Makada CCM wakata rufaa ubunge wa Lema

Makada CCM wakata rufaa ubunge wa Lema

environmental

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Posts
1,054
Reaction score
137
Waomba hukumu ya Mahakama ya Rufaa ipitiwe upya

Makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopinga ubunge wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na kufanikiwa kumvua ubunge kabla ya Mahakama ya Rufaa kumrejesha wadhifa wake, wamewasilisha maombi ya kutaka hukumu ya mahakama hiyo ipitiwe upya.

Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama, makada hao waliwasilisha maombi yao Februari 13, mwaka huu chini ya hati ya dharura wakitaka yasikilizwe haraka.

Desemba 21, mwaka jana Mahakama ya Rufaa ilimrejesha tena Lema bungeni baada ya kukubali rufaa yake dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge wake.

Makada hao waliolalamikia ushindi wa Lema wakiwa ni wapigakura wa Jimbo la Arusha Mjini, wanadai kuwa na sababu sita za kutaka mahakama hiyo ipitie uamuzi wake kwa madai kuwa kuna maeneo ambayo hayakuamuliwa vizuri. Jana NIPASHE ilizungumza na Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, ambaye alithibitisha kuwa na taarifa za maombi hayo na kuahidi kutoa ufafanuzi baadaye.

Naye wakili wa wanachama wa CCM, Alute Mughway, jana alithibitisha kuwa wateja wake wamewasilisha maombi hayo Mahakama ya Rufaa.

Wanachama hao wa CCM, ambao ni Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, walifungua kesi dhidi ya Lema katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake, Lema alikuwa akitumia lugha za matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Buriani.

Kufuatia kesi hiyo, Lema alivuliwa ubunge na mahakama hiyo, Aprili 5, mwaka huu, katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo. Jaji Rwakibarila aliisikiliza kesi hiyo baada ya Jaji Aloyce Mujulizi aliyekuwa amepangiwa kuisikiliza kesi hiyo kujitoa kufuatia ombi la Lema kuwa hakuwa na imani naye.

Hata hivyo, baadaye mwishoni mwa mwaka jana, Lema kupitia mawakili wake, Kimomogoro na Tundu Lissu, alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyomvua ubunge wake.

Hukumu ya kumrejeshea ubunge Lema ilitolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Nathalia Kimaro. Wengine ni Salum Massati na Bernard Luanda.
 
Ni baada ya CCM kuwaruka katika kumlipa fidia Lema!
 
hivi wanachowaza wanafikiri kitafanikiwa??hata hiyo kesi iongozwe the hague na ocampo arudi kama mwendesha mashata ubunge wa lema hauvuki ng'o!kwani hawa majamaa hawana majimbo mengine ya kukatia rufaa?
 
Anayejua sheria naomba anijuze. Mtu aweza kukata rufaa hadi lini? na Mahakama ya Mwisho TZ ni ipi?
 
------- hawa,wanatupotea muda na kuacha kufikiria mambo mengine.
 
hawana hela ya kulipa hao.... wanarukaruka tuu.. EL aliwapa kichwa sasa awasaidie tuu kulipa..
 
Batilda mwenyewe hana habari na kinachoendelea. Poleni sana.
 
Hawa jamaa wanaotaka kukata rufaa inatakiwa wafungwe na baada ya kifungo wachapwe viboko kumi na viwili siku wakitoka wakawaadisie wake zao na mabwana zao na bila kusahau kumlipa fidia Lema!
 
hawa watu ni wapuuzi sasa, hawana kazi za kufanya hivi
 
Waache kujizungusha waande lumumba wawambie waliowatuma kwamba Lema ni ngoma nzito
 
Wanakata rufaa katika mahakama ya rufaa, kwani hukumu ilitolewa mahakama gani jamani, mmh hapa wajuzi wa sheria wanaweza kutoa ufafanuzi zaidi. Hiyo kesi itasikilizwa na Jaji wa mahakama gani, napata utata mkubwa hapa.

Msaada please ipi mahakama ya mwisho kiuamuzi hapa kwetu Tz.
 
Mahakama ya rufani si ndo ya mwisho? Sasa rufaa wamekata kwa nani tena?
 
na hawa wanao kata rufaa kwa kesi ya lema sasa, ni lazima mahama ipime akili zao!
 
Anaejua jumla ya kiasi wanachotakiwa kulipa anijuze wakuu,ni milion ngapi na kulingana na agizo la mahakama deadline ni lini?
 
Wanakata rufaa katika mahakama ya rufaa, kwani hukumu ilitolewa mahakama gani jamani, mmh hapa wajuzi wa sheria wanaweza kutoa ufafanuzi zaidi. Hiyo kesi itasikilizwa na Jaji wa mahakama gani, napata utata mkubwa hapa.

Msaada please ipi mahakama ya mwisho kiuamuzi hapa kwetu Tz.

Wanataka ifanyoke review ya hukumu, nadhani kama ni review itakuwa chini ya majaji watano badala ya watatu.
 
Hukumu iliagiza kuwa mtu asiyehusika haruhusiwi kukata rufaa. Anayetakiwa kukata rufaa ni Batilda sio hao wasiokuwa na kazi za kufanya. Maoni yangu Mahakama iwape sharti kwamba walipe kwanza ile fedha wanayotakiwa kumlipa Lema na gharama za kesi kwanza.
 
ili iweje tena? waambieni wanakera! AMIN AMIN NINAWAAMBIA pale Arusha lema kajikamilisha kwenye nyoyo za watu sana. Mtu yeyote anayempinga inambidi amuulize Munguwake sana maana kama ni Mungu mumba mbingu na Nchi, ndie aliempa kijana huyu karama ya kutamka na kua mbele ya raia anaewaongoza!
 
Kuna uzi ulibandikwa humu siku chache mara baada ya rufaa ile iliomrudishia Ubunge Godbless Lema kwamba hawa jamaa matumbo joto cause wanatakiwa kulipa fidia ya gharama zote za kesi, mmoja wapo inasemekana alikimbilia Singida kwa Sangoma ili amsaidie na swaga lile liliendelea kua Bi Happiness ndoa yake ilikua hatarini cause mumewe hakua radhi kuona nyumba yao inapigwa mnada hivi hvi, mwenye ukaribu na hawa watu please!

Nahisi magamba wanafurahi zaidi kumwona Lema yupo Bungeni kuliko akiwa mtaani, madhara aliyoyasababisha akiwa Honey Moon ni makubwa zaidi kuliko anapokua Bungeni, i think, Lumumba wanaweza wasitoe pesa za ku-finance rufaa hii.
 
Back
Top Bottom