Makaburu na utawala wa CCM kuna tofauti gani?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Makaburu wa South Africa na ccm kuna tofauti gani katika kuongoza nchi? Kwanini tuliwasaidia south africa wapate uhuru ndani ya uhuru? Tukumbuke South Africa haikupata uhuru 1994, bali mwaka 94 ulikua ni uhuru dhidi ya wananchi wake wanaokandamiza wananchi wenzao. Ubaguzi huo ulijulikana kama ubaguzi wa rangi.

Wale wote waliokua wanafaidika na utawala ule wa kibaguzi hawakutambua ubawa wa utawala ule maana wanakula na kushiba. Hata wabaguzi yaan watu weupe walipata wafuasi toka kwa watu weusi wale wanaowafaidisha katika utawala wao.

Hata katika utawala wa ccm kuna watu wanafurahia mambo yanayoendelea bila kuona athari zake zilizojaa ubaguzi wa vyama. Ubaguzi ni ubaguzi tu hata uwe ni ubaguzi wa makabila. Kwa wale ambao hawaoni ubaguzi wa vyama hebu nikumbusheni haya mambo kadhaa hayapo? Ili niondoe dhana ya ubaguz wa vyama vya siasa katika utawala wa ccm.
Tukumbuke ubaguzi ni ubaguzi hata uwe ubaguzi umri.

Ni kiongozi gani wa wilaya au mkoa ambaye sio mwana ccm? Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi . Mtaniambia hao ni wawakilishi wa rais wanapaswa kuwa ccm. Kwann tuwe na vyama vingi lakn tukawa na mfumo wa utawala wa chama kimoja?? Kwann tusivunje mifumo ya chama kimoja iliyokuwepo kabla ya vyama vingi . Je huo sio ubaguz wa vyama katika nchi? Huu ni ubaguzi wa kuongoza taifa.

Ni yupi mkuu wa bodi ambaye sio kibaraka wa ccm?

Wakurugenzi waliotakiwa kuingia katika nyazifa zao kwa taaruma zao na uzoefu wao, sasa wanaingia kwa ukada wa chama.

Ukiwa mfanya biashara mkubwa na ukaonekana kusapoti upinzani ujue wafwaaaaaa.

Ukiwa ccm unaweza kumiliki hata kijiji usibughudhiwe . Ila ukitaka kuonja joto la jiwe uwe na heka kumi harafu uhamie upinzani wafwaaa. Huu ni ukaburu tu!!

Ukitaka kupata kaz sifia watawala, hapo umeula. Ukionekana kutofautiana kimtizamo ww ni adui. Huu ni ubaguzi!!

Nenda kwenye huduma za jamii! Viongozi wanaenda kutibiwa ulaya huku tukinadi haki sawa!! Kesi ya mbunge wa ccm kukamatwa na nyala za serikali analipishwa faini ya milion 130 huku mbunge wa upinzani anakata utepe wa police anafungwa jela miezi 6. Huku akitetea haki yake ya kupiga kura.
Kwanini tuwatofautishe na makaburu . Kwani makaburu walikua wanakula watu??

Niambienie ubaya gani mkubwa walioufanya makaburu ambao ccm hawaufanyi? Sion tofauti ya makaburu na utawala wa ccm. Maana mawazo ya mtu ambaye ni mpinzani wa kisiasa kwao ni mawazo ya shetan . Hawawezi kumsikiliza kamwe. Kama huo sio ukaburu nini? Nani aliye waambia wana ccm peke yao ndio wana akili?? Lini tulikaa na wapinzani na kuchukua mawazo yao kama kweli tunawaona ni watanzania na wana haki sawa na wana ccm? Nenda mpaka bungeni , wapinzani wanaweza kushauri jambo na wasisikilizwe, linaenda kwa wananchi linakataliwa linarudi bungeni na kulipangua. Je wangewasikiliza wapinzani kabla kungekua na ubaya gani. Kwann tuwatofautishe ccm na makaburu??

Tunapaswa kuamka kutafuta uhuru wa kisisa toka kwa huyu kaburu wa siasa hapa tanzania. Kama hatuon ukaburu wa kisiasa basi ujue hatujui nini tulikipigania makaburu waachie uhuru kwa watu wote South Africa.
 
Back
Top Bottom