Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

lugha gani ya ajabu niliyotumia!! nilivyom-adress...ndivyo alivyo! mtu ambaye masaa 24 yuko busy kufatilia habari za wengine na kuanza kuhukumu bila prove..anaitwaje? kama sio mmbea!
Ndo Ukristo huo?? Hizo lugha unazotumia??
 
Ohooooo! Haaaa! Nicheke bint wa Yesu! Haya mipovu yote hiyo ya nini?? mara ukimwi..nini sasa! unautaka? kwa njia zako hizo..utaupata tu!…halafu kama umechanganyikiwa hivi? Nimewagusa pabaya eeh?? Kwani uongo? Sema, hiyo kashfa haipo? Eti sijui historia ya katoliki…itanisaidia nini? maana kama ni kwenda mbinguni njia ni Yesu wala si dhehebu lolote! Aibu zako unayeabudu dhehebu
Nakwambia wewe hujitambui. Hata arguments zako unaona kabisa hujitambui wewe ni nani. Umekanyagwa na Ulokole mpaka hujielewi! Hujui ukatoliki historia yake ndio maana hujitambui! Kama unaamini kuwa gwajima una UKIMWI atakuponya virus wayeyuke, hakika nakwambia hujitambui! Kama unaamini kwa kuja na kopo kanisani Gwajima ataliombea liwe Scania, hakika hujitambui
 
Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Wajinga na wafuasi wa kibwetele
ndo waliwao.
 
Last edited by a moderator:
Kodi yake kwa mwaka huyu kule TRA ni kiasi gani? Au kasamehewa hastahili kulipa kodi? Na yule mjenzi wa Uwanja wa ndege Chato naye kishalipwa 341 billion na Serikali kishalipa kodi TRA au yatakuwa yale yale ya Lugumi ya kukwepa kodi?

Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Unapoyasema ya Gwajima, anza kwanza na ya unakoswali wewe mwenyewe. Haifai kumsema mtumishi wa Mungu wakati tunajua kuwa yupo pale kwa wito wake. Mbona tunaona wengine wakipewa misimbazi mkononi bila kuambiwa ni kiasi gani alipewa??
Kama vip nawe kaanze kanisa lako upewe ka huyo. Hakuna aliyesema kuwa alienda kumwomba ampe maujanja akamfukuza. Kama waidhani ni biashara laini kaanze nawe kanisa lako.
Waacheni watumishi wa Mungu.
 
Maandiko ya Neno la Mungu yanamruhusu mtumishi kuishi kwa kuitegemea madhabahu.
Nilichokuwa natamani ni kuona na yeye akirudisha kwa jamii hapo Huduma Fulani kama sadaka yake kwa Mungu.
T.B Joshua wa Nigeria ananta hivyo kielimu, afya,wakimbizi etc.
 
Back
Top Bottom