepata wapi hela, mimi sioni kosa hapo, wewe nawe hukatazwi kuja kutuelimisha kuhusu hayo mambo ya TRA
 
Msitake kudanganya watu, idadi ya watu elfu 70 sio mchezo. tazama tuu uwanja wa taifa wakitoka uwanjani barabara zote zinajaa, hakuna nafasi. na hao ni 60,000. ije kuwa hao wawili hapo kwa gwajima.? yaani kama wengi sana ni 20,000 sio zaidi. na data zipo sahihi kabisa.
Hata 20000 bado ni hypothetical....

Pale kwa Gwajima wakizidi sana ni watu 2000..
 
mmmm wakubwa.tumeona mapapa yanachota mabilon ya esrow hela za wananchi wameshindwaa kuwahoji nchi hii.wako wahuni wameficha uswisi mabilion hawahojiwi
 
Yaani hana hospitali , shule, kituo ca yatima nk! Hela yake ni ya Kupiga tu maisha
 
Back
Top Bottom