Wanabodi,
Wanabodi nauliza, hii sumu ya siasa za ukabila na ukanda are they real au ni dhana tuu?!.
Jee Watanzania hawana makabila yao?, Lazima tukubali tukatae, Tanzania kuna dorminant tribes na makabila madogo madogo. Kati ya hizi dorminant tribes lazima tukubali kuna baadhi yake wana ukabila wa kutisha!, kuna baadhi yake wana nyodo za ajabu!, kwani iliwahi kutamkwa au kuandikwa popote kuwa watu wamakabila fulani sio hawafai kuchukua urais wa nchi hii, bali hawawezi kupewa kwa sababu matokeo tunayajua!, hivi tuu walivyo na hizo nafasi kubwa kubwa tayari ni miungu watu, wakiukwaa urais si ndio wataota pembe kabisa!. Ni general unwritten public opinion kuwa rais wa nchi hii asitokee kwenye hizi dorminant tribes!. Kuna wagombea fulani walinyimwa kura maeneo fulani kwa kuitwa wakuja!. Kuna mikoa fulani mgombea ambaye sio mzawa huitwa "chasaka" na wanakuambia kabila letu kamwe haliwezi kumchagua "chasaka"!. Jee hii ni dhana tuu ya ukabila au ndio ukweli wenyewe?.
Jee mbegu hii ya sumu kaipanda nani?, jee tunaweza kuipiga vita kwa kuikanusha tuu (denial) au tunatakiwa kuubali ukweli mchungu na kukabiliana nao (facing the problem)!.
Nauliza tuu?
Pasco