Majuto ni mjukuu!

Majuto ni mjukuu!

sokwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
2,022
Reaction score
1,065
Nilikuwa na rafiki yangu mtaani ambaye tulikwenda shule ya msingi pamoja, japokuwa baada ya kumaliza elimu ya msingi hakuweza kuendelea na masomo zaidi lakini tuliendelea kuwa washikaji,ikatokea wakati nipo Tz mshikaji akamtokea dada mmoja mtaani,kumbe Yule dada alikuwa muathirika wa vvu na taarifa hizo nilizipata kutoka kwa uncle wangu ambaye ni daktari. Kwahiyo uncle akaniomba nimuonye mshikaji asitembee na huyo dada, ilikuwa ni kazi ngumu kwasabab kumwambia dada anae date nae ni muathirika angeweza kuniuliza nimepata wapi taarifa? Na sio rahisi kumtaja uncle moja kwa moja kwasabab madaktari hawaruhusiwi kutoa taarifa za wagonjwa, nilichofanya nakumbuka ni kununua line ya simu mpya na kumtumia text mshikaji kuhusu issue ya huyo Demu na baadae nikaitupa line. Mshikaji akashituka sana na kuja kuniambia kuna f.a.la kamtumia text kwamba Demu anae date nae Ana ngoma akawa anadai kwamba kwann hakumfuata moja kwa moja na kumuambia, kwa vile niliona issue imeshakuwa ngumu moja nikamchana kwamba aliyetuma hiyo text ni Mimi.tukagombana sana mshikaji akidai taarifa hizo nimezitoa wapi ila nilishindwa kumuambia kwa kweli, lakini alikwenda kumuambia huyo dada na urafiki wetu ukafa kabisaa, sasa huyo dada amefariki na mshikaji ameshindwa hata kwenda kwenye mazishi yake kwa taarifa nilizipata kutoka kwa Mdogo wangu. Sasa mshikaji anapiga bia sana na kujirusha na vimwana kwenda mbele! Tahadhali unapoambiwa jambo na rafiki yako au nduguyo Uwe unasikia usiweke hisia zaidi, weekend njema.
 
tatizo vijana wengi siku ya kwanza tu tunatifuana! sasa huo ujumbe wakati unampa ukute walishacheza mechi kibao za ugenini na nyumbani!
may be it was too late aliona ameshaharibu haina maana kuachana so usimlaumu sana sokwe
 
Hata sielewi smile, ila natamani ningefanya bidii zaidi ili aachane nae huyo dada kwa kweli inasikitisha.
 
Hata sielewi smile, ila natamani ningefanya bidii zaidi ili aachane nae huyo dada kwa kweli inasikitisha.
je kama walishaambukizana ingesaidia?
 
Tahadhali unapoambiwa jambo na rafiki yako au nduguyo Uwe unasikia usiweke hisia zaidi, weekend njema.
  • Yap hili nalo neno, mwenye kusikia na asikie
 
Nashindwa hata kumpigia simu mshikaji! Hata sielewi.
 
Inasemekana demu alikuwa anatumia hila hafuati masharti, ila mshikaji sina uhakika Kama anatumia ila anajidunga sana pombe.
 
Back
Top Bottom