Makada CCM wakata rufaa ubunge wa Lema

Makada CCM wakata rufaa ubunge wa Lema

Waomba hukumu ya Mahakama ya Rufaa ipitiwe upya

Makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopinga ubunge wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na kufanikiwa kumvua ubunge kabla ya Mahakama ya Rufaa kumrejesha wadhifa wake, wamewasilisha maombi ya kutaka hukumu ya mahakama hiyo ipitiwe upya.

Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama, makada hao waliwasilisha maombi yao Februari 13, mwaka huu chini ya hati ya dharura wakitaka yasikilizwe haraka.

Desemba 21, mwaka jana Mahakama ya Rufaa ilimrejesha tena Lema bungeni baada ya kukubali rufaa yake dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge wake.

Makada hao waliolalamikia ushindi wa Lema wakiwa ni wapigakura wa Jimbo la Arusha Mjini, wanadai kuwa na sababu sita za kutaka mahakama hiyo ipitie uamuzi wake kwa madai kuwa kuna maeneo ambayo hayakuamuliwa vizuri. Jana NIPASHE ilizungumza na Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, ambaye alithibitisha kuwa na taarifa za maombi hayo na kuahidi kutoa ufafanuzi baadaye.

Naye wakili wa wanachama wa CCM, Alute Mughway, jana alithibitisha kuwa wateja wake wamewasilisha maombi hayo Mahakama ya Rufaa.

Wanachama hao wa CCM, ambao ni Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, walifungua kesi dhidi ya Lema katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake, Lema alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Buriani.

Kufuatia kesi hiyo, Lema alivuliwa ubunge na mahakama hiyo, Aprili 5, mwaka huu, katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo. Jaji Rwakibarila aliisikiliza kesi hiyo baada ya Jaji Aloyce Mujulizi aliyekuwa amepangiwa kuisikiliza kesi hiyo kujitoa kufuatia ombi la Lema kuwa hakuwa na imani naye.

Hata hivyo, baadaye mwishoni mwa mwaka jana, Lema kupitia mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu, alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyomvua ubunge wake.

Hukumu ya kumrejeshea ubunge Lema ilitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Nathalia Kimaro. Wengine ni Salum Massati na Bernard Luanda.

Eti ndiyo mipango yamaendeleo inayopangwa na viongozi wa nchi hii wakifuata maagizo ya Usalama!!
Wanapoteza muda kwa upuuzi mambo yamaana yanawashinda nchi inayumba sasa!....
 
KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA:Makada hao watatu hawakati rufaa. Hii ni kwakuwa hakuna rufaa nyingine yoyote kisheria toka katika hukumu ya Mahakama ya Rufani. Wanachofanya makada hao ni kuomba marejeo(Review) ambayo kimsingi yatafanywa na Mahakama hiyo hiyo ya Rufani.

Ninachokiona,makada hao wanalenga zaidi kulegezwa kwa gharama za kesi walizoamriwa kuzilipa kwa Lema (na Mawakili wake).
 
Waomba hukumu ya Mahakama ya Rufaa ipitiwe upya

Makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopinga ubunge wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na kufanikiwa kumvua ubunge kabla ya Mahakama ya Rufaa kumrejesha wadhifa wake, wamewasilisha maombi ya kutaka hukumu ya mahakama hiyo ipitiwe upya.

Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama, makada hao waliwasilisha maombi yao Februari 13, mwaka huu chini ya hati ya dharura wakitaka yasikilizwe haraka.

Desemba 21, mwaka jana Mahakama ya Rufaa ilimrejesha tena Lema bungeni baada ya kukubali rufaa yake dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge wake.

Makada hao waliolalamikia ushindi wa Lema wakiwa ni wapigakura wa Jimbo la Arusha Mjini, wanadai kuwa na sababu sita za kutaka mahakama hiyo ipitie uamuzi wake kwa madai kuwa kuna maeneo ambayo hayakuamuliwa vizuri. Jana NIPASHE ilizungumza na Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, ambaye alithibitisha kuwa na taarifa za maombi hayo na kuahidi kutoa ufafanuzi baadaye.

Naye wakili wa wanachama wa CCM, Alute Mughway, jana alithibitisha kuwa wateja wake wamewasilisha maombi hayo Mahakama ya Rufaa.

Wanachama hao wa CCM, ambao ni Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, walifungua kesi dhidi ya Lema katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake, Lema alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Buriani.

Kufuatia kesi hiyo, Lema alivuliwa ubunge na mahakama hiyo, Aprili 5, mwaka huu, katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo. Jaji Rwakibarila aliisikiliza kesi hiyo baada ya Jaji Aloyce Mujulizi aliyekuwa amepangiwa kuisikiliza kesi hiyo kujitoa kufuatia ombi la Lema kuwa hakuwa na imani naye.

Hata hivyo, baadaye mwishoni mwa mwaka jana, Lema kupitia mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu, alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyomvua ubunge wake.

Hukumu ya kumrejeshea ubunge Lema ilitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Nathalia Kimaro. Wengine ni Salum Massati na Bernard Luanda.
Wakuu hapo hakuna cha walalamikaji ni CCM inatafuta jinsi ya kutoka, lakini inabidi walipe gharama za kesi!!! Wanatafuta jinsi ya kupoteza hukumu ya haki ili wapate Jdg wa kupindisha sheria kama Lwakibalila ili wasilipe gharama na kumuweka Mhse Lema under preasure, ila wajue huyo Jdg sasa hivi miguu haitembei!!!!

hawa watu ni wapuuzi sasa, hawana kazi za kufanya hivi

Nadhani tatizo liko kwenye malipo ambayo wanatakiwa walipe kama gharama za kesi.. Hii inawaumiza na haswa baada ya kuona ccm haina mpango wa kuwasaidia kulipa.. So wana-buy time hawa.. Salama yao kudedi..
 
hao hawana hela ya kumlipa lema so wanapiga danadana si unajua mahesabu ya time value of money?
 
Kwa sisi tunaoamini kwenye miujiza, ninaamini, unawezekana ukafanyika muujiza CCM wakaweza wakabahatisha kusimamisha mgombea na wakabahatisha kusinda jimbo la Ohi, US but si Arusha! Wasahau! o
 
wanasheria embu tupeni mwanga kuhusu hii rufaa? kisheria inaweza kuwa na merit kwa mrufani? au mjibu rufaa?
 
Dawa ya wakuda wape muda.........waacheni waruke sarakasi wakimaliza fidia ndiyo mpango mzima.
 
Hukumu iliagiza kuwa mtu asiyehusika haruhusiwi kukata rufaa. Anayetakiwa kukata rufaa ni Batilda sio hao wasiokuwa na kazi za kufanya. Maoni yangu Mahakama iwape sharti kwamba walipe kwanza ile fedha wanayotakiwa kumlipa Lema na gharama za kesi kwanza.

mkuu hii ni kesi malaya mtu yeyote anaweza kata rufaa ndani ya sisiem,aliyetukanwa anakula bata kenyaaa.....
nitaishangaa mahakama kama hii kesi itarudi kusikilizwa tena Tz haiishi vioja
 
Sasa hivi sio jimbo la arusha tu, hata jimbo la chalinze likiwa wazi maccm chaliiiiiiiii

ImageUploadedByJamiiForums1361989882.015019.jpg Yaan hata Chalinze lazima Chaliii chezea BABU PADRI WA KIFREEMASON
 
watengeneze kadi za mchango wapeleke LUMUMBA!!!!!!!!!! kamata wezi meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen
 
nasubiri mkuu,funguka mkuu.

Tz tunafuata Common Law Legal system, ni mwanzo tu huo,sisi ngazi ya chini kabisa ya mahakama ni mahakama ya Mwanzo,Wilaya,mahakama ya hakimu mkazi au mkoa,mahakama Kuu na Mahakama ya rufaa ambayo ndio ya mwisho kwa ngazi ya nchi ambayo maamuzi yake hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote isipokuwa kwa mtu ambaye hajaridhika na maamuzi kuiomba mahakama hiyo kuyapitia maamuzi hayo ambayo kuyatangua lazma ikae full bench(majaji 7) chini ya uenyekiti wa jaji mkuu ili kutangua maamuzi ya awali. Au waende mahakama ya Afrika Mashariki au Afrika japo hatua zake ni mchakato mrefu sana kwenda huko na ukizingatia hawa vilaza wa Magamba wanaoendeshwa na hisia za kisiasa zaidi so ni wapofu ,sijui ngoja tuwaone
 
Back
Top Bottom