Majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
ban.sheria.jpg

Allan Kajembe

amka2.gif
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni mojawapo ya tume iliyopewa majukumu makubwa na muhimu, katika utekelezaji na usimamizi wa utawala bora na haki za binadamu hapa nchii.
Ni tume iliyoanzishwa na sheria yake mahususi, ambayo ni sura namba 39 ya marejeo ya sheria ya mwaka 2002 ya seria za Tanzania.
Sheria hiyo imeipa mamlaka tume hiyo kufanya kazi katika pande zote za Tanzania yaani Tanzania Bara na visiwani kama ambavyo kifungu cha 3 cha sheria hiyo kinavyosema.
Kitu kingine cha muhimu katika sheria hiyo ni matumizi ya sheria hiyo yanavyokwenda sambamba na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara), kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha sheria hiyo.
Tume hiyo imepewa majukumu mengi na ya muhimu katika kusimamia utawala bora na haki za binadamu ambazo ni pamoja na kuinua na kulinda haki za binadamu kama ambavyo zinaelekezwa na katiba yetu, pia kufanya uchunguzi kuhusu mambo yote yanayohusisha uvunjifu wa haki za binadamu hapa nchini.
Tume hiyo pia ina majukumu ya kufanya utafiti juu ya haki za binadamu na utawala bora na pia kuielimisha jamii kuhusiana na mambo hayo.
Majukumu mengine yaliyopewa kwa tume hiyo ni jukumu linalopatikana chini ya kifungu cha 6(1) kifungu kidogo cha (e) ambacho kinaipa tume mamlaka ya kumfungulia mtu, watu au idara yoyote ile, kesi mahakamani, kama itajiridhisha kulikuwa na uvunjaji wa haki za binadamu na kwamba tume itakuwa inaomba fidia kwa ajili ya mwathirika wa uvunjaji huo wa haki za binadamu.
Ina majukumu ya kuhakikisha mikataba yote ya kimataifa ambayo Tanzania inaingia kuhusiana na haki za binadamu inaridhiwa na kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo hapa nchini.
Jukumu jingine linaloendana na hilo ni kushirikiana na serikali, tume imeagizwa kushirikiana na idara na vyombo vya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Madola na vyombo kadhaa vitakavyoanzishwa kwa makubaliano ya nchi mbili au zaidi, na hata kushirikiana na taasisi za hapa nchi au za nchi nyingine katika kuhakikisha kuna ulinzi na kuinua haki za binadamu na utawala bora hapa nchini.
Tume hiyo pia ina majukumu ya kusaidia upatanishi na maridhiano baina ya pande mbili zilizo katika mgogoro ambao wameenda kupata ufumbuzi katika tume.
Tume hiyo pia inaweza kutembelea maeneo au watu walioathirika na uvunjifu wa haki za binadamu kama vile vizuizini au panapofanana na hivyo ambapo chini ya kifungu cha 6(1),(h) ya sheria hiyo, tume baada ya kufika eneo au kwa mtu huyo itafanya makadirio na uchunguzi kwa mtu/watu hao na mwisho kutoa mapendekezo yake kuhusu njia gani za kuwalipa fidia wahanga wa uvujnifu wa haki za binadamu kwa kuzingatia mahitaji ya sheria hiyo.
Pamoja na kuwa na majukumu mengi ndani ya sheria, tume imepewa mamlaka ya kutoa maoni yake kuhusiana na sheria, kanuni au miongozo yoyote iliyopo ili kuhakikisha kwamba viwango vya haki za binadamu pamoja na kanuni za utawala bora zinafikiwa na kutekelezwa.
Jukumu hili linakwenda sambamba na kutoa ushauri kwa serikali na taasisi zingine za umma kuhusiana na masuala yahusuyo haki za binadamu na utawala bora hapa nchini.
Ndugu msoamaji, majukumu ya tume hiyo ni mengi na yoye yanahusu haki za binadamu na utawala bora, aidha kama haki hizo zimevunjwa au kuna nia ya kuzivunja basi tume hiyo uhusika moja kwa moja kuchukua hatua itakayoona inafaa.
Uongozi wa tume hiyo umewekwa chini ya Mwenyekiti wa tume, ambaye kwa mujibu wa kifungu cha 7, anapaswa kuwa jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania au ya Zanzibar, au Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.
Pia tume ina Makamu Mweneyekiti ambaye kimajukumu anapaswa kutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano dhidi ya ule wa Mwenyekiti, kwa maana ya kwamba kama mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamu wake atapaswa kutoka Tanzania visiwani, kwa mujibu wa kifungu cha 7(1), (b) cha sheria hii.
Pamoja na kuwa na mwenyekiti na makamu mwneykiti, tume hii pia itakuwa na wajumbe wasiozidi watano ambao wanajulikna kama makamishna, ambao uteuzi wanaopaswa kuzingatia vigezo vya kuwa watu wenye elimu na uelewa, uzoefu kuhusiana na mambo yanayohusu haki za binadamu, sheria, masuala ya kiserikali, siasa na masuala ya kijamii.
Makamishna hawa watasaidiwa na makamishna wasaidizi na wote hawa huteuliwa na rais baada ya kupata maoni kutoka kwa kamati ya uteuzi.
Hata hivyo mtu yeyote atakayeteuliwa kuwa Kamishna, Naibu Kamishna au Mweneyekiti wa tume hiyo, chini ya vifungu vya 8 na 9 watatakiwa kuacha kazi kama wanafanya kazi katika ofisi kama mbunge, mwakilishi (kwa Zanzibar), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Spika wa Baraza la wawakilishi.
Kwa mujibu wa kifungu hicho atatakiwa pia kuacha kazi ikiwa atakuwa jaji au ofisa yeyote wa mahakama, ofisi yoyote ya umma, ofisa wa tume ya uchaguzi, au ofisa wa serikali za mitaa au ofisi yoyote ya umma.
Hata hivyo mweneykiti anaweza kutolewa katika nafasi yake kama atatangazwa mufilisi au kama atastaafu au kufariki dunia.
Kifungu hiki cha sheria hii kinaendana sambamba na matumizi ya ibara ya 129(6) ya Katiba ya Muungano.
Kamishna ambaye ataacha ofisi/kazi katika mojawapo ya ofisi zilizoainishwa kifungu cha 9(1), yaani tulivyoviona hapo juu, atarudishwa katika nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake kama kamishna.
Haya ni mahitaji ya sheria hii chini ya kifungu cha 9(2) cha sheria hii.
Kwa maelekezo ya kifngu cha 10 cha sheria hii, kamishna ataondolewa kuwa kamishna kama atakuwa anashindwa kutimiza majukumu yake kutokana na ugonjwa, tabia mbaya/utovu wa nidhamu kinyume na maadili ya viongozi wa umma, au kwa sababu nyingine yoyote itakayoonekana inafaa.
Tume hiyo pia itakuwa na katibu mkuu ambaye pia atateuliwa na rais baada ya kushauriana na tume, miongoni mwa watu wanaoongoza au waliowahi kuongoza nafasi za juu serikalini.
Katibu huyu ni lazima awe na shahada ya sheria kutoka katika chuo kikuu kinachotambuliwa na serikali na ana uzoefu wa miaka mitano ya uongozi katika taasisi za umma, au amefanya kazi za sheria kwa maana ya uwakili, kufanya tafiti au kufundisha sheria, kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
Tume hii inaweza kufanya uchunguzi kwa kuamua yenyewe au baada ya kupokea malalamiko kwa mujibu wa sheria hii toka kwa mtu aliyeathirika na uvunjaji wa haki zake za kibinadamu ambapo tume itafanya uchunguzi kwa niaba ya mtu huyo, pia inaweza kupokea malalamiko kutoka katika kikundi cha watu au jumuiya.
Hata hivyo mamlaka ya tume hii katika kufanya uchunguzi imewekewa mipaka kwa kutumia Ibara za 46 ya Katiba ya Jamhuri na ibara ya 36 ya Katiba ya Zanzibar, haitakuwa na uwezo wala mamlaka ya kumchunguza Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pia tume imewekewa mipaka ya kutochunguza shauri lililopo mahakamani au katika baraza lolote lenye mamlaka ya kimahakama, kuhusu masuala yanayohusu kazi kati ya serikali ya Tanzania na serikali za nje au kampuni au shirikisho lolote la nje, au kuchunguza suala lolote linalohusiana na msamaha wa rais.
Katika mambo hayo, tume haitakuwa na mamlaka ya kuchunguza kitu chochote isipokuwa kama rais ataelekeza vinginevyo, kama ambavyo kifungu cha 16(3) cha sheria hii kinavyoelekeza.
Malalamiko yanaweza kupelekwa katika tume hii kwa njia ya mdomo au kwa maandishi na yatatakiwa kujazwa katika fomu maalumu zinazopatikana katika tume hiyo.
Inapotokea kama malalamiko yatapelekwa na mtu aliyeko chini ya ulinzi kama jela au mahabusu au kama ni mgonjwa aliyeko hospitali, basi malalamiko yatapelekwa haraka na mtu atakaye pewa na mtu huyo.
Malalamiko hayo yanaweza kupelekwa na mtu binafsi au na kampuni, iwe imesajiliwa au la.
Mtu anayepeleka malalamiko yake katika tume, anaweza kuwakilishwa na wakili katika malalalmiko yake, na kwamba baada ya kupokea malalamiko hayo, tume itamuita mlalamikiwa au mtu yeyote aliyekaribu naye na kwamba tume itatoa muda na nafasi ya kutosha kwa kila upande unaohusika na malalamiko hayo.
Tume hii pia ina uwezo wa kumwamrisha mtu kwenda kwa njia ya samansi kumhoji mtu akiwa chini ya kiapo kwa malalamiko yaliyopo mbele yake na pia kutoa amri ya muda mfupi ikisubiriwa kumalizika kwa shauri zima.
 
Tatizo ya Tume hizi zote hatujui viongozi wake walipatikanaje? Bunge ni lazima lihusishwe katika teuzi ihizi na wahusika waziombe kupitia vyombo vya habari ili kutoa fursa sawa kwa kila mtu.......................
 
Back
Top Bottom