Makabidhiano ya pikipiki baina ya tajiri na bodaboda

Makabidhiano ya pikipiki baina ya tajiri na bodaboda

Mimi Sasa hivi Nina pikipiki mbili na ndio zinanisaidia kupata hela za kula.
Kwa uzoefu wangu nimegundua biashara ya bodaboda inaweza kukulipa au isikulipe pia.
Kukulipa kwake inategemea sana dereva uliyemchagua kwa ajili ya kukuendeshea chombo chako,na hapa ndio wengi huwa wanabugi.
Hapa ni lazima umpate dereva mstaarabu na anayejitambua tena ikiwezekana umpate mwenye mke na watoto,usichukue wale vijana wadogo wanaonyoa viduku utajuta,hata Kama una mkataba naye bado usumbufu utaupata tu.
Kwa maana hiyo ni vema uanze kumpata dereva kwanza halafu ndio ununue chombo,usinunue chombo kabla hujampata dereva mzuri.
Hautanunua kamwe
 
ninaomba kufahamu utaratibu wa kukabidhiana pikipiki kwa mkataba.
nimenunua kapikipiki sasa nahitaji kumkabidhi bodaboda ni utaratibu upi wa kufuatwa lengo likiwa baada ya kurejesha kwa muda kadhaa pikipiki inakuwa yakwake ahsanteni na karibu wajuzi wa mambo
Fanya mwaka mmoja tu but awe analipa 10 per day lkn wewe uchukue kwa wiki 70 ambapo kama hautakuwa na njaa utanunua pikipiki 2 baada ya mwaka 1
 
Duh! Hela nzuri hii

Kwa route au kupack sehem , maana naishi karibu na chuo(udsm) sioni kama wanaingiza hiyo helaa
Tena huko ndio inalipa sana.
Imagine ukiikodi Bajaj kutoka ubungo/mawasiliano Hadi mwenge nauli yake ni kwa wastani ni 7000 tsh.
Kwa maana hiyo ukikomaa kwa siku ukopata vichwa kumi una sh ngapi.
 
Mm nlkua naambiwa achana na hyo biashara ni pasua kichwa lkn now nko na bajaji na inafanya poa..
Tanguliza positivity..
Kwa kila mtu mmoja aliyebahatika kufanikiwa boda boda unajua ni wangap wamefilisika? Hii sio ata biashara, ni upuuz flani
 
Tena huko ndio inalipa sana.
Imagine ukiikodi Bajaj kutoka ubungo/mawasiliano Hadi mwenge nauli yake ni kwa wastani ni 7000 tsh.
Kwa maana hiyo ukikomaa kwa siku ukopata vichwa kumi una sh ngapi.
Achana na hao wa kukodi , kuna wale wa jerojero ubungo mwenge
Au ubungo changanyikeni , ndo ninaoona ngum kufikisha hiyo laki au elfu sabini kwa siku
 
Tofautisha kati ya bajaji na pikipiki bajaji ikopowa pikipiki A K A boda boda nishida
Maneno hayo eti pasua kichwa yapo pia katika bajaji na daladala
Humu usipojicomit mwenyewe utaishia kutishwa na watu kama nyie na ukute huna lolote mkuu zaidi unakatisha watu tamaa
 
Nadhani komaa tu uuze hizo pikipiki uongezee ununue bajaji moja. Ukimpa mtu mwenye familia kwa mkataba wa kiongozi wa mtaa anapoishi na kwa wakili akikuzingua unatafuta mwingine. Kwa mwaka hela yako itakuwa imerudi. Akiongeza miaka miwili ukimwachia utakuwa umeshanunua bajaji mbili
 
Kama kuna mwenye softcopy ya mkataba wa boda boda ituwekee hapa itatufaidisha wote
 
Back
Top Bottom